Sidhani kama tanzania tunahitaji ujasusi ili tupige hatua kutoka hapa tulipoi tangu uhuru......naamini ujasusi ni hatua ya juu kabisa na matatizo yetu watanzania ni ya kipekee kabisa na hayahitaji ujasusi.......tukizingatia yafuatayo tutaondoka kwanza hapa tulipo na ndipo baadaye nasi tutakuwa na uwezo na nafasi ya kufanya ujasusi.........
"tanzania ina kila baraka kutoka kwa mungu"...sina haja kuzitaja kwani karibia kila siku wanaharakati wanasiasa na hata kikwete mwenyewe alipokuwa anaaingi madarakani alisema "kwa tz yenye neema inawezekana"...rais anajua nchi ina neema na ndivyo mungu alivyo tupa...lakini rais huyohuyo anapoulizwa na wale wanaotufadhiri chanzo cha umasikini anasema hajui kwa nini na hachukui hatua za makusudi kuondoa umasikini.......
"nasikia ikijakutokea miujiza siku moja tukaamka asubuhi tukajikuta watz wote tupo marekani(usa) na wamarekani wote wakajikuta wapo tanzania na tukapeana miaka mitatu tu......matokeo yake marekani itageuka kuwa km tz ya sasa na tz itageuka kuwa zaidi ya marekani ilivyo sasa"...kwa nini inaweza kuwa hivyo kwa sababu viongozi wetu wa sasa wanajua kupanga matumizi yasiyo ya maendeleo...nakumbuka wakoloni walituachia viwanda vingi sana ambavyo vilikuwa vinaliingizia taifa pesa nyingi na vilisaidia sana kupunguza tatizo la ajiras nchi......natamani wakoloni wangekuja wajenge viwanda ili mradi tupate ajira na serikali ipate kodi
1.kwanza tunahitaji viongozi waadilifu na ambao wako tayari kuweka mbele maslahi ya taifa...kuanzia rais na wafuasi wake
2. Selikali kama ya tanzania ina matumizi na matanuzi makubwa sana wakati bajeti yetu inategemea wafadhiri ambao serikali zao zina matumizi na matanuzi madogo......(fikiria uingereza ambayo ni mfadhiri wetu mkuu, waziri mkuu amependekeza kupunguza matumizi kwa kukata mishahara na marupurupu wkt tz masikini wa kutupwa rais wa nchi anatapanya mali ndogo za nchi kwa anasa
3. Tukajifunze kwa wenzetu kuhusu uwekezaji na wenzetu wana masharti gani kwa wageni wanaotaka kuwekeza na serikali inanufaika vipi na uwekezaji, tusiende china tuende nigeria,kenya, zambia kwani kutoka kenya tunapata vikombe vya plastic na tooth stick......tukaangalie huko ili nasisi tuondokane na ujinga wa mrahaba wa 3%(ajabu duniani)
-sijawahi kuona mantiki yoyote ya kugawa mikoa na wilaya na majimbo ya uchaguzi kwani hii ni kuongeza mzigo wananchi kwani huko kote kunahitaji gharama kubwa.....hakuna takwimu zozote hapa tanzania zinazoonesha kuwa mikoa midogo ina maendeleo makubwa kuliko mikoa mikubwa au wilaya ndogo zina maendeleo makubwa kuliko zile ndogo na kadhalika...hapa ni matakwa tu ya viongozi wetu ili mradi waonekane wamefanya kitu fulani hata kama ni cha kipumbavu
-baraza letu la mawaziri ni kubwa mno kuliko hata mabara ya wafadhiri wetu na lina hitaji fedha nyingi kuliendesha wakati rais wa nchi hayuko kuwawajibisha hata pale wanapoamua kusaini mikataba usiku na nje ya nchi.......haya yote ni matumizi yasiyo ya lazima ...linatakiwa baraza dogo na lenye tija...
-bado kikwete haamini kuwa viongozi wanaishi kwa mishahara na marupururpu ya anasa kupindukia na hayuko tayari kupunguza mshahara wake na wa wasaidizi wake ambayo ni mikubwa sana,,,,,,,sitaki kutaja mishahara yao hapa kwani wananchi wengine wakijua sana wana ghadhabu kupita kiasi na si vizuri watu km hao wakajua sana kwani wanaweza kuasi
-hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa wezi wa mali ya umma, wanaendelea kutanua na rais ananendelea kuwakejeli watz kwa kuwasafisha na hata wengine ambao kesi zipo mahakamani.....nchi haiwezi kuendelea na tunahitaji majasusi wa kuwafanyia ujasusi viongozi wetu ili kuwajua kama kweli wana nia ya dhati ya kutukomboa ana wana lao jambo km kikwete anavyopenda kusema..........
-kikwete alipoingia madarakani 2005 kitu cha kwanza alichofanya ni kuangalia namna gani atarudisha fadhira kwa marafiki zake......kitu cha kwanza kufanya yeye lowasa,rostamu waliamua kujitengenezea kampuni feki ya richmond na kuwaibia watz 152,000,000 kila siku.........baada ya hayo unatakiwa ujasusi kujua kikwete kwa sasa anataka kuwapa fadhira watu wa kundi gani? Makundi ya dini?...dini gani? Kwa nini?...marafiki zake?...familia yake?...tumfanyie ujasusi....tukifanya hivyo tutaepusha mengi....
-nchi haina dira kila kiongozi akiingia anaendesha nchi kama wamasai wanavyoswaga ng,ombe....tumefikia mahali rais anaangalia nani wa upande wake na nani wa upande wa yule .....hatuhitaji ujasusi ktk haya
naamini nimewachosha sana...poleni sana hii ni kwa sababu ya machungu nani nawakilisha machungu ya wengi ukiwemo wewe unayesoma either ni ccm,chadema au.....