Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi zitakazopigwa Ban kuingia Marekani mara tu Trump atakapoapishwa!

Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi zitakazopigwa Ban kuingia Marekani mara tu Trump atakapoapishwa!

Screenshot_20241203-121555_1.jpg
 
Wakuu,

Nadhani kutokana na mambo yanayoendelea nchini image ya taifa imezidi kuchafuka.

Hivi karibuni nimekutana na listi ambayo inaonesha orodha ya nchi ambazo zinaweza kupigwa ban kuingia Marekani iwapo bwana Trump ataapishwa and yes Tanzania tumo.

List hiyo imetolewa na Cornel University, chuo kilichoanzishwa mwaka 1865 na katika bandiko lao wameonesha orodha ya nchi ambazo iwapo Trump ataingia basi kuingia Marekani itakuwa ni ndoto.

Katika orodha hiyo, Tanzania tumewekwa kwenye kundi moja na Kyrgyzstan, Nigeria, Myanmar, Sudan, Tanzania, Iran, Libya, North Korea, Syria, Venezuela, Yemen, and Somalia.

Hivi kweli leo sisi ni wa kuwekwa kwenye kundi moja na Myanmar, Sudan na North Korea?

Ile Royal Tour ilikuwa na kazi gani kama hata image ya nchi haijasafishika na mambo yako vile vile kama 2017?
Kwanza kabisa hawa wanapiga ramli kusema hili linaweza kutokea kwa sababu lilitokea Trump alipokuwa rais.

Trump mwenyewe hajasema kitu.

But let us entertain this "what if?" game. Wasiwasi ndiyo akili, lakini wasiwasi sana siyo dili.

Pili, Trump akifanya hivyo, nitawashukuru wale Watanzania-Wamarekani waliojitoa akili na kumpigia kura. Niliwaambia huyu mwehu hatabiriki si mtu wa kumpa nuclear codes.

Tatu, Watanzania wanatakiwa kuacha kupashobokea Marekani kama mbinguni.

Trump akipiga ban Tanzania na nyie Tanzania pigeni ban Wamarekani wasiingie Tanzania. Najua mnapenda hela zao za utalii, lakini jitoeni akili muongeze Wachina na wazungu wa Ulaya, halafu tuone kama mtakufa. Mkifanya hivyo Wamarekani wote wanaotaka kuja Serengeti, Kilimanjaro, Zanzibar na Selous watamuwashia moto Trump. Pigeni mpaka sisi ndugu zenu wenye uraia wa Marekani tusiingie Bongo, halafu angalieni wale watu wa mashauzi ya kuja Bongo mara nne kwa mwaka watakavyochakalika kumfanya Trump aondoe hiyo ban.

Diplomacy is driven by reciprocity.
 
Hii siasa chafu/utekaji/mauaji vinatuharibia kimataifa.
Ccm wajitathmini.
Kitendo cha kuunganishwa na hizo nchi tayari ni doa.
Tuache ujuaji.
Mkuu,

Mpaka sasa hakuna list yoyote Trump aliyoitaja.

Hicho chuo kinapiga ramli kutokana na uzoefu wa list kutoka urais wa Trump uliopita.
 
Kwa imani zetu. Lakini tunaweza kwenda nchi nyingine. Kama mtu hakutaki kwako kwanini ulazimishe? Ni kujipendekeza

Hii ndiyo kanuni yangu ya maisha, silazimishi kwenda nisipotakiwa.

Kuna dada yangu mmoja mdogo wa mwisho kwetu, alienda ubalozi wa US kuomba visa aje kutusalimia huku US. Ilikuwa likizo yake ya kazini huko Tanzania.Akawaonesha documents zote ubalozini, barua ya mualiko, barua ya kazini, documents za ties Tanzania, etc.

Ubalozini wakaanza kumzingua maswalii meengi ya ajabu. Katikati ya maswali yao ya kishenzi, bidada akakasirika, akasema kama mnafanya US kwenda maswali yote haya, nishaghairi kwenda naomba pasipoti yangu, naenda kusalimia tu safari yenyewe haina umuhimu hivyo.

Yule counselor kusikia hivyo mwenyewe akaona aibu, akampa visa yake.

Kuanzia siku hiyo huyo dada hajawahi kusumbuliwa visa ya US.

Trump anatakiwa kukutana na watu jeuri wa kumwambia kama mnatupiga ban na sisi tunakupiga ban.

Mjamaica anakwambia "Me no beg no friend".

Siombelezei urafiki.
 
Mkuu,

Mpaka sasa hakuna list yoyote Trump aliyoitaja.

Hicho chuo kinapiga ramli kutokana na uzoefu wa list kutoka urais wa Trump uliopita.
Kuna Ubaya wowote ikiwa Tanzania itapigwa Ban kutokana na uchafu unaofanyika nchini mwao? Hizi juhudi unazozifanya kuzuia ban kwanini usizielekeze kuzuia Utekaji na mauaji?
 
Jiongelee wewe, and for the record almost vitu vingi mnavyotumia today vinatoka kwao,
Mna viwanda au uchumi wa kuwa match?
Vitu gani vinavyotoka kwao bwashee! Tuanze na magari.... Ni asilimia ngapi yanatoka marekani? Twende kwenye chakula, Madawa, Mali ghafi katika ujenzi (chuma n.k). Sijui niendelee au niishie hapo.

Akitupiga ban Mjapani, mchina, India na Uturuki ningesema tumekwisha, lakini Marekani ahhhhh!
Kwanza MRUSI atafurahi sana na hiyo ban, maana ni advantage kwake.

Tutachokosa Tanzania toka marekani ni Coca, Pepsi na McDonald. Hii inamaanisha watatusaidia kuimarisha Afya zetu. Ugonjwa wa sukari utapungua.

Ndugu, mmarekani hana Jeuri sana kama zamani, siku hizi Tech imekuwa sana katika nchi nyingi.
 
Kuna Ubaya wowote ikiwa Tanzania itapigwa Ban kutokana na uchafu unaofanyika nchini mwao? Hizi juhudi unazozifanya kuzuia ban kwanini usizielekeze kuzuia Utekaji na mauaji?
Kwanza kabisa hakuna popote nilipozuia ban yoyote.

Nimesema wakiwapiga ban na nyie wapigeni ban tu, which is reciprocity, a central theme in diplomqlacy.

Pili, kupiga ban nchi nzima kwa sababu ya matatizo ya utekaji na mauaji yanayofanywa na watu wachache ni ujinga.

Kama issue ni utekaji na mauaji, kwa nini wasipigwe ban hao watekaji na wauaji? Mbona Mike Pompeo alishaanza kwa kumpiga ban Makonda? Kwa nini wapige ban nchi nzima kwa kuweka mtego wa panya unaonasa wanaotakiwa na wasiotakiwa wakati wanaweza kulipiga ban baraza zima la mawaziri na rais na mtandao wake wa watekaji?
 
Hii ndiyo kanuni yangu ya maisha, silazimishi kwenda nisipotakiwa.

Kuna dada yangu mmoja mdogo wa mwisho kwetu, alienda ubalozi wa US kuomba visa aje kutusalimia huku US. Ilikuwa likizo yake ya kazini huki Tanzania.Akawaonesha documents zote ubakozini, barua ya mualiki, barua ya kazini, documents za ties Tanzania, etc.

Ubalozini wakaanza kumzingua maswalii meengi ya ajabu. Katikati ya maswali yao ya kishenzi, bidada akakasirika, akasema kama mnafanya US kwenda maswali yote haya, nishaghairi kwenda naomba pasipoti yangu, naenda kusalimia tu safari yenyewe haina umuhimu hivyo.

Yule counselor kusikia hivyo mwenyewe akaona aibu, akampa visa yake.

Kuanzia siku hiyo huyo dada hajawahi kusumbuliwa visa ya US.

Trump anatakiwa kukutana na watu jeuri wa kumwambia kama mnatupiga ban na sisi tunakupiga ban.

Mjamaica anakwambia "Me no beg no friend".

Siombelezei urafiki.
Tunapaswa kuwapotezea. Twende nchi nyingine tatizo tumezidi kujipendekeza
 
Kwako haya mauaji yanayofanyika ni jambo la Kawaida?
Ni kweli yapo na yanasikitisha lakini sidhani kama Trump au marekani wanajali maisha ya waafrika hasa Trump. Leo Biden yuko Angola, huko Kuna mapungufu mengi ya uhuru wa kisiasa lakini kaenda sababu za kiuchumi. Makampuni yao ya mafuta yako huko miaka.
 
Tunapaswa kuwapotezea. Twende nchi nyingine tatizo tumezidi kujipendekeza
Kuna miaka ya nyuma ya utawala wa Nyerere, Wajerumani walitupa msaada wa kuweka mtandao wa nyaya za simu, nafikiri ilikuwa Tanga.

Basi wakagombana na Nyerere mambo fulani, nafikiri ilikuwa siasa za Afrika Kusini, siku nyingi kidogo nimesahau details, lakini walikuwa wanataka kumpanda kichwani Nyerere kwa sababu wamempa msaada, wakafikiri Nyerere atawaogopa.

Nyerere akapandisha kichaa chake cha Kizanaki, akawaambia msifikiri mnaweza kutupangia siasa zetu kwa sababu mmetupa msaada wa simu tu, kwanza simu zenyewe hatuzihitaji kihivyo.

Nyerere akang'oa zile nyaya za simu na kuendelea na siasa zake alivyotaka yeye.

Trump akikutana na marais watatu watano wa Afrika kama hivi atashusha kende zake mwenyewe.
 
Una miaka mingapi chifu ?
Hakuna kitu bora kama mahusiano na watu au taifa kwa taifa, hali ya usalama nchini ni tete sasa si unakuwa unaleta taharuki kwa watu.
Nani alikwambia mahusiano na Marekani yanaongeza usalama wa nchi yako? Ni kinyume, hao ni watu wa pesa tu na kugawa silaha. Uwape kama Mabutu alivyofanya na mwishowe wakikuchoka watakutosa na kuiingiza nchi yako katika vita, ili wachukue bureee malighafi bila mikataba. Mfano Afghanistan, Libya haijapoa mpaka leo, Iraq (Sadam anatengeneza bomu la Nuklia/uongo), Syria n.k.
 
Kwani bila wao kuna chochote unaweza mkuu?

Wanakupa ARV, chandarua, madawa na kuna baadhi ya vyoo vya primary vina logo yao kuwa wametusaidia

Wanakupa pesa ujenge hizi SGR

Wanakupa pesa za mikakati ya kuzuia na kupunguza umasikini, barabara, madaraja na vivuko

Kiufupi mkuu hakuna jambo lolote utafanya bila wao.
Hujui kitu kimoja, wao wnatuhitaji zaidi kuliko tunavyowahitaji. Ukikataa mkopo wao kama Gadafi alivyokuwa akifanya ni dhambi kubwa na utatoka tu. Hujui jinsi wao wanavyofaidika kwa nchi yako kwenda kukopa kwao.

Kalaga baho!
 
Kwani tusipoenda marekani tutakufa?
Hii ndio inawapa jeuri hao wazungu kuona kuwa bila wao si hatuwezi.
Kweli kabisa bila wazungu hatutoboi.kama akili zetu zinatutuma kutekana,kuuana,wizi,uchawi,uchu wa madaraka,umbumbumbu,ujinga nk halafu mseme bila Marekani mnatoboa wapi bwana.sisi ambao akili zetu zinaweza ngono hata kutengeneza chupi hatuwezi halafu mnasema mnatoboi kwa robo gani hilo?
 
Kwani tusipoenda marekani tutakufa?
Hii ndio inawapa jeuri hao wazungu kuona kuwa bila wao si hatuwezi.
Soma tena ulichoandika halafu uulize, symbion, vyandarua, condom, huduma ya mama na mtoto, na fedha za USAID, ikiwemo mashirika la Amref nk, na Kamala Hariss alikuja bongo kufanyaje! Do you guys think?
 
Hii ndiyo kanuni yangu ya maisha, silazimishi kwenda nisipotakiwa.

Kuna dada yangu mmoja mdogo wa mwisho kwetu, alienda ubalozi wa US kuomba visa aje kutusalimia huku US. Ilikuwa likizo yake ya kazini huko Tanzania.Akawaonesha documents zote ubalozini, barua ya mualiko, barua ya kazini, documents za ties Tanzania, etc.

Ubalozini wakaanza kumzingua maswalii meengi ya ajabu. Katikati ya maswali yao ya kishenzi, bidada akakasirika, akasema kama mnafanya US kwenda maswali yote haya, nishaghairi kwenda naomba pasipoti yangu, naenda kusalimia tu safari yenyewe haina umuhimu hivyo.

Yule counselor kusikia hivyo mwenyewe akaona aibu, akampa visa yake.

Kuanzia siku hiyo huyo dada hajawahi kusumbuliwa visa ya US.

Trump anatakiwa kukutana na watu jeuri wa kumwambia kama mnatupiga ban na sisi tunakupiga ban.

Mjamaica anakwambia "Me no beg no friend".

Siombelezei urafiki.
Mkuu wale jamaa wa ubalozi washasoma mindset za waafrika hasa watanzania.

Yani kama mtu hana travel history yeyote, Au ana travel history ya nchi zetu hizi za hapahapa Afrika, Wana assume ni mzamiaji...😄

Halafu wewe sasa ndio unatakiwa ujitetee kwamba utakwenda na kurudi.
 
Una miaka mingapi chifu ?
Hakuna kitu bora kama mahusiano na watu au taifa kwa taifa, hali ya usalama nchini ni tete sasa si unakuwa unaleta taharuki kwa watu.
Sasa kama unaohusiana nao hawakutaki utalazimisha?
 
Back
Top Bottom