Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya

Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya

Kwa mujibu wa barua ya Johari, issue yahusu ndege za mizigo lakini Tanzania yapiga ban ndege za abiria.

Hii waisoma vipi hii?
Tena wapige ban na magari ya abiria na mizigo.

Wanajidai wajanja, sasa wataijuwa Tanzania walikuwa wameisahau.
 
Kumekucha.

Kama kupata tupate wote, kwa nini unazuia ATCL isinlbebe mizigo Tanzania na kutua Kenya.

Nadhani kuna haja ya kutumia forum za kidiplomasia za EAC. Vinginevyo tuambiwe EAC imeshindwa kukutanisha viongozi wake ili kutatua mambo yao kwa amani.

======
Taarifa ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania imeeleza kuwa kwa niaba ya Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeamua kufuta vibali vya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuendesha safari za abiria kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia 22 Januari 2024

Taarifa hiyo imedai hatua hii ni baada ya uamuzi wa mamlaka ya anga ya Jamhuri ya Kenya kwenda kinyume na Kifungu cha 4 cha Mkataba wa Maelewano kuhusu Huduma za Ndege, kati ya Tanzania na Kenya yaliyotiwa saini Novemba 24, 2016 Jijini Nairobi

Kufuatia Uamuzi huu, hakutakuwa na safari za ndege za abiria kwa KQ kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 Januari 2024.

UPDATES:
- Kenya na Tanzania kusuluhisha Mzozo wa Safari za Ndege ndani ya Siku 3

View attachment 2872698
Wakati walipozuia ndege za Tz kwa kigezo cha lockdown Watz wengi walilishwa sumu kwamba tatizo ni Magufuli (roho mbaya yake) na siyo ushindani, sasa hili la leo pia Magufuli ndiyo bado ni tatizo?
 
Mama yenu si alifungua Nchi.
Alimfavour Ruto, akajiwahi kumpongeza kushinda urais wakati kesi ikingali Mahakama ya Upeo kusubiri uamuzi, acha Ruto amnyooshe.

Kenya chini ya utawala wa Ruto Tz ijiandae kulia sana. Hii ni "intro" "duction" bado.
 
Na hatuwaoi tena wakenya
Wake zenu watawafuata tu kupitia Rombo kwenda kuhemea mimba.

Mama pia alisema nyumbu wetu wa Serengeti wanaenda kuchukuwa mimba Kenya (kama vile huko ndiyo kuna madume tu), diplomasia ya uchukuaji mimba Kenya hahahaaa...
 

Taarifa ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania imeeleza kuwa kwa niaba ya Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeamua kufuta vibali vya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuendesha safari za abiria kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia 22 Januari 2024

Taarifa hiyo imedai hatua hii ni baada ya uamuzi wa mamlaka ya anga ya Jamhuri ya Kenya kwenda kinyume na Kifungu cha 4 cha Mkataba wa Maelewano kuhusu Huduma za Ndege, kati ya Tanzania na Kenya yaliyotiwa saini Novemba 24, 2016 Jijini Nairobi

Kufuatia Uamuzi huu, hakutakuwa na safari za ndege za abiria kwa KQ kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 Januari 2024
Hili jambo linahitaji high level intervention ili lisiendelee kuhatarisha EAC.
 
Good move ATCL. WaKenya ukiwachekea chekea wana janja janja nyingi sana.

Kama wamekatalia ndege za ATCL kubeba mizigo ina maana za makampuni mengine zinabeba. Why ATCL akataliwe?
Ila tukumbuke hasara ni kubwa kwa Tz kuliko Kenya kwa sababu licha ya JKIA kuwa ndogo kwa JNIA; JKIA ni Hub. Ukizuiliwa ku-access Hub umeuawa kibiashara. Tupambane JNIA iwe Hub kwa sababu kwa ujenzi wake, ni ya pili kwa idadi kubwa ya abiria inayotakiwa kuhudumia kwa mwaka nyuma ya Oliva Tambo International Airport. Tatizo kwa serikali ya CCM yetu hili hili ni gumu kutekelezeka.
 
Wakati walipozuia ndege za Tz kwa kigezo cha lockdown Watz wengi walilishwa sumu kwamba tatizo ni Magufuli (roho mbaya yake) na siyo ushindani, sasa hili la leo pia Magufuli ndiyo bado ni tatizo?
Haiondoi ukweli kwamba JP waa a blood sucking monster
 
Hii Jumuiya kila mtu ashike lake tu kwa sasa
Mbona wanachama wapya wanataka kujiunga Ethiopia, Djibouti na Somalia na kufanya EAC consumer market kuwa na watu 800ml sawa na 57.14% ya watu wa Uchina.

Ila cha ajabu, nchi za vita na migogoro ndizo zinajiunga EAC.
 
Safi sana hiyo kitu kwenye diplomasia ya kimataifa inaitwa scratch my back I Scratch yours

Safi sana Raisi Samia uko vizuri sana kwenye hili

Nipongeze na wataalamu walioshauri uamuzi huo uchukuliwe wako vizuri kichwani

Serikali iendelee kuajiri walio vizuri sana vichwani kushika nafasi nzito Raisi hawi na kazi nzito sana

Wataalamu wamenifurahisha sana Kwa hili limeenea kiusomi,kiutaalamu na kiuzalendo
Ila mkuu tukichunguza kiumakini bado tuna hasara Tz kuliko Kenya kwa vigezo vifuatavyo:-

1. Watalii wanaokuja direct Tz toka ng'ambo ya bahari wanatumia KQ na mashirika mengine yanayotumia JKIA kama Hub ya EAC Corridor.

2. ATCL inawindwa kila kona duniani kukamatwa kufidia madai hivyo hata ku-fly overseas i.e. Europe na Americas kuleta watalii ni shida.

3. National Carrier yetu ita break-even-point 2032 wakati KQ inaingiza faida (waliishatoka kwy ku-break-even-point miaka mingi).

4. ATCL imejaa wenye njaa na machawa tu wasioweza kufikiri kiushindani na kimkakati dhidi ya KQ.

NB.
Kesho KQ ikielemewa tena wata impose ban mara ya 3.

Nadhani ATCL iingie mkataba na Ethiopian Airlines ku-fly route ya JKIA kwa niaba ya ATCL ili wagawane mapato wakati huo huo Tz iendelee kuiadabisha KQ kwa zuio.
 
EAC ni muungano wa kihuni sana na utasambaratikaga kihuni sana,Rwanda na Burundi wana bifu,Rwanda na Congo bifu,Uganda na Kenya bifu ya biashara ya mafuta na sasa Kenya na Tanzania tena. Muungano kama EU wana mashariti magumu sana kupokea wanachama,ndio maana huwezi sikia wanakwaruzana wao kwa wao.EAC ni muungano wa kihuni
Hujui undani wa migogoro ya EU, BREXIT ni zao la mivutano!
 
Back
Top Bottom