Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi 7 zinazotarajiwa kuwekewa vikwazo vya kuingia Marekani

Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi 7 zinazotarajiwa kuwekewa vikwazo vya kuingia Marekani

Serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli nini kimetokea? Hadi tufikiriwe kuwekewa vikwazo?

Au Marekani wanatuonea wivu tu?

*******************

A senior Trump administration official said that countries that failed to comply with security requirements, including biometrics, information-sharing and counter-terrorism measures, faced the risk of limitations on U.S. immigration

*******************
Bablai mbona unaonekana kama hujielewi flani hivi? Au ndio wale inaosemekana wanaiombea Tanzania MEMA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wajinga wanafikiri hivyo vikwako vitamuumiza Meko au vitaitoa CCM madarakani.

Huko Zimbabwe wanaheshiana?
 
Mbona ndio tunako elekea huko.Tutafika tu kwenye vikwazo vya kiuchumi. Tushaelekezwa huko na Magufuli. ZIMBABWE..!
 
Sitashangaa nikiona kwamba Tanzania iliongezwa kwenye orodha kimakosa na bila hata kuijua nchi iko wapi. You see, huyo Drumpf na serikali yake ni kwamba hawajui chochote au kidogo sana kuhusu Afrika. Kioja kimoja kilitokea mwaka jana waliorodhesha Wakanda kama preferred trading partner wa US kwenye tovuti ya serikali.
 
Daniel Agger,
Kama unataifa lako binafsi nahisi ni vyema ukaenda kuishi huko, Tanzania mama yetu hatujafikia hatua hiyo ya kuikana na kuitabilia mambo yasiokua na tija kama haya.

Punguza chuki mzee hakuna taifa lililo tamu kila nchi inachangamoto zake,hata wewe hapo ulipo kuna watu wanaokuzunguka wanakereka na namna unavyoishi nao lakini wanakuvumilia kulingana n a mapungufu yako
 
Mtoto anamshtaki baba yake kwa watesi wake ili kumkomoa ila nyumba anayoishi na shibe apatayo inatoka mikononi mwa baba yake.

Hivi hivyo vikwazo vya kiuchumi vitamuumiza nani zaidi? tuwe tunafikiria sana tusije kuwa ka wana wa Gaddafi
 
Wamarekani wangeweza pia kutuuliza ni nani na nani wanatuendeshea ugaidi dhidi ya RAIA ili watumie njia kama ile walifanya kwa Noriega wa Panama. Walituma makomando na kumteka kwenda kumshtaki kwao. Sisi tukiwapa orodha yetu hawashindwi.

Ila tu wasitumie Drone kwani zitamaliza na ndugu zetu wema walio jirani. Nimeandika hii kama utani, lakini namaanisha kuwa watusaidie kuwatoa madarakani kwani mfumo wa kura unakuwa mgumu maana wao wanatumia dola kupora kura.
 
Huu ni ukweli
Makusudio ya Vikwazo vutavyowekwa Ni kutaka kuwaamsha watz wamtguafute mchawi wa matatizo wanayoyapitia sababu hasa ni nani. Sasa kama vikwazo hivi tutawekewa, ni wazi fisiem itaadhibiwa na wananchi kupitia kura.
Kwani kuipigia kura fisiem ni inamaana wanakubali vikwazo viendelee,

Na wakitokea watz kuipigia kura fisiem na kuipa ushindi nitaungana na wale wanaosema kuwa mccm yatosha kuwepo ktk rekodi ya maajabu ya dunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto anamshtaki baba yake kwa watesi wake ili kumkomoa ila nyumba anayoishi na shibe apatayo inatoka mikononi mwa baba yake.

Hivi hivyo vikwazo vya kiuchumi vitamuumiza nani zaidi? tuwe tunafikiria sana tusije kuwa ka wana wa Gaddafi
Kodi zetu ndicho kiburi cha watawala
 
Reuters - The Trump administration is planning to add seven countries - Belarus, Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar, Nigeria, Sudan and Tanzania - to its travel ban list, U.S. media reports said on Tuesday.

=======
Tanzania ni moja ya nchi kadhaa ambazo huenda zikakumbwa na masharti maalum kwa raia wake kupewa visa kuja Marekani, kwa mujibu wa rasimu ambayo imeandaliwa na utawala wa Trump kuhusu hatua mpay za uhamiaji.

Rais Donald Trump huenda wiki ijayo akapitisha marufuku ya kusafiri ambayo itazikumba nchi saba nazo ni Tanzania, Sudan, Nigeria, Eritrea, Kyrgyzstan, Belarus na Myanmar, vyanzo karibu na suala hilo vimesema.

Rasimu ambayo imeandaliwa itaweka masharti ya uhamiaji kwa nchi hizo lakini siyo marufuku ya moja kwa moja kwa raia wa mataifa hayo kuingia nchini Marekani. Masharti hayo huenda yakawakumba maafisa fulani fulani wa serikali, kwa mfano, wale ambao wataomba aina fulani ya visa.

Kwa mujibu wa gazeti la Politico nchni Marekani, masharti yoyote mapya huenda yakaleta mivutano ya uhusiano kati ya Marekani na nchi ambazo zinalengwa, katika mpango huu mpya, ambapo baadhi ya nchi zimekuwa ni mshirika wa Marekani katika mapambano dhidi ya Ugaidi.

Rais Trump katika mahojiano na The Wall Street Journal akiwa Davos, Uswizi kuhudhuria kikao cha uchumi amesema kuwa kuna mataifa zaidi ambayo yatakumbwa na masharti maalum ya kusafiri kuja Markeani, lakini alikataa kutoa orodha ya mataifa hayo.

Msemaji wa White House, Hogan Gidley hakutaka kufafanua zaidi kuhusu mipango ya kuongeza nchi nyingine katika marufuku ya kusafiri, lakini alisema hatua hiyo ambayo awali iliyakumba baadhi ya mataifa yenye waislamu wengi imekuwa na mafanikio makubwa katika “kuilinda nchi yetu na kuongeza wigo wa usalama kote duniani,” ameongeza Gidley.

Trump alitia saini marufuku ya kusafiri kwa wananchi wake kupewa visa kuja Marekani, Januari 27, 2017 wiki moja tu baada ya kuingia madarakani. Amri hiyo awali iliwanyima visa Marais kutoka mataifa saba yenye waislamu wengi. Baadhi ya mataifa hayo ni Iran, Libya, Somalia, Syriana Yemen. Chad ilikuwemo lakini iliondolewa katika orodha ya awali.

Screenshot_20200123-075906.jpeg
Screenshot_20200123-081749.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua haya matawala bogus yanaringa sababu kuna mijitu bado unaichagua? so shoka likiwa shingoni hayo majitu yanaowachagua akili zitakaa Sawa! hukweli hakuna mtu mwenye akili anaetamani vikwazo Ila hakuna njia nyingine yakuwaamsha wapuuzi wanaochagua watawala wa hovyo
Daniel Agger,
Tutaangamia usiombe vikwazo vya kiuchumi...haya majitu yenyew hayatapata shida hapa ndo siwaelew marekan wanashindwa nin kufocus na haya maviongoz?Kwa sabab vikwazo vya kiuchumi vinawaaathiri wananchi na sio haya maviongoz mabinafs.Sema yote lakin usiombe economic sanctions

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Travel ban kama itakuwa kwa some indivifuals basi iwe na kwa watoto na familia zao kama wako katika mfumo mmoja na iwe extended na EU countries basi litakuwa pigo tosha hilo. Mimi nashangaa namuona DAB anajikoga kwenye mitandao akiwa US, wanampaje visa mtu kama yule?
Kaenda kuomba majuzi wamemnyima anajua na nilimpokea hapa reception.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa, safari bado inaendelea hivyo yetu macho, masikio na uhamuzi.
 
Back
Top Bottom