Tanzania yetu ina majasusi wa aina gani?

Status
Not open for further replies.
Wenzetu wanayojua shughuli hizo husaidia sana nchi zao. Sasa nyinyi ndugu zangu mnaolaumu ujasusi wa Tanzania mnanyeti gani ambazo zitasaidia uchumi na maendeleo ya bongo licha ya kuwa yawezekana kabisa kuna mambo chungu mzima yako mbele ya macho yenu huko mliko ambayo yangenufaisha nchi yenu lakini aidha hamyaoni. au mnapuuzia. Jasusi wa uchumi au biashara hana haja kuwa na uhusiano na chama au serikali bali husukumwa kwa uchungu na mapenzi na nchi yake.
 
Hapa hakuna majasusi. Waliopo ni informers tu. Kwanza jasusi huwezi kumjua kwa sababu anafanya kazi kwa usiri mkubwa, hio ni sifa ya kwanza. Pili, ni 'intelligent' sana, anajua mambo mengi nk. Hapa watu wanaona ujiko kujulikana tu ni informer.
well said halafu kutwa kujitaja,na kujisisfia.hata shule hakuna
 

Mzee Mlowezi,

How was it possible for Tanzania to fall victim of disintegrating under EAC, while at the same ina mashushushu?

-- Mlenge
 
Mi nadhani swala la ujasusi wa kiuchumi linapaswa kufanywa na wizara husika katika maeneo yao, kwa mfano hilo la kujengwa kiwanda cha kukata dhahabu Uganda wizara ya madini ilipaswa kulifahamu. hili linawezekana kama kutakuwa na kitengo maalum cha kufuatilia kitu gani kipya chaja kwenye sekta yao.
Mfano katika kampuni nilizo bahatika kufanyia kazi kulikuwa na vutengo hivyo ambavyo kazi yake ni kukusanya taarifa za soko na kuziweka kwenye mtandao kwa watu wote kuona na kuzifanyia kazi, kwa kufanya hivyo kazi ya kufanya maamuzi inakuwa rahisi maana unakuwa na taarifa mapema kuhusu soko
 
Zamani hii kazi ya UWT ilionekana si lolote si chochote, ni kazi ya hali ya chini na watu wasiokuwa na elimu . Mtu alikuwa akishindwa kabisa ndiyo , anapepesukia huko hivyo ilikuwa katika daraja la kazi za uaskali kwa mtizamo wa wengi na hakuna ntu aliyeitaka. Kwa hali hiyo watu wengi wenye madaraka huko leo ni wale darasa la saba ama fomu 4 feliea na wanaogopa sana vijana wenye elimu nzuri kuingia huko maana watawapindua . Usitegemee kabisa hawa UWT waweze kufanya kazi za kitaalamu za kuleta maendeleo Tanzania,wanachofanya ni kazi ya uifoma tu, Lakini ukisoma historia ya mashirika ya ujasusi ya nchi zilizotaka maendeleo na kuyapata utaona katika idara hii inatakiwa taalumu hasa na wala si kujuana kama ilivyo hapa kwetu. Huko ughaibuni library unaweza ukaona vitabu ambavyo hapa Bongo unaweza kuambiwa ni siri kuhusu haya mashirika ya ujasusi.
 

Kuna mwana JF. Jana aliuliza swali linalosema kuwa kazi ya usalama wa Taifa ni nini? Na mada hiyo ilionekana kuwavuta watu wengina wengine walikuwa wanatoa mchango kulingana na mawazo yao lakini
Nashukuru kuona humu ndani kuna watu wenye akili na kujua kuyachumbua mambo kiundani zaidi na hiki alichosema mchangiaji huyu wa mwisho hapa una ukweli kwa sehemu kubwa na ndipo mahali tulipopoteza mwelekeo maana kama Idara hii ingefanya kile ambacho kinafanywa na nchi mbalimbali kwa manufaa ya nchi zao tungekuwa mbali sana kimaendeleo na kama idara hii ikiwa imara hakuna kinachoshindikana kwenye nchi kama hii yenye rasilimali nyingi sana za asili na kwa wanaojua kuzitumia idara hizi vizuri hata kunapotokea vita wao wanaweza kumaliza vita kirahi sana kama waisrael bila kuingia gharama kubwa ya vita ila huku kwetu majungu yamezidi na wanaopewa kazi nzuri na za ngazi ya juu ni wale tu ambao ni waoga hawawezi kuuliza chochote kuhusu serikali iliyoko madarakani
 
umenikumbusha mtaalamu mmoja wa mambo ya intelijinsia alisema kuwa asilimia 90 ya taarifa zinapatikana bure lakini umuhimu wake ni 10% wakati 10% inaweza kupatikana kwa kazi nzito na umuhimu wake ukawa 90%.
Labda tujiulize watu wa usalama wetu wanafanyia kazi taarifa zipi? Zinazopatikana almost bure au zinazopatika kwa jasho?
 
well said halafu kutwa kujitaja,na kujisisfia.hata shule hakuna

... usitukane wakunga...
waachie wenyewe TISS. Ila kidogo tu, wapo watu ambao ni extremely, narudia extremely blessed ndani ya chombo hicho.
Wewe mwenyewe jaribu kujibu, which comes first, the egg or the chicken halafu utofautishe soksi unazovaa (si condom) ipi ya kushoto na ipi ya kulia. Ukipata jibu, sasa uongeze hapo, nani ana husika na sera na visheni, na kwa hiyo majibu yapo hapo hapo.
 

dah, hili jibu limeniuma sana.....naomba isiwe kweli
 
halafu kuna watu wanapenda kutishatisha wenzao humu ndani.....yaani wanaboa......nia ni kujifunza na kuelewa ili tuweze kufanya maamuzi ya ukweli....sio kutishanatishana na kufanya watu waogope kujifunza.....elimu ni muhimu sana jamani....tuelimishane bila kutishana
 
Tanzania ina majasusi ambao kazi yao ni kuchumia tumbo wala sio kujali maslahi ya watz. Kazi yao kubwa ni pamoja na kuiba kura,kuiba rasilimali za taifa na kusema ni siri kubwa, kulinda wanasiasa wa ccm, kuiba mali ya umma
:A S angry:
 

Una hoja lakini hii ni kumpigia mbuzi jitaa (Guitar) unategemea aondoke miondoko ipi. Majasusi wa Tanzania ni wa kufuatilia nani anahatarisha nafasi ya Lowasa kuwa Rais 2015 au ni vipi tunaweza kuchakachua matokeo. Kuna vijana wangapi wa Tanzania wapo nje hawapewi nyenzo na uwezo wa kuweza kuiba teknolojia kwa ajili ya nchi yetu? Hivi karibuni kulikuwepo scandal ya kijasusi kati ya Marekani na Russia...Miongoni mwa spies ni wale ambao walikuwepo rasmi kujua sera za Ikulu ya Marekani na hivyo kujipanga katika masuala ya policies (hii ni pamoja na technolojia na uchumi). Sisi tukienda mbali sana ni kujaribu kujua Kenya wana silaha zipi...lakini uchumi wao vipi it is not our business!
 
hapa hakuna ujasusi wa uchumi kuna ujasusi wa kujua kula za wapinzani zitakuwa ngapi!
 
Wao majasusi sisi informers.
 
usisahau kupiga picha na wasanii wa america na kuletewa jezi za wachezaji wa futiboli. pathetic
 

Kiwanda tunacho pale Iringa Tancut Almasi. Tunahitaji pesa kidogo tukikarabati mambo yawe mswano
 
wako hapa majasusi wetu na wanatusikia kiundani.hata hvyo kinachoharibu idara hii ni nidhamu ya chama badala ya nidhamu ya taaluma wanaangalia zaidi ni jinsi gani ccm itaendelea kua madarakani na sio usalama wa taifa kama agenda yao ilivyo
 
Mzee Mlowezi,

How was it possible for Tanzania to fall victim of disintegrating under EAC, while at the same ina mashushushu?

-- Mlenge

Well said Mlenge
 

Swala la tax holiday lilisharekebishwa,kampuni ambayo inapewa tax holiday inatakiwa kulipa kodi kama kawaida kwa kile kipindi cha msamaha ambayo inakuwa kama dhamana just incase akiondoka tunakuwa tumepata kodi yetu.Mda wa holiday ukiisha kile ambacho atatakiwa kulipa kama kodi kinapunguzwa kutoka kwenye hela aliyokuwa amelipa hivyo hivyo mpaka hela aliyolipa mwanzoni ikiisha ndio anakuwa analipa.Na hii ni pale kampuni inapokuwa inaanza operation TZ kwa mara ya kwanza tu,hizo style za kubadilisha majina hazina taabu tena wanapouziana serekali inakula kodi,mfano zain kuuzwa kwake si tz tu ni duniani kote mmiliki anabadilika ktk biashara ni kitu cha kawaida.Pia kuna restriction za misamaha inayotokana na EA community,lakini tatizo hapa kwetu inaonekana hili la pili bado halifuatwi sana kwani bado kuna misamaha holela.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…