Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi 7 zinazotarajiwa kuwekewa vikwazo vya kuingia Marekani

Kwa vyovyote mbinyo wa demokrasia uliotamalaki na utawala mbovu kama huu wa vibwetere wa bongo ndiyo sababu za vikwazo hivyo. 'Kuukataa ushoga' itakuwa kisingizio cha wanasiasa uchwara wa CCM mafisadi wa mali amali na utu wa Watanzania. Chini ya utawala wa Trump ushoga na usagaji umepigwa vita na madhara yake kuzigusa nchi nyingi ikiwemo Tanzania. Trump amefuta ruzuku zote katika miradi ya uzazi wa mpango, ushoga na usagaji na sasa gharama hizo zinabebwa na nchi husika. Kwa hiyo kusingizia eti vikwazo vitakuwa vinasababishwa na kuukataa ushoga ni uhayawani!
 
chonde chonde hivyo vikwazo vya kiuchumi tafadhali sana visihusishe uingizwaji wa kondom nchini maana dah mabaharia watazama,
tumeshindwa hata kuwa na kiwanda ya ndomu
 
Ni sahihi! Nchi zinazofadhili ugaidi wa kuteka watu na kupoteza watu ni sahihi ziwekewe vikwazo!
 
Kwakua watu wengi watanzania sio wafatiliaji mtawadanganya sababu inayo taka kupelekea watanzania kuzuiwa kuingia marekan sio sababu ya ugaid wala serekal ya magufuli msipende kupoteza watu na kumbebesha mzee wa watu mizigo asio stail wamarekani wanampango wa kutuziwia tusiingii marekan ni sababu ya watanzania weng wakienda kule Hua wanazidisha muda wao wa visa pia wengine hutoweka kabisa so hii ndio habar kamili na kingine marekan kule sio pepon na kingine hawato nyimwa visa kabisa ila wataweka ugumu kuipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itabidi kina JK na Mkapa waingilie kati kumsaidia Ngosha.Ni kama vile maji yameshazidi unga.Ushauri wa hao wazee wastafu ni muhimu sana.Hii Tanzania ni yetu sote yasijetukuta ya Zimbabwe!
 
Umeandika nini kwa mfano!
 

Nani anachekelea kupigwa mabomu kwa Wakenya!?. Naona hauna facts Watanzania sio watu wa type hiyo.
 
Hatuwezi kuwakatza. Dola yao tunaipenda sana kupitia watalii wa USA, investors etc. Hela yetu tshs bado haina nguvu
Basi sawa acha waje wao kama wao hawataki...nakumbuka zamani kuna basi la Tanga silitaji nyuma walikua wameandika "KAMA HATAKI NIPE MIYE"
 
Namba kubwa ya vijana wa Tanzania inajiingiza ISIS, Al-Shabab ect. Yote haya yanasababishwa na kukosa ajira.

Kuwekeza katika nguvu kazi ya vijana ni muhimu.
Huko ISIS na Al-Shabab wanalipaje wao hadi vijana waende huko?!
Wanapokea na waumini wa Zamaridi na wa Kakobe au vijana wapi wana qualify huko?!
 
Nani anachekelea kupigwa mabomu kwa Wakenya!?. Naona hauna facts Watanzania sio watu wa type hiyo.

Utakua mgeni kwenye mada zinazohusu Wakenya, njoo kule uone kila bomu likilipuka, humo comments hutiririka za kukejeli na kuchekelea, na usiseme Watanzania sio wa type hiyo maana hakuna watu wanaitwa Watanzania, hizo ni jamii zlikusanywa na mzungu akachora mpaka na kuwaita Watanzania.
Alikuta watu tofauti na mila na tamaduni zao kisha akawakomba pamoja na kuwapa nchi. Kila binadamu huwa na mawazo yake binafsi, unless kama baada ya mzungu kuwakomba pamoja aliwapa maagizo muwe mnawaza kwa kutumia ubongo mmoja.
 
Huko wanapata $200 kwa mwezi na chakula bure
Hahaha Paund au Dollar?! $200 kweli?! hao watakuwa wendawazimu, huko wanabeba box au kuna kazi gani huko?!
Yani laki 4 kwa mwezi?!
Wanalipwaje cash au wana deposit kwenye account zao bongo?! Maana kulipwa vitani unaitunza wapi hiyo pesa, au wanajitolea tu mnawasingizia haya malipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…