Tanzania yenye vyama vingi vya siasa, sawa na Tanzania isiyokuwa na vyama. Nini tatizo?

Tanzania yenye vyama vingi vya siasa, sawa na Tanzania isiyokuwa na vyama. Nini tatizo?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
Wana JF,
SALAAM!

Nawauliza kuna tatizo gani nchini KWETU hususan kwa hawa wanaojiita watetezi wa wananchi kupitia forums za vyama vya siasa. Naona kila jambo linaloanzishwa na Serikali liwe zuri au baya linapita bila kikwazo.

Mfano:-
(a). Tozo. - hizi zimeanzishwa kimzahamzaha lkn mwisho wake zimepenya na kuwa mwiba kwa wananchi. Hakuna uhalali wa kuanzia rundo la vikodi ktk mazingira ambayo uchumi unakumbwa na anguko;

(b). Miamala ya simu - hii nayo imeingiziwa na wachumi uchwara kwa madai ya kuongeza mapato ya Serikali lkn wakati huo mzigo ukibebwa na walalahoi. Watu wamepiga yowe lkn vyama viko kimya, SASA MBONA SIONI DHIMA YA KUANZISHWA KWA VYAMA VINGI!

(c). Miamala ya benki - hii imepita na watumiaji wa benki kuanza kukatwa fedha isivyo halali kwa kuwa fedha hizo kwa mfanyakazi anakuwa ameshakatwa kodi, kwa mfanyabishara anakuwa ameshalipa kodi - SASA vyama vimefyata mkia as if hili jambo ni zuri;

(d). Kikokotoo - kimeletwa kikilenga watumishi wa umma zaidi. Mtu afanye kazi hadi at age ya 60 halafu pension yake uikate na kubaki nayo huku ukimlipa mafungu mafungu. Hili ni unyanyasaji na ukilitimba dhidi ya watumishi. SASA VYAMA VINGI VYA SIASA NCHINI VINA MSAADA GANI KWA WANANCHI?

Nimeandika haya nikipenda vyama vijitathmini na kujikosoa vinginevyo ruzuku zetu wanazokula ni moto wa laana utakaowalamba.

Msakila M Kabende
Kakonko - Kigoma.
 
... wapinzani wakinyanyaswa hujawahi kunyanyua mdomo japo kukemea. Yamekufika (hayo uliyotaja) ndio unalaumu wapinzani. Wapinzani si walituchelewesha sana? Twendeni na CCM chama kinachowajali wanyonge!
 
Katiba iliyopo ina demokrasia ndani ya chama kimoja chama dola. Haya ya vyama vingi yaliletwa kwa shinikizo na matakwa ya IMF na mabeberu wengine ili tupate misaada zaidi.

Sent from my Infinix X605 using JamiiForums mobile app
 
Wakina Mbowe wakibambikiwa kesi za michongo ulinyamaza kimya.

Lissu akitandikwa mirisasi kedekede uliona sawa ni kama movie za kina Rambo.

Wapinzani wakibambikiwa kesi za mauaji na wengine mpaka leo hawaonekani uliona sawa.

Lipa tozo ndio ujue faida ya upinzani.
 
Back
Top Bottom