mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 47,054
- 58,689
wameyatimba🤣🤣🤣.
eti tanzania napo kuna uhuru wa kisiasa
eti tanzania napo kuna uhuru wa kisiasa
Hawaeleweki, na wawe wakweliWaafrika hasa watanzania wana upumbavu wa milele.
Pesa zitatoka warabuni na umoja wa Africa na nyengine ktk michango ya wananchi"Tanzania inakaribisha kuendelea kwa msaada kutoka umoja wa ulaya na washirika wote wa kimataifa"
... mwisho wa kunukuu...
Kwa kuwa hata pesa ya kufanya uchaguzi nchini ni msaada toka nje, Reforms zitafanyika kwenye katiba na tutapata Tume huru ya uchaguzi na Tundu lissu ataachiwa huru.
Tusubiri 🙏
Pesa za uarabuni ni kwa ajili ya kujenga misikiti na kununulia futari.Pesa zitatoka warabuni na umoja wa Africa na nyengine ktk michango ya wananchi
Ni kweli kabisa, hivi ni kweli mihimili ya dola haiingiliani na inajitegemea? Serikali imekua ikiingilia mihimili mingine kwa maelekezo kila siku. Bunge la ulaya hawakurupuki wanaongea kitu walichofanyia utafiti usio na shaka, hizi siasa chafu tufanyiane wenyewe, hii nchi Ina madeni mengi kutoka ulaya, na inategemea misaada kutoka huko nashangaa bunge linavyojitoa ufahamuWaafrika hasa watanzania wana upumbavu wa milele.
Bandarini zipo za wazungu? Wazungu zao mpaka uunge mkono ushogaPesa za uarabuni ni kwa ajili ya kujenga misikiti na kununulia futari.
Ndugu yangu, ubovu wa watawala wetu ndo unaopelekea tuseme hayo. Bunge letu ambalo lilitakiwa kupigania HAKI za Watanzania, limepoteza uelekeo na kujikuta linaungana na Dola. Katika uchaguzi uliofanyika wakati wa utawala dhalimu wa kikoloni Mwalimu Nyerere aliweza kushinda uchaguzi lakini uchaguzi unaosimamiwa na sisi wenyewe waafrika wapinzani hawawezi kutangazwa washindi, Je, kati ya wakoloni na watawala wetu wa sasa ni bora nani?Waafrika Mungu atusaidie. Unahisi Tanzania inaweza kuamua mambo ya nchi nyingine? Ipo siku jirani yako ataamua maisha ya mke wako blaza. Jitafakari!
Linapokuja suala la haki za binadam basi tambua kwamba halina mipaka ni suala la mikataba ya kimataifa.Waafrika Mungu atusaidie. Unahisi Tanzania inaweza kuamua mambo ya nchi nyingine? Ipo siku jirani yako ataamua maisha ya mke wako blaza. Jitafakari!
Sijui kama watakuwa wameelewa hao vichwa maji. Cha muhimu tuache kuomba misaada yo yote kutoka nchi hizo kwank huwa ni ya kinyanyashaji mara zote. Wanatuona sisi bado ni koloni lao.
Aliyeandika majibu hayo kulijibu bunge la Ulaya ni kilaza kweli kweli. Hakuna cha maana alichoandika. Wapinzani wanatekwa na kupotea na wengine kuuawa huku serikali inakaa kimya inauhadaa umma kwamba inafanya uchunguzi. Bunge la Ulaya lijibiwe kwa mantiki sio majibu ya kipuuzi kama hayo.
Unabishana na waraka wa serikali paragraph ya mwisho niliyonukuu?Pesa zitatoka warabuni na umoja wa Africa na nyengine ktk michango ya wananchi
Mi nimeona kuwa hapa TUMEJITETEA NA KUPIGA MAGAOTI UTADHANI MUOMBA LIFT PORINI,LKN HATUJAISHIA HAPO,AYA YA MWISHO TUMESISITIZA KUENDELEA KUTEGEMEA NA KUOMBA MISAADA YAO.TAMKO LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA ULAYA
Dar es Salaam, 8 Mei 2025
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea taarifa ya azimio lililopitishwa na Bunge la Ulaya tarehe 8 Mei 2025 kuhusu mwenendo wa mashauri ya kisheria yanayoendelea nchini Tanzania. Wakati Tanzania ikiheshimu uhuru wa taasisi wa Bunge la Ulaya na kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya, inaona ni muhimu kufafanua baadhi ya mambo ya msingi na kusisitiza tena dhamira yake ya muda mrefu ya kuzingatia misingi ya demokrasia, utawala bora, na sheria.
Tangu Machi 2021, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitekeleza mageuzi ya kisiasa na kisheria kupitia dhana ya 4R – Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Upya. Mageuzi haya yameleta mafanikio ya dhahiri ikiwa ni pamoja na kurejesha uhuru wa kisiasa, kupanua haki za kiraia, kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, na kupitishwa kwa sheria mpya za uchaguzi mwezi Machi 2024, zilizowezesha kuanzishwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Tanzania ni nchi huru inayoongozwa kwa mujibu wa Katiba yake na utawala wa sheria. Masuala yote ya kisheria yanashughulikiwa kwa uhuru na mhimili wa Mahakama ambao ni miongoni mwa mihimili ya dola, kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kwa kuzingatia viwango na kanuni bora za kimataifa, ambapo Serikali (Tawala) haina mamlaka ya kuingilia mashauri ya mahakama. Hivyo basi, matamko yoyote yanayodokeza au kuhamasisha Serikali kuingilia mashauri yanayoendelea mahakamani siyo tu kwamba hayafai, bali pia yanakwenda kinyume na misingi ya uhuru wa Mahakama kama ilivyobainishwa katika Katiba ya Tanzania na kama inavyohimizwa na Umoja wa Ulaya.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ina wasiwasi na mwenendo unaojitokeza kwenye azimio la Bunge la Ulaya ambapo baadhi ya wadau wa kimataifa wanatoa maamuzi kwa msingi wa taarifa pungufu au zenye upendeleo, bila kupitia njia rasmi za kidiplomasia. Mtazamo huu unapotosha na kuwasilisha taswira isiyo sahihi kuhusu hali halisi ya mambo nchini.
Soma Pia: Hoja ya azimio la Bunge la Ulaya kuhusu kukamatwa na hatari ya kunyongwa kwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema
Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo mashauri mahususi ya kisheria, yanashughulikiwa kwa ukaguzi maalum, huku mafanikio makubwa katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari, ushirikishwaji wa kisiasa, mageuzi ya uchaguzi, na ujenzi wa amani ya kikanda yakipuuzwa.
Wakati Tanzania ikiendelea kuheshimu haki na utu wa kila mtu kama ilivyoainishwa katika Katiba yake, ni muhimu kufafanua kuwa masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia yameshaainishwa wazi ndani ya mfumo wa Katiba ya Tanzania, sheria za kitaifa, mila, na desturi za jamii. Tanzania inasisitiza kuwa ushirikiano wowote lazima ujengwe juu ya kuheshimiana kwa misingi ya maadili, ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya kikatiba, mifumo ya kisheria, na utambulisho wa kitaifa, huku ushirikiano wa baadaye ukilenga vipaumbele vya pamoja katika maendeleo, utawala, ukuaji wa uchumi, na ustawi wa watu.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya na iko tayari kwa mazungumzo ya wazi, yenye heshima, na yanayozingatia ushahidi kuhusu masuala ya maslahi na umuhimu wa pamoja. Hata hivyo, mazungumzo haya lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana, na uelewa kamili wa uhuru wa taasisi za kila nchi, Katiba zake, pamoja na muktadha wa sheria na utamaduni wa kila taifa.
Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Serikali ya Tanzania inathibitisha tena dhamira yake ya kulinda amani, kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, na kulinda haki na uhuru wa msingi wa wananchi wote kwa mujibu wa Katiba.
Tanzania inakaribisha kuendelea kwa msaada kutoka Umoja wa Ulaya na washirika wote wa kimataifa wanaojitokeza kwa nia njema na uelewa ulio sahihi kuhusu safari ya kidemokrasia ya nchi hii, na wako tayari kushirikiana na wale ambao bado hawajafahamu vya kutosha kuhusu maadili na utamaduni wa Kitanzania.
MWISHO
Imetolewa na:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI – JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
View attachment 3328439
View attachment 3328440
sie ni waungwana lazima tujibu kiungwanaMi nimeona kuwa hapa TUMEJITETEA NA KUPIGA MAGAOTI UTADHANI MUOMBA LIFT PORINI,LKN HATUJAISHIA HAPO,AYA YA MWISHO TUMESISITIZA KUENDELEA KUTEGEMEA NA KUOMBA MISAADA YAO.
Nilitegemea tunawafumba midomo kwa kutukemea lkn kumbe sivyo.