Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi 7 zinazotarajiwa kuwekewa vikwazo vya kuingia Marekani

Ni kweli ushauri wa Dr.Bushiru ni mzuri sana na wa kuzingatia mkuu.View attachment 1331560

dodge
Sijaelewa umamanisha nini?
Anyway siko hivyo unataka niwe,nami sio mfuasi wa Chama chochote cha siasa.
Ni mtanzania huru,maelekezo ya Ndugu Bashiru ni kwa wafuasi wa Chama chake.
Nanyi kama kuna maelekezo ya Chama chenu myafuate.
 
Ujue kutofautisha ufadhili na msaada
[emoji1][emoji1][emoji1] Kwahivyo msaada wa hela za kununua madawati na madawa, kutoka kwa mabwana zenu mabeberu ni sawa na ufadhili ambao Sportpesa huwa wanawapa Yanga na Simba? Itabidi basi watz wote muanze kuvaa jezi ambazo zimeandikwa kwa mbele, Mabeberu Ltd, 'Educating Dona Kantri, Since 1961'.
 
Nimeandika hii kama utani, lakini namaanisha kuwa watusaidie kuwatoa madarakani kwani mfumo wa kura unakuwa mgumu maana wao wanatumia dola kupora kura.
Hata Libya walisaidiwa na hao wakubwa kumtoa Ghadaffi matokeo yake leo yanaonekana.

Syria pia mwanzoni walisaidiwa kumg'oa Assad matokeo yake nchi imeharibika na Assad yupo bado.

Hatujafika huko pa kusaidiwa maana nchi yetu ni salama Sana. Usiruhusu siasa zikupofushe.
 
Nimesikia uvumi kuwa Trump anakusudia kuiingiza nchi yetu kwenye orodha ya nchi za kufungiwa (Travel ban) watu wake kusafiri kuingia Marekani.

Bara la Africa siku zote limekuwa likipitia changomoto kubwa hasa kuanzia kupata Uhuru na hatimaye baada ya kupata Uhuru.

Walitupa Uhuru kama danganya toto kwakujua watakuja kututawala kwa namna nyingine ambayo kumiliki Uchumi wetu kupitia vibaraka na Makuadi wao.

Prof Kitila Mkumbo alipata kulielezea hili kwamba vita ngumu ambayo tunakabiliana nayo Africa na hasa Tanzania ni Vita ya Kiuchumi na sio ile ya Bendera.

Trump anazunguka "Mbuyu" lakini uhalisia unajulikana tu,Toka Rais John Magufuli aingie madarakani na hasa kubadilisha sheria zote za madini ambazo zilikuwa kandamizi kwa Nchi yetu.

Ushauri wangu kwa AU sasa ni kutekeleza kwa vitendo Ushauri wa Marehem Gaddaf kwamba huu umoja sasa lazima uwe sauti moja ili kuzuia huu uonevu ambao umekuwa wa nenda rudi kila uchao kana kwamba hatuna Viongozi.

La mwisho Rais wetu mpendwa Dr John Magufuli endelea kuchapa kazi sie Wananchi wako tupo pamoja na wewe Daima

Alex Fredrick

Dar es salaam



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli OYEEEEeeeeh

#waambiehapakazituu

yess BiShoo haswaaAaa
 
Trump na Republican wana pinga ushoga acha kukariri maisha na ujinga
 
umoja sasa lazima uwe sauti moja ili kuzuia huu uonevu ambao umekuwa wa nenda rudi kila uchao kana kwamba hatuna Viongozi
Kunyimwa kuingia Marekani ni uonevu??
Acha kulia lia wakati utawala wa awamu ya tano imepoteza, imefungulia mashtaka ya kughushi waandishi, wanasiasa na hata mwananchi yeyote anaepiga tuu picha kuonyesha kero zinazotukabili huku mtaani
 
Acha ushamba ndugu, unamjua trumpet wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi na Tanzania inaweza kuwekea raia wa marekani vikwazo vya kuigia nchini Tanzania ili ngoma iwe droo
 
Sportpesa sio wafadhili,sportpesa ni wadhamini wa simba na yanga

Ni vizuri pia ukijua tofauti ya ufadhili na udhamini
 
Sportpesa sio wafadhili,sportpesa ni wadhamini wa simba na yanga Ni vizuri pia ukijua tofauti ya ufadhili na udhamini
Unaumwa. Ila acha yaishie hapo maanake nyinyi watu wa ID mbili mbili huwa mna matatizo ya ajabu ajabu.
 
Unasema hivyo kwa sababu wanaokuhusu hawajaguswa ukaona uchungu na maumivu.
Kuna watu wamepotezwa, kusjambuliwa, na kufanyiwa unyama mkubwa unadhani wao wanasubiri eti hadi wawe wengi ndio watasikia uchungu?
Hao Libya ni yao, sisi tuna yetu
 
Statistically, Watanzania wachache sana wanakuja USA kwa mwaka. Kama hiyo ingekuwa sababu, nchi zenye watu wengi wanaokuja USA zingejaza list hii.

Serikali ya Marekani hawana rekodi za watu wanao overstay visa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Suala sio wingi wa watu wanaokuja, ila asilimia ya wanaopitiliza visa, mnaweza kuja milioni kumi kwa mpigo, ila kila mmoja akatoka ndani ya muda wa visa, lakini pia mnaweza kuja elfu moja tu, ila mia nne mkajificha ndani kwa ndani.
Rekodi za watu wanao-overstay mbona kazi rahisi tu, just a simple database query, kila mmoja huandikwa sikua anayoingia na siku anazopewa.
 
Watanzania wengi tumepata na mstuko tuliposikia kuwa Rais Donald John Trump anaingalia Tanzania kwa jicho la darubini kuhusu kupiga marufuku baadhi ya hati za kusafiria kwenye nchi hiyo.

Tumesikia kauli ya Prof Kabudi akilia lia kuwa vikwazo vyote lazima vipitie baraza la usalama la umoja wa mataifa , Prof Kabudi atambue kuwa kuna mataifa makubwa duniani yamewekewa vikwazo na Marekani bila vikao vya baraza la usalama la umoja wa mataifa . Moja wapo ya nchi hizo ni Urusi na Iran. Haya ni mataifa yenye nguvu duniani.

Tujiulize kulikoni TANZANIA , kwanini i isiwe Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, au Zambia.Tujiulize watanzania maswali haya muhimu , Je nchi yetu imekosa nini mpaka Trump atupe tahadhari . Je Tanzania imekuwa kitua cha kuzalilisha magaidi, Je nchi yetu inaheshimu haki za binadama, Je nchi yetu iko sambamba na misingi ya demokrasia. Tukipata majibu ya maswali haya tutajua tunapoelekea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…