Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya

Angalau hapa mwanasheria nguli wa TCAA msomi Hamza Johari amefanya uzalendo unaukubalika, kutetea maslahi ya Tanzania.

Na katazo hili liwe siyo tu baina ya Nairobi na Dar es Salaam tu bali Kenya na viwanja vyote vikubwa vya kimataifa vya nchini Tanzania.

Tanzania blocks Kenya Airways flights in reciprocity dispute​

thecitizen.co.tz
https://www.thecitizen.co.tz › national
Tanzania blocks Kenya Airways flights in reciprocity dispute | The Citizen

37 minutes ago — Tanzania blocks Kenya Airways flights in reciprocity dispute. Monday, January 15, 2024.
Missing
 
Hao Punda wa Kunyaland ni kwenda nao hivyo hivyo.

Wana chuki sana na Tzn sijui Huwa yakoje
 
Sababu wao walijiandaa kutufungia, basi hata wakitufungulia itabidi na sisi tutumie angalau mwaka hivi tukijiandaa kuwafungulia...wangese sana hawa wakenya.
 
Huwezi kuunganisha mabomu madogo madogo kadhaa halafu utegemee usalama. Hizi nchi za EAC zote zina matatizo ya ndani makubwa tu. Sahihi ilitakiwa wa-draft sheria na kanuni (tena wawape third party kufanya hii kazi) halafu kuwe na ulazima wa kila nchi ku-adhere to them. Kwa mfani kuwe na kanuni kuwa kila nchi ni lazima uchaguzi uwe baada ya miaka mitano na kuwe na ukomo wa urais bila kusahau uchaguzi huru na wa haki.
 
Safi sana hiyo kitu kwenye diplomasia ya kimataifa inaitwa scratch my back I Scratch yours

Safi sana Raisi Samia uko vizuri sana kwenye hili

Nipongeze na wataalamu walioshauri uamuzi huo uchukuliwe wako vizuri kichwani

Serikali iendelee kuajiri walio vizuri sana vichwani kushika nafasi nzito Raisi hawi na kazi nzito sana

Wataalamu wamenifurahisha sana Kwa hili limeenea kiusomi,kiutaalamu na kiuzalendo
 
Kenya hufanya hujuma sana za kichini chini kufanya abiria wanaokuja Tanzania kupitia JKIA Jomo Kenyatta International Airport Nairobi kwa kuwaweka masaa kibao ili abiria hao waseme usafiri kwenda Tanzania ni mgumu sana hivyo kama masuala ya kiutalii, biashara n.k bora wamalizie Nairobi Kenya badala ya kwenda 'shamba kijijini' Tanzania ambapo usafiri wa ndege ni mgumu sana...
 


Badala ya kufungua mjadala mnazuia, wanajua connection za KQ kuja Tanzania zilivyo muhimu?
 
Wakenya hata mipakani kwao wana wasumbua sana watanzania, maafisa wana kuta wana shout unakwenda Kenya kufanya nini? Sema tu kama una kwenda kwa mchumba wako, mambo useless kuuliza vitu vya kijinga kijinga kama mtu ambae hana elimu, EAC inatakiwa irahisishe biashara na muungiliano wa watu.

Ujinga mwingine ni kuzuia kitu cha mwenzio kisiingie nchini mwako wakati wewe unapeleka katika nchi nyingine.

Hii hatua ni nzuri ambayo serikali imechukua.
 
Hongera sana Johari kusimamia taaluma,utaalamu na uzalendo vyote Kwa mpigo wengine waige kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…