Tanzania yatoa majibu na msimamo wake kwa Azimio la Bunge la Ulaya la Mei 8, 2025

TAMKO LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA ULAYA

Dar es Salaam, 8 Mei 2025

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea taarifa ya azimio lililopitishwa na Bunge la Ulaya tarehe 8 Mei 2025 kuhusu mwenendo wa mashauri ya kisheria yanayoendelea nchini Tanzania. Wakati Tanzania ikiheshimu uhuru wa taasisi wa Bunge la Ulaya na kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya, inaona ni muhimu kufafanua baadhi ya mambo ya msingi na kusisitiza tena dhamira yake ya muda mrefu ya kuzingatia misingi ya demokrasia, utawala bora, na sheria.

Tangu Machi 2021, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitekeleza mageuzi ya kisiasa na kisheria kupitia dhana ya 4R – Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Upya. Mageuzi haya yameleta mafanikio ya dhahiri ikiwa ni pamoja na kurejesha uhuru wa kisiasa, kupanua haki za kiraia, kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, na kupitishwa kwa sheria mpya za uchaguzi mwezi Machi 2024, zilizowezesha kuanzishwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Tanzania ni nchi huru inayoongozwa kwa mujibu wa Katiba yake na utawala wa sheria. Masuala yote ya kisheria yanashughulikiwa kwa uhuru na mhimili wa Mahakama ambao ni miongoni mwa mihimili ya dola, kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kwa kuzingatia viwango na kanuni bora za kimataifa, ambapo Serikali (Tawala) haina mamlaka ya kuingilia mashauri ya mahakama. Hivyo basi, matamko yoyote yanayodokeza au kuhamasisha Serikali kuingilia mashauri yanayoendelea mahakamani siyo tu kwamba hayafai, bali pia yanakwenda kinyume na misingi ya uhuru wa Mahakama kama ilivyobainishwa katika Katiba ya Tanzania na kama inavyohimizwa na Umoja wa Ulaya.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ina wasiwasi na mwenendo unaojitokeza kwenye azimio la Bunge la Ulaya ambapo baadhi ya wadau wa kimataifa wanatoa maamuzi kwa msingi wa taarifa pungufu au zenye upendeleo, bila kupitia njia rasmi za kidiplomasia. Mtazamo huu unapotosha na kuwasilisha taswira isiyo sahihi kuhusu hali halisi ya mambo nchini.

Soma Pia: Hoja ya azimio la Bunge la Ulaya kuhusu kukamatwa na hatari ya kunyongwa kwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema

Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo mashauri mahususi ya kisheria, yanashughulikiwa kwa ukaguzi maalum, huku mafanikio makubwa katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari, ushirikishwaji wa kisiasa, mageuzi ya uchaguzi, na ujenzi wa amani ya kikanda yakipuuzwa.

Wakati Tanzania ikiendelea kuheshimu haki na utu wa kila mtu kama ilivyoainishwa katika Katiba yake, ni muhimu kufafanua kuwa masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia yameshaainishwa wazi ndani ya mfumo wa Katiba ya Tanzania, sheria za kitaifa, mila, na desturi za jamii. Tanzania inasisitiza kuwa ushirikiano wowote lazima ujengwe juu ya kuheshimiana kwa misingi ya maadili, ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya kikatiba, mifumo ya kisheria, na utambulisho wa kitaifa, huku ushirikiano wa baadaye ukilenga vipaumbele vya pamoja katika maendeleo, utawala, ukuaji wa uchumi, na ustawi wa watu.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya na iko tayari kwa mazungumzo ya wazi, yenye heshima, na yanayozingatia ushahidi kuhusu masuala ya maslahi na umuhimu wa pamoja. Hata hivyo, mazungumzo haya lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana, na uelewa kamili wa uhuru wa taasisi za kila nchi, Katiba zake, pamoja na muktadha wa sheria na utamaduni wa kila taifa.

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Serikali ya Tanzania inathibitisha tena dhamira yake ya kulinda amani, kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, na kulinda haki na uhuru wa msingi wa wananchi wote kwa mujibu wa Katiba.

Tanzania inakaribisha kuendelea kwa msaada kutoka Umoja wa Ulaya na washirika wote wa kimataifa wanaojitokeza kwa nia njema na uelewa ulio sahihi kuhusu safari ya kidemokrasia ya nchi hii, na wako tayari kushirikiana na wale ambao bado hawajafahamu vya kutosha kuhusu maadili na utamaduni wa Kitanzania.

MWISHO

Imetolewa na:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI – JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

View attachment 3328439
View attachment 3328440
Laiti wangekua na uwezo wabunge wa Ulaya wangepotezwa! Kwakua nguvu yetu imeishia hapa Bongo land, kilichobaki ni kuandika Barua za kulialia ila ukweli utabaki ukweli, sasa mnataka wawahoji ili mseme Mzee Kibao alikufa kwa sababu ya kifo ni kifo tu ? Siku hizi Twitter/X ndio uwanja mpya na kule ndio kila kitu kinawekwa mezani. Tubadilike.
 
"Hakuna mwekezaji mkubwa wa kimataifa anayeweza kukubali kukitokea mgogoro, maamuzi yafanyike na mahakama za nchini Tanzania, mahakama zinazosubiria maelekezo ya Serikali, ndiyo zitoe hukumu" -- Rostam Aziz, ambaye amewahi kuwa mweka hazina mkuu wa CCM. Hata DPW, mkataba wao unasema migogoro yote itaamliwa kwa sheria za Uingereza. Halafu kuna mwehu anasema kuwa mahakama za Tanzania ni mhimili huru na zinafanya kazi kwa weledi. Hopless kabisa, huyo aliyeandaa tamko hili.
 
Sijui kama watakuwa wameelewa hao vichwa maji. Cha muhimu tuache kuomba misaada yo yote kutoka nchi hizo kwank huwa ni ya kinyanyashaji mara zote. Wanatuona sisi bado ni koloni lao.

Mnataka muendelee kuteka, kuua na kutesa watu bila ya kusumbuliwa!! Hopeless satan followers, cursed you are and your generation, for you do not think anything worth that evil.
 
TAMKO LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA ULAYA

Dar es Salaam, 8 Mei 2025

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea taarifa ya azimio lililopitishwa na Bunge la Ulaya tarehe 8 Mei 2025 kuhusu mwenendo wa mashauri ya kisheria yanayoendelea nchini Tanzania. Wakati Tanzania ikiheshimu uhuru wa taasisi wa Bunge la Ulaya na kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya, inaona ni muhimu kufafanua baadhi ya mambo ya msingi na kusisitiza tena dhamira yake ya muda mrefu ya kuzingatia misingi ya demokrasia, utawala bora, na sheria.

Tangu Machi 2021, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitekeleza mageuzi ya kisiasa na kisheria kupitia dhana ya 4R – Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Upya. Mageuzi haya yameleta mafanikio ya dhahiri ikiwa ni pamoja na kurejesha uhuru wa kisiasa, kupanua haki za kiraia, kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, na kupitishwa kwa sheria mpya za uchaguzi mwezi Machi 2024, zilizowezesha kuanzishwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Tanzania ni nchi huru inayoongozwa kwa mujibu wa Katiba yake na utawala wa sheria. Masuala yote ya kisheria yanashughulikiwa kwa uhuru na mhimili wa Mahakama ambao ni miongoni mwa mihimili ya dola, kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kwa kuzingatia viwango na kanuni bora za kimataifa, ambapo Serikali (Tawala) haina mamlaka ya kuingilia mashauri ya mahakama. Hivyo basi, matamko yoyote yanayodokeza au kuhamasisha Serikali kuingilia mashauri yanayoendelea mahakamani siyo tu kwamba hayafai, bali pia yanakwenda kinyume na misingi ya uhuru wa Mahakama kama ilivyobainishwa katika Katiba ya Tanzania na kama inavyohimizwa na Umoja wa Ulaya.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ina wasiwasi na mwenendo unaojitokeza kwenye azimio la Bunge la Ulaya ambapo baadhi ya wadau wa kimataifa wanatoa maamuzi kwa msingi wa taarifa pungufu au zenye upendeleo, bila kupitia njia rasmi za kidiplomasia. Mtazamo huu unapotosha na kuwasilisha taswira isiyo sahihi kuhusu hali halisi ya mambo nchini.

Soma Pia: Hoja ya azimio la Bunge la Ulaya kuhusu kukamatwa na hatari ya kunyongwa kwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema

Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo mashauri mahususi ya kisheria, yanashughulikiwa kwa ukaguzi maalum, huku mafanikio makubwa katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari, ushirikishwaji wa kisiasa, mageuzi ya uchaguzi, na ujenzi wa amani ya kikanda yakipuuzwa.

Wakati Tanzania ikiendelea kuheshimu haki na utu wa kila mtu kama ilivyoainishwa katika Katiba yake, ni muhimu kufafanua kuwa masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia yameshaainishwa wazi ndani ya mfumo wa Katiba ya Tanzania, sheria za kitaifa, mila, na desturi za jamii. Tanzania inasisitiza kuwa ushirikiano wowote lazima ujengwe juu ya kuheshimiana kwa misingi ya maadili, ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya kikatiba, mifumo ya kisheria, na utambulisho wa kitaifa, huku ushirikiano wa baadaye ukilenga vipaumbele vya pamoja katika maendeleo, utawala, ukuaji wa uchumi, na ustawi wa watu.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya na iko tayari kwa mazungumzo ya wazi, yenye heshima, na yanayozingatia ushahidi kuhusu masuala ya maslahi na umuhimu wa pamoja. Hata hivyo, mazungumzo haya lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana, na uelewa kamili wa uhuru wa taasisi za kila nchi, Katiba zake, pamoja na muktadha wa sheria na utamaduni wa kila taifa.

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Serikali ya Tanzania inathibitisha tena dhamira yake ya kulinda amani, kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, na kulinda haki na uhuru wa msingi wa wananchi wote kwa mujibu wa Katiba.

Tanzania inakaribisha kuendelea kwa msaada kutoka Umoja wa Ulaya na washirika wote wa kimataifa wanaojitokeza kwa nia njema na uelewa ulio sahihi kuhusu safari ya kidemokrasia ya nchi hii, na wako tayari kushirikiana na wale ambao bado hawajafahamu vya kutosha kuhusu maadili na utamaduni wa Kitanzania.

MWISHO

Imetolewa na:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI – JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

View attachment 3328439
View attachment 3328440
Ukiisoma hii taarifa unaweza ukafikiri hawa viongozi ni watakatifu sana, wenye uzalendo wa hali ya juu, wanaojali sana na kutetea demokrasia ya nchi yetu, kumbe mioyo yao imejaa tamaa, uhasama na dhuluma. Mpaka Bunge la ulaya linafika hatua ya kujadili swala kama hili msifikiri ni kwa maneno ya kuambiwa tu, wana obsevers wengi ndani ya nchi hii na wanaona kwa macho yao mambo yanayotendeka. Watanzania sio wapumbavu kiasi hicho wa kudanganywa na maneno matamu matamu huku wakiishi kimaskini halafu nyie na familia zenu mnatajirika kupitia migongo yao. Mwisho wenu U karibu
 
TAMKO LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA ULAYA

Dar es Salaam, 8 Mei 2025

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea taarifa ya azimio lililopitishwa na Bunge la Ulaya tarehe 8 Mei 2025 kuhusu mwenendo wa mashauri ya kisheria yanayoendelea nchini Tanzania. Wakati Tanzania ikiheshimu uhuru wa taasisi wa Bunge la Ulaya na kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya, inaona ni muhimu kufafanua baadhi ya mambo ya msingi na kusisitiza tena dhamira yake ya muda mrefu ya kuzingatia misingi ya demokrasia, utawala bora, na sheria.

Tangu Machi 2021, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitekeleza mageuzi ya kisiasa na kisheria kupitia dhana ya 4R – Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Upya. Mageuzi haya yameleta mafanikio ya dhahiri ikiwa ni pamoja na kurejesha uhuru wa kisiasa, kupanua haki za kiraia, kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, na kupitishwa kwa sheria mpya za uchaguzi mwezi Machi 2024, zilizowezesha kuanzishwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Tanzania ni nchi huru inayoongozwa kwa mujibu wa Katiba yake na utawala wa sheria. Masuala yote ya kisheria yanashughulikiwa kwa uhuru na mhimili wa Mahakama ambao ni miongoni mwa mihimili ya dola, kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kwa kuzingatia viwango na kanuni bora za kimataifa, ambapo Serikali (Tawala) haina mamlaka ya kuingilia mashauri ya mahakama. Hivyo basi, matamko yoyote yanayodokeza au kuhamasisha Serikali kuingilia mashauri yanayoendelea mahakamani siyo tu kwamba hayafai, bali pia yanakwenda kinyume na misingi ya uhuru wa Mahakama kama ilivyobainishwa katika Katiba ya Tanzania na kama inavyohimizwa na Umoja wa Ulaya.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ina wasiwasi na mwenendo unaojitokeza kwenye azimio la Bunge la Ulaya ambapo baadhi ya wadau wa kimataifa wanatoa maamuzi kwa msingi wa taarifa pungufu au zenye upendeleo, bila kupitia njia rasmi za kidiplomasia. Mtazamo huu unapotosha na kuwasilisha taswira isiyo sahihi kuhusu hali halisi ya mambo nchini.

Soma Pia: Hoja ya azimio la Bunge la Ulaya kuhusu kukamatwa na hatari ya kunyongwa kwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema

Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo mashauri mahususi ya kisheria, yanashughulikiwa kwa ukaguzi maalum, huku mafanikio makubwa katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari, ushirikishwaji wa kisiasa, mageuzi ya uchaguzi, na ujenzi wa amani ya kikanda yakipuuzwa.

Wakati Tanzania ikiendelea kuheshimu haki na utu wa kila mtu kama ilivyoainishwa katika Katiba yake, ni muhimu kufafanua kuwa masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia yameshaainishwa wazi ndani ya mfumo wa Katiba ya Tanzania, sheria za kitaifa, mila, na desturi za jamii. Tanzania inasisitiza kuwa ushirikiano wowote lazima ujengwe juu ya kuheshimiana kwa misingi ya maadili, ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya kikatiba, mifumo ya kisheria, na utambulisho wa kitaifa, huku ushirikiano wa baadaye ukilenga vipaumbele vya pamoja katika maendeleo, utawala, ukuaji wa uchumi, na ustawi wa watu.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya na iko tayari kwa mazungumzo ya wazi, yenye heshima, na yanayozingatia ushahidi kuhusu masuala ya maslahi na umuhimu wa pamoja. Hata hivyo, mazungumzo haya lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana, na uelewa kamili wa uhuru wa taasisi za kila nchi, Katiba zake, pamoja na muktadha wa sheria na utamaduni wa kila taifa.

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Serikali ya Tanzania inathibitisha tena dhamira yake ya kulinda amani, kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, na kulinda haki na uhuru wa msingi wa wananchi wote kwa mujibu wa Katiba.

Tanzania inakaribisha kuendelea kwa msaada kutoka Umoja wa Ulaya na washirika wote wa kimataifa wanaojitokeza kwa nia njema na uelewa ulio sahihi kuhusu safari ya kidemokrasia ya nchi hii, na wako tayari kushirikiana na wale ambao bado hawajafahamu vya kutosha kuhusu maadili na utamaduni wa Kitanzania.

MWISHO

Imetolewa na:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI – JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

View attachment 3328439
View attachment 3328440
Hivi mnaona kwamba hao Umoja wa Ulaya hawana wanasheria? Hawajui kwamba serikali ndo imemkamata na kumbambikizia Lissu kesi? Hawajui kwamba DPP wenu anachonga kesi na akiamua anazifuta bila kidokezo?
 
Maazimio ya Bunge la EU yatekelezwe kwanza ndo zije hizi ngonjera.
Waafrika Mungu atusaidie. Unahisi Tanzania inaweza kuamua mambo ya nchi nyingine? Ipo siku jirani yako ataamua maisha ya mke wako blaza. Jitafakari!
 
Hivi mnaona kwamba hao Umoja wa Ulaya hawana wanasheria? Hawajui kwamba serikali ndo imemkamata na kumbambikizia Lissu kesi? Hawajui kwamba DPP wenu anachonga kesi na akiamua anazifuta bila kidokezo?
Acha kumpa Lissu umuhimu hivyo. Kwamba EU waje kuhangaika na kesi yake? Labda kwa kuwa anawasaidia kutetea mashoga😄
 
Kamuulize Samia mwenyewe akutajie tu hizo R ni mnyama gani kama ataweza?
Mi nacheka sana nikisikia no reform! Hivi hata vionjo CHADEMA lazima watengenezewe na wazungu. Sasa wapo busy kupita kuwaeleza wananchi maana yake😄
Mjifunzege jamani ligha yetu ni KISWAHILI!
 
TAMKO LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA ULAYA

Dar es Salaam, 8 Mei 2025

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea taarifa ya azimio lililopitishwa na Bunge la Ulaya tarehe 8 Mei 2025 kuhusu mwenendo wa mashauri ya kisheria yanayoendelea nchini Tanzania. Wakati Tanzania ikiheshimu uhuru wa taasisi wa Bunge la Ulaya na kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya, inaona ni muhimu kufafanua baadhi ya mambo ya msingi na kusisitiza tena dhamira yake ya muda mrefu ya kuzingatia misingi ya demokrasia, utawala bora, na sheria.

Tangu Machi 2021, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitekeleza mageuzi ya kisiasa na kisheria kupitia dhana ya 4R – Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Upya. Mageuzi haya yameleta mafanikio ya dhahiri ikiwa ni pamoja na kurejesha uhuru wa kisiasa, kupanua haki za kiraia, kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, na kupitishwa kwa sheria mpya za uchaguzi mwezi Machi 2024, zilizowezesha kuanzishwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Tanzania ni nchi huru inayoongozwa kwa mujibu wa Katiba yake na utawala wa sheria. Masuala yote ya kisheria yanashughulikiwa kwa uhuru na mhimili wa Mahakama ambao ni miongoni mwa mihimili ya dola, kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kwa kuzingatia viwango na kanuni bora za kimataifa, ambapo Serikali (Tawala) haina mamlaka ya kuingilia mashauri ya mahakama. Hivyo basi, matamko yoyote yanayodokeza au kuhamasisha Serikali kuingilia mashauri yanayoendelea mahakamani siyo tu kwamba hayafai, bali pia yanakwenda kinyume na misingi ya uhuru wa Mahakama kama ilivyobainishwa katika Katiba ya Tanzania na kama inavyohimizwa na Umoja wa Ulaya.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ina wasiwasi na mwenendo unaojitokeza kwenye azimio la Bunge la Ulaya ambapo baadhi ya wadau wa kimataifa wanatoa maamuzi kwa msingi wa taarifa pungufu au zenye upendeleo, bila kupitia njia rasmi za kidiplomasia. Mtazamo huu unapotosha na kuwasilisha taswira isiyo sahihi kuhusu hali halisi ya mambo nchini.

Soma Pia: Hoja ya azimio la Bunge la Ulaya kuhusu kukamatwa na hatari ya kunyongwa kwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema

Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo mashauri mahususi ya kisheria, yanashughulikiwa kwa ukaguzi maalum, huku mafanikio makubwa katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari, ushirikishwaji wa kisiasa, mageuzi ya uchaguzi, na ujenzi wa amani ya kikanda yakipuuzwa.

Wakati Tanzania ikiendelea kuheshimu haki na utu wa kila mtu kama ilivyoainishwa katika Katiba yake, ni muhimu kufafanua kuwa masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia yameshaainishwa wazi ndani ya mfumo wa Katiba ya Tanzania, sheria za kitaifa, mila, na desturi za jamii. Tanzania inasisitiza kuwa ushirikiano wowote lazima ujengwe juu ya kuheshimiana kwa misingi ya maadili, ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya kikatiba, mifumo ya kisheria, na utambulisho wa kitaifa, huku ushirikiano wa baadaye ukilenga vipaumbele vya pamoja katika maendeleo, utawala, ukuaji wa uchumi, na ustawi wa watu.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya na iko tayari kwa mazungumzo ya wazi, yenye heshima, na yanayozingatia ushahidi kuhusu masuala ya maslahi na umuhimu wa pamoja. Hata hivyo, mazungumzo haya lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana, na uelewa kamili wa uhuru wa taasisi za kila nchi, Katiba zake, pamoja na muktadha wa sheria na utamaduni wa kila taifa.

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Serikali ya Tanzania inathibitisha tena dhamira yake ya kulinda amani, kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, na kulinda haki na uhuru wa msingi wa wananchi wote kwa mujibu wa Katiba.

Tanzania inakaribisha kuendelea kwa msaada kutoka Umoja wa Ulaya na washirika wote wa kimataifa wanaojitokeza kwa nia njema na uelewa ulio sahihi kuhusu safari ya kidemokrasia ya nchi hii, na wako tayari kushirikiana na wale ambao bado hawajafahamu vya kutosha kuhusu maadili na utamaduni wa Kitanzania.

MWISHO

Imetolewa na:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI – JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

View attachment 3328439
View attachment 3328440
Ngoja wakate misaada tuone mtafika wapi. Kipande cha Reli cha 3 na cha 4 hadi sasa hakina mfadhili juzi mlikuwa POLAND mnatafuta mipoko, endeleeni na kiburi muone mtakapoishia.
 
Back
Top Bottom