Tanzania yatoa majibu na msimamo wake kwa Azimio la Bunge la Ulaya la Mei 8, 2025

Tanzania yatoa majibu na msimamo wake kwa Azimio la Bunge la Ulaya la Mei 8, 2025

Kata misaada na wape personal ban kwenye kusafiri na account zao za wizi, hayawezi kubadilika bila maumivu ya uhuru wao na account zao
Hawana huo ubavu kwa sasa wanaihitaji Afrika zaidi ya tunavyowahitaji,,,,,wakikata misaada watapata wapi rasilimali za kitonga
 
Hili Andiko limeandikwa na maafisa Utumishi pale wizara mambo ya Nje….. wahuni wale wazee wa kupanga safar za nje

Wamemmisslead waziri
 
Nakwambia hivii, swali si haki gani zimevunjwa, swali ni haki gani hazijavunjwa.

Taja haki yoyote ya binadamu ambayo haijavunjwa Tanzania.
Haki zikavunjwa na hapakua na bunge la EU,kushtakiwa lissu kwa kuchochea uasi, vikwazo!?
 
Serikali ikaze,nchi ipigwe vikwazo, uchumi uzorote,halafu huku ground tutadili na hao nguchiro waliopeleka minduku yao kujambajamba EU,akiwemo yule domokaya
 
Sijui kama watakuwa wameelewa hao vichwa maji. Cha muhimu tuache kuomba misaada yo yote kutoka nchi hizo kwank huwa ni ya kinyanyashaji mara zote. Wanatuona sisi bado ni koloni lao.
Vipi kuhusu watalii, uwekezaji na huduma za taasisi kama zote za kigeni zilizopo, kanisa la roma lina hospitali ngapi nchini na taasisi za kielimu.
 
Haki zikavunjwa na hapakua na bunge la EU,kushtakiwa lissu kwa kuchochea uasi, vikwazo!?
Nakwambia hivii, swali si haki gani zimevunjwa, swali ni haki gani hazijavunjwa.

Taja haki yoyote ya binadamu ambayo haijavunjwa Tanzania.

Umeelewa swali?
 
Nakwambia hivii, swali si haki gani zimevunjwa, swali ni haki gani hazijavunjwa.

Taja haki yoyote ya binadamu ambayo haijavunjwa Tanzania.

Umeelewa swali?
Tukubali tz ilivunja haki huko nyuma,mbona hapakuitishwa kikao cha bunge la EU na wito wa vikwazo!?
 
Tukubali tz ilivunja haki huko nyuma,mbona hapakuitishwa kikao cha bunge la EU na wito wa vikwazo!?
Kwani ni lazima kila Tanzania ikivunja haki za binadamu Bunge ka EU lifanye kikao?
 
TAMKO LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA ULAYA


Dar es Salaam, 8 Mei 2025

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea taarifa ya azimio lililopitishwa na Bunge la Ulaya tarehe 8 Mei 2025 kuhusu mwenendo wa mashauri ya kisheria yanayoendelea nchini Tanzania. Wakati Tanzania ikiheshimu uhuru wa taasisi wa Bunge la Ulaya na kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya, inaona ni muhimu kufafanua baadhi ya mambo ya msingi na kusisitiza tena dhamira yake ya muda mrefu ya kuzingatia misingi ya demokrasia, utawala bora, na sheria.

Tangu Machi 2021, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitekeleza mageuzi ya kisiasa na kisheria kupitia dhana ya 4R – Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Upya. Mageuzi haya yameleta mafanikio ya dhahiri ikiwa ni pamoja na kurejesha uhuru wa kisiasa, kupanua haki za kiraia, kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, na kupitishwa kwa sheria mpya za uchaguzi mwezi Machi 2024, zilizowezesha kuanzishwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Tanzania ni nchi huru inayoongozwa kwa mujibu wa Katiba yake na utawala wa sheria. Masuala yote ya kisheria yanashughulikiwa kwa uhuru na mhimili wa Mahakama ambao ni miongoni mwa mihimili ya dola, kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kwa kuzingatia viwango na kanuni bora za kimataifa, ambapo Serikali (Tawala) haina mamlaka ya kuingilia mashauri ya mahakama. Hivyo basi, matamko yoyote yanayodokeza au kuhamasisha Serikali kuingilia mashauri yanayoendelea mahakamani siyo tu kwamba hayafai, bali pia yanakwenda kinyume na misingi ya uhuru wa Mahakama kama ilivyobainishwa katika Katiba ya Tanzania na kama inavyohimizwa na Umoja wa Ulaya.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ina wasiwasi na mwenendo unaojitokeza kwenye azimio la Bunge la Ulaya ambapo baadhi ya wadau wa kimataifa wanatoa maamuzi kwa msingi wa taarifa pungufu au zenye upendeleo, bila kupitia njia rasmi za kidiplomasia. Mtazamo huu unapotosha na kuwasilisha taswira isiyo sahihi kuhusu hali halisi ya mambo nchini.

Soma Pia: Hoja ya azimio la Bunge la Ulaya kuhusu kukamatwa na hatari ya kunyongwa kwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema

Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo mashauri mahususi ya kisheria, yanashughulikiwa kwa ukaguzi maalum, huku mafanikio makubwa katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari, ushirikishwaji wa kisiasa, mageuzi ya uchaguzi, na ujenzi wa amani ya kikanda yakipuuzwa.

Wakati Tanzania ikiendelea kuheshimu haki na utu wa kila mtu kama ilivyoainishwa katika Katiba yake, ni muhimu kufafanua kuwa masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia yameshaainishwa wazi ndani ya mfumo wa Katiba ya Tanzania, sheria za kitaifa, mila, na desturi za jamii. Tanzania inasisitiza kuwa ushirikiano wowote lazima ujengwe juu ya kuheshimiana kwa misingi ya maadili, ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya kikatiba, mifumo ya kisheria, na utambulisho wa kitaifa, huku ushirikiano wa baadaye ukilenga vipaumbele vya pamoja katika maendeleo, utawala, ukuaji wa uchumi, na ustawi wa watu.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya na iko tayari kwa mazungumzo ya wazi, yenye heshima, na yanayozingatia ushahidi kuhusu masuala ya maslahi na umuhimu wa pamoja. Hata hivyo, mazungumzo haya lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana, na uelewa kamili wa uhuru wa taasisi za kila nchi, Katiba zake, pamoja na muktadha wa sheria na utamaduni wa kila taifa.

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Serikali ya Tanzania inathibitisha tena dhamira yake ya kulinda amani, kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, na kulinda haki na uhuru wa msingi wa wananchi wote kwa mujibu wa Katiba.

Tanzania inakaribisha kuendelea kwa msaada kutoka Umoja wa Ulaya na washirika wote wa kimataifa wanaojitokeza kwa nia njema na uelewa ulio sahihi kuhusu safari ya kidemokrasia ya nchi hii, na wako tayari kushirikiana na wale ambao bado hawajafahamu vya kutosha kuhusu maadili na utamaduni wa Kitanzania.

MWISHO


Imetolewa na:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI – JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

View attachment 3328439
View attachment 3328440
Sawa ngoja tuone mwisho wa hili!!
 
Waziri anayeishi kinyumba na mwanaume mwenzake Dodoma ni nani? Watanzania wanapaswa kumfahamu.

Waziri Dom.PNG
 
Bunge EU lilishakaa kwa ajili ya museveni, netanyahu!?..
Kwa hiyo mnataka nchi yetu iwe kama ya Museven

Tanzania Ina misingi yake ya Kusimamia haki tangu zamani huwezi kuzifafanisha na nchi nyingine

Ila Kuna watu wajinga wanataka kuharibu hadhi ya nchi yetu
 
Watulie wapokee agenda sita, watazileta soon.,..waache kuweweseka😆, wameshindwa kuheshimu binadamu wengine....ngoja wasaidiwe na wenzao
 
Back
Top Bottom