Tanzania yashindwa kesi, yakubali kuilipa fidia Kampuni ya Montero Tsh. Bilioni 71 kwa kukiuka Masharti ya Mkataba

Tanzania yashindwa kesi, yakubali kuilipa fidia Kampuni ya Montero Tsh. Bilioni 71 kwa kukiuka Masharti ya Mkataba

Hiyo ni michongo ya watu. Hawa wanyonyaji kipindi wanafurushwa walinywea na kukubali yaishe. Wamesubiri hadi nchi kashika bibi yao saivi ni kujilimbikizia tu mimali.

Hadi sasa kesi zaidi ya 5 hakuna hata moja tulioshinda, ni vikampuni uchwara vinajitokeza na kudai fidia na cha ajabu wanashinda na hela wanalipwa right away. Huu ni uhuni tunafanyiwa kama nchi.
🤣Hio ni michongo ya kupiga hela bila shaka. Mtu kafukuzwa miaka 5 nyuma akatulia tulii maana alijua amecheza rough na hizo kampuni nyingi ni camouflage za Watanzania wenzetu. Leo hii wanaibuka sababu mazingira ya kupiga hela kupitia kesi ni rahisi.

Nakumbuka Magu alipiga marufuku mchezo wa wanasheria wa serikali kushindwa kesi na kulipa fidia kwa style hio maana walikuwa wana migao kwenye hizo fidia. Sahizi huo mchezo umerudi tena. Ni kama organized crime money.
 
Hatari sana kuwa na rais wa hovyo.Tungekuwa na bunge linalojitambua lingemuondoa Kwa kutokuwa na Imani Naye lakini Kwa kuwa hatuna bunge inabidi tuvumilie tu Nchi yetu kufilisiwa na haya makampuni ya kitapeli
 
Baba wa mikataba Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi aliyekuwa mshauri mkuu wa rais wa awamu ya 5 na sasa waziri wa sheria katika serikali ya rais wa awamu ya 6.

Hadi sasa jumla ya fidia nchi ya Tanzania ilizolipa inabidi wanaJF tufungue uzi maalum tujue uzito wa sheria na maamuzi ya wanasiasa wetu yameligharimu nchi kiasi gani na pia kama kuna faida ni kiasi gani nchi imevuna kutokana na maamuzi hayo ya kuvunja mikataba.
 
Hatuna Watalaamu wa sheria,tuna wapiga kelele majukwani.unajua mahakama za kimataifa ni tofauti na Mahakama ya hakimu mkazi pale kisutu au sijui magogoni,pale ambapo Jaji anafikiria mara mbili mbili kabla ya kutoa haki hasa kama kesi inaihusu serikali.wakisha maliza Law skuli basi wanajionadaga ni wansheria wa dunia.Uwezo wa wanasheria wetu ku-review international contract/Agreement ni mdogo sana. Wanatuingiza hasara.
Lakini pia wale wa kwenye negotiation panel wako weak sana sana.Mikataba ina kuwa na vifungu tata wao wanaipitisha hivyo hivyo tuu kwa kuwa hawezi kubishana sana kwa kingereza,kichwa kina pata moto
Tundu Lissu alitoa ushauri mujarab kabisa. Ila Dikteta akamshindilia risasi 16. Na Mungu kamuepusha Lissu na kifo ili aje kutusuta kwa kupuuza ushauri wake
 
Ndivyo mikataba inavyokuwa. Makubaliano lazima yafikiwe. Ni kawaida dunia nzima
Huo ni ufisadi unaofanywa nà ma CCM, yanaandikisha mikataba ya uongo halafu yanaenda mahakamani kujifanya yameshindwa hàlafu mnachota hela mnagawana.
 
Back
Top Bottom