Tanzania yatoa majibu na msimamo wake kwa Azimio la Bunge la Ulaya la Mei 8, 2025

Tanzania yatoa majibu na msimamo wake kwa Azimio la Bunge la Ulaya la Mei 8, 2025

Watawala wasidhani Bunge la EU ni kama Bunge letu la kusifu na kuabudu. Ni Bunge lenye weledi na huwezi kulidanganya kwa maneno matupu bila matendo na mifano hai.

Watawala wetu wakubali yaishe, vinginevyo watapigwa VIKWAZO mpaka wataomba mizimu yao iwasaidie.

Rai yangu, watawala wetu wasiendelee kubishana na Bunge la EU kwa maneno rahisi rahisi haya, wajitathmini na waongoke kwa mioyo yao yote.
Kiburi kimewajaaa....fanya kiburi ukiwa na akili sasa na nguvu kiuchumi....yaan huu ujinga waliondika hapa ndo utawashawish wale watu...arrogance hii imeptiliza...waendelee kujizma data
 
Maazimio yaliyojadiliwa ni yapi?​

Wameitaka Serikali ya Tanzania kumwachilia mara moja Lissu na bila masharti yoyote, ili kuhakikisha usalama wake na haki yake ya kusikilizwa kwa haki na uwakilishi wa kisheria.
Wabunge hao wanazitaka mamlaka za Tanzania kukomesha ukandamizaji unaoendelea, ukamataji hovyo, unyanyasaji, mashambulizi na unyanyasaji dhidi ya wanachama wa upinzani, watetezi wa haki za binadamu, watu wa kiasili, wanaharakati wa LGBTIQ+, waandishi wa habari na mashirika ya kiraia, na kuchunguza kwa uhuru dhuluma za polisi na kupotea kwa watu, kudumisha utawala, sheria, vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na mahakama.
 
Hivi mnaona kwamba hao Umoja wa Ulaya hawana wanasheria? Hawajui kwamba serikali ndo imemkamata na kumbambikizia Lissu kesi? Hawajui kwamba DPP wenu anachonga kesi na akiamua anazifuta bila kidokezo?
Wanafikir wale jamaa ni wajinga kma wao
 
Watu wanaimba kama kasuku tu 4R,4R,4R!

Kwa ground tuna 0R,kila siku tunasikia,"Sheria zilizofanya mkimbie nchi hapo nyuma bado zipo".

Hayo mageuzi makubwa ya sheria ni yepi km bado mnatisha watu sheria hizo bado zipo???

Ila umasikini ni mbaya,cheki mlivyojieleza!!!
😂😂😂😂😂😂
 
Demokrasia maana yake government of the people for the people lakini hii hapa Tanzania ni kama government of the leaders for the people .Yaani haki ya kulinda demokrasia nchini ipo kwenye makaratasi na mdomoni lakini sio katika uhalisia . Chama cha upizani kinachoneonekana kina nguvu viongozi wake wanatengenezewa zengwe yaani chaguzi tunazofanya ni kama kiini macho kuidanganya dunia kwamba kuna utawala wa kidemokrasia ili hali ni uongo mchana kwaupe.
Halafu huwa nashangaa .. kuna watu wanaona sawa tu....bila shaka kuna jinsi wanafadikia na dhuluma hii....
 
Hapo kwenye Mageuzi ya Tume huru ya uchaguzi nimebaki kucheka tu.

Hapo wanaposema wapo tayari kwa mazungumzo ndio penyewe sasa,....
Sasa mazungumzo hayo yafanyike tu endapo kuna pande 3 zikutanishwe.....
Serikali, Opposition na Delegation ya Euro assembly.......huku hoja za kila upande ziwasilishwe, zisikilizwe na zipimwe.

Mazungumzo ya gizani gizani iwe marufuku.
 
Kwahiyo Wahisani hawatakiwi kuingilia mambo ya ndani ya nchi husika ndio kigezo cha kujifichia kufanya chaguzi za kihuni, Wateka Wakosoaji, kufanya ufisadi nk?

Hii Sheria ya jumla ya kimataifa ni lazima itengenezewe kanuni.....Kwamba mamlaka za ndani hazitaingiliwa tu ikiwa upo ushahidi kwa machafu mengine hayafanyiki.
 
Mjomba aliwaminya vya kutosha wapinzani, walitekwa, kupotezwa na hata kuuwawa wengi sana,

Alifkuza au kuwafungia kazi za michongo yao wazungu(acacia na wenzao), alizuia na kufunga kabisa harakati za siasa kwa miaka mtano, ofisi za wapinzani zilijaa vumbi, nk nk.

Ajabu hakuna eu wala su wala bunge la eu au la us lililokaa na kumjadili au kuijadili serikali halali ya Tanzania.
Wala kutishia vikwazo vyovyote na mjomba hakuwahi hata kwenda huko kwao ndani ya utawala wake, yaani aliwadharau wazungu kwa kipimo cha mwisho kabisa, hongera sana magu

Sasa basi kwa maelezo haya tunahitimisha na kukubaliana wote kwa pamoja kwamba huu ni udini wa kiwango cha kimataifa

Ni UDINI tu, hakuna chochote kile, udini umekwenda hadi kimataifa, sasa na sisi upande huu tutafanya kama mnavyofanya, tunajua zamu yenu itafika nasi tutatumia mbinu hizi hizi

Kama ufanyavyo utafanyiwa

NB:
Povu ruksa, ila ukinitukana nitakuna mara mbili zaidi
Wewe ndio mdini na tushajua wa upande gani, na huyo uliyemsifia alipata nini cha maana
 
😂
 
sitaki kuamini kama hili tangazo ni laserikali ,murilo na wahuni wezenu mnalakujifunza.......

serikali imegeuzwa kibra...... nabado
 
Hata hivyo, mazungumzo haya lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana, na uelewa kamili wa uhuru wa taasisi za kila nchi, Katiba zake, pamoja na muktadha wa sheria na utamaduni wa kila taifa.
Hapa wangeongezea kipengele cha kupinga mitazamo ya kiukoloni mamboleo, ili kuwapiga bit hao waojifanya kuwa ni watawala wa dunia.
 
Ili tuweze kujitengemea nilazima misaada ikome hata mtoto hawezi kuacha kunyonya bila kupaka pilipili kwenye nyonyo angalia nchi zote zenye vikwazo vs zisizo na vikwazo majibu utapata
 
Back
Top Bottom