Tanzania yatoa majibu na msimamo wake kwa Azimio la Bunge la Ulaya la Mei 8, 2025

Tanzania yatoa majibu na msimamo wake kwa Azimio la Bunge la Ulaya la Mei 8, 2025

Kwa hiyo kwa vile nyuma hamkuchuliwa hatua ndo mnaendelea na maovu yenu ??
Uko sawa hapo upstairs kweli ?
Bunge EU lilishakaa kwa ajili ya museveni, netanyahu!?..
Kwa hiyo mnataka nchi yetu iwe kama ya Museven

Tanzania Ina misingi yake ya Kusimamia haki tangu zamani huwezi kuzifafanisha na nchi nyingine

Ila Kuna watu wajinga wanataka kuharibu hadhi ya nchi yetu
Unakwepa siyo!!?.. unakwepa kwamba kuna agenda maalum tz toka kwa wavaa majoho,wastaafu, walitanguliza domokaya..hamtofaulu
 
Kwani ni lazima kila Tanzania ikivunja haki za binadamu Bunge ka EU lifanye kikao?
Kuna ishara za agenda maalum tz,ukitazama nyendo za wavaa majoho, wastaafu na domokaya..now,wavaa majoho wamefikisha mambo EU, serikali washikilie hapohapo Ili litote,tugawane mbao.. halafu tuone sadaka zitatoka wapi
 
Kuna ishara za agenda maalum tz,ukitazama nyendo za wavaa majoho, wastaafu na domokaya..now,wavaa majoho wamefikisha mambo EU, serikali washikilie hapohapo Ili litote,tugawane mbao.. halafu tuone sadaka zitatoka wapi
Ukijikojolea, watu wakasema kweli umejikojolea, hapo huna haki ya kusema wana ajenda maalum.

Suala ni, umejikojolea kweli au hujajikojolea?
 
Sijaona majibu yoyote kwenye hicho kipeperushi cha serikali Lumumba.

Naona ngojera na uchawa mtupu.
 
Ukijikojolea, watu wakasema kweli umejikojolea, hapo huna haki ya kusema wana ajenda maalum.

Suala ni, umejikojolea kweli au hujajikojolea?
Ukijikojolea inakua kweli umejikojolea,so hilo swali mwishoni halina maana,labda usiwe na uhakika kama kweli kajikojolea
 
Ukijikojolea inakua kweli umejikojolea,so hilo swali mwishoni halina maana,labda usiwe na uhakika kama kweli kajikojolea
Sasa mbona umeambiwa umejikojolea halafu unaanza kuuliza mbona hata jana nilijikojolea hamjaniambia nimejikojolea, mnaniambia nimejikojolea leo?
 
Waafrika Mungu atusaidie. Unahisi Tanzania inaweza kuamua mambo ya nchi nyingine? Ipo siku jirani yako ataamua maisha ya mke wako blaza. Jitafakari!
Mkuu hujawahi kuona mwaname anakunjwa makofi akikosa heshima kwenye familia yake?
 
TAMKO LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA ULAYA


Dar es Salaam, 8 Mei 2025

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea taarifa ya azimio lililopitishwa na Bunge la Ulaya tarehe 8 Mei 2025 kuhusu mwenendo wa mashauri ya kisheria yanayoendelea nchini Tanzania. Wakati Tanzania ikiheshimu uhuru wa taasisi wa Bunge la Ulaya na kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya, inaona ni muhimu kufafanua baadhi ya mambo ya msingi na kusisitiza tena dhamira yake ya muda mrefu ya kuzingatia misingi ya demokrasia, utawala bora, na sheria.

Tangu Machi 2021, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitekeleza mageuzi ya kisiasa na kisheria kupitia dhana ya 4R – Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Upya. Mageuzi haya yameleta mafanikio ya dhahiri ikiwa ni pamoja na kurejesha uhuru wa kisiasa, kupanua haki za kiraia, kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, na kupitishwa kwa sheria mpya za uchaguzi mwezi Machi 2024, zilizowezesha kuanzishwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Tanzania ni nchi huru inayoongozwa kwa mujibu wa Katiba yake na utawala wa sheria. Masuala yote ya kisheria yanashughulikiwa kwa uhuru na mhimili wa Mahakama ambao ni miongoni mwa mihimili ya dola, kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kwa kuzingatia viwango na kanuni bora za kimataifa, ambapo Serikali (Tawala) haina mamlaka ya kuingilia mashauri ya mahakama. Hivyo basi, matamko yoyote yanayodokeza au kuhamasisha Serikali kuingilia mashauri yanayoendelea mahakamani siyo tu kwamba hayafai, bali pia yanakwenda kinyume na misingi ya uhuru wa Mahakama kama ilivyobainishwa katika Katiba ya Tanzania na kama inavyohimizwa na Umoja wa Ulaya.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ina wasiwasi na mwenendo unaojitokeza kwenye azimio la Bunge la Ulaya ambapo baadhi ya wadau wa kimataifa wanatoa maamuzi kwa msingi wa taarifa pungufu au zenye upendeleo, bila kupitia njia rasmi za kidiplomasia. Mtazamo huu unapotosha na kuwasilisha taswira isiyo sahihi kuhusu hali halisi ya mambo nchini.

Soma Pia: Hoja ya azimio la Bunge la Ulaya kuhusu kukamatwa na hatari ya kunyongwa kwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema

Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo mashauri mahususi ya kisheria, yanashughulikiwa kwa ukaguzi maalum, huku mafanikio makubwa katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari, ushirikishwaji wa kisiasa, mageuzi ya uchaguzi, na ujenzi wa amani ya kikanda yakipuuzwa.

Wakati Tanzania ikiendelea kuheshimu haki na utu wa kila mtu kama ilivyoainishwa katika Katiba yake, ni muhimu kufafanua kuwa masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia yameshaainishwa wazi ndani ya mfumo wa Katiba ya Tanzania, sheria za kitaifa, mila, na desturi za jamii. Tanzania inasisitiza kuwa ushirikiano wowote lazima ujengwe juu ya kuheshimiana kwa misingi ya maadili, ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya kikatiba, mifumo ya kisheria, na utambulisho wa kitaifa, huku ushirikiano wa baadaye ukilenga vipaumbele vya pamoja katika maendeleo, utawala, ukuaji wa uchumi, na ustawi wa watu.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya na iko tayari kwa mazungumzo ya wazi, yenye heshima, na yanayozingatia ushahidi kuhusu masuala ya maslahi na umuhimu wa pamoja. Hata hivyo, mazungumzo haya lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana, na uelewa kamili wa uhuru wa taasisi za kila nchi, Katiba zake, pamoja na muktadha wa sheria na utamaduni wa kila taifa.

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Serikali ya Tanzania inathibitisha tena dhamira yake ya kulinda amani, kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, na kulinda haki na uhuru wa msingi wa wananchi wote kwa mujibu wa Katiba.

Tanzania inakaribisha kuendelea kwa msaada kutoka Umoja wa Ulaya na washirika wote wa kimataifa wanaojitokeza kwa nia njema na uelewa ulio sahihi kuhusu safari ya kidemokrasia ya nchi hii, na wako tayari kushirikiana na wale ambao bado hawajafahamu vya kutosha kuhusu maadili na utamaduni wa Kitanzania.

MWISHO


Imetolewa na:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI – JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

View attachment 3328439
View attachment 3328440
CCM NI MAZIMWI YANADANGANYA MPAKA WAZUNGU
 
Sasa mbona umeambiwa umejikojolea halafu unaanza kuuliza mbona hata jana nilijikojolea hamjaniambia nimejikojolea, mnaniambia nimejikojolea leo?
Sijajikojolea,nakushangaa wewe kusema nimejikojolea
 
Haya mambo yanafurahisha kweli tungejifunza, ECOWAS ilichoifanyia Gambia.
Pia tujifunze Rwanda ilichowafanyia waCongo walipojiona wanahaki ya kwaburuza watutsi.
Kimsingi hata sisi watz tulipokuwa na AKILI TIMAMU kisiasa, raisi wetu aliwahi iambia rwanda iache kuleta chokochoko huko congo.

Sasa kinachotushinda kuelewa hapa kwamba tunazngua ni nini?.
Kwa mwenendo huu tusubiri kukemewa na wakenya,kuchekwa na waganda na wanyarwanda tulivyokuwa tunajifanya tunaijua siasa za amani.
Kwani TISS hawawaelezi ukweli enyi viongoz wetu kwamba wananchi wana moto na vidonda mioyoni mwao juu ya hayo mnayolalamikiwa?

Basi mtusamehe sis wananchi wenu tulio wakosefu, enyi viongozi wetu mlio malaika ktk miili ya kibinadamu.
 
viongozi wetu wana ujinga mwingi sana. Tuna wasomi wajinga sana. Tundu Lissu amebeba agenda ya Mungu juu ya Tanzania mpya. Hazuiliki.
Waache wakaze mafuvu, wajue tu ukitaka kumuondoa unaondoka ww, sijui Kwann hawajifunzi awamu iliyopita
 
Sijajikojolea,nakushangaa wewe kusema nimejikojolea
Nimekwambia swali si hujajikojolea, nimekwambia mkojo rangi gani hujajikojolea?

Umeshindwa kutaja rangi ya mkojo ambao hujajikojolea.
 
Haki zikavunjwa na hapakua na bunge la EU,kushtakiwa lissu kwa kuchochea uasi, vikwazo!?
Unaelewa maana ya uasi? anyway debating chawa kama ni waste of time tuu, acha wenye akili waendelee na kazi, wewe na ndugu zako mtafaidika pia na kuacha kula kwa uchawa
 
Tatizo sioni Serikali ikichukua hatua ya kulinda Raia hasa wale wenye maoni tofauti na wenye kuikisoa serikali,
Bunge halijadili kuhusu kutekwa na kuuwawa Kwa watu , Bali linaongelea mambo ambayo Kwa ujumla Wala hayana tija
 
Mjomba aliwaminya vya kutosha wapinzani, walitekwa, kupotezwa na hata kuuwawa wengi sana,

Alifkuza au kuwafungia kazi za michongo yao wazungu(acacia na wenzao), alizuia na kufunga kabisa harakati za siasa kwa miaka mtano, ofisi za wapinzani zilijaa vumbi, nk nk.

Ajabu hakuna eu wala su wala bunge la eu au la us lililokaa na kumjadili au kuijadili serikali halali ya Tanzania.
Wala kutishia vikwazo vyovyote na mjomba hakuwahi hata kwenda huko kwao ndani ya utawala wake, yaani aliwadharau wazungu kwa kipimo cha mwisho kabisa, hongera sana magu

Sasa basi kwa maelezo haya tunahitimisha na kukubaliana wote kwa pamoja kwamba huu ni udini wa kiwango cha kimataifa

Ni UDINI tu, hakuna chochote kile, udini umekwenda hadi kimataifa, sasa na sisi upande huu tutafanya kama mnavyofanya, tunajua zamu yenu itafika nasi tutatumia mbinu hizi hizi

Kama ufanyavyo utafanyiwa

NB:
Povu ruksa, ila ukinitukana nitakuna mara mbili zaidi
 
Hongera sana wizara, mumejibu vizuri sana,
Wakijibu jibuni tena, wakiweka vikwazo tutaumia wote na ndio tutajua nani rafiki wa kweli na nani mpinzani wa kweli kwani kuna wengine wameshajiwekea makazi huko inje ya inchi
 
Back
Top Bottom