Tanzania, Zanzibar zasaini Hati ya Makubaliano Sekta ya Madini
Hivi hii ni Awamu ya 5 au ya 6?

Mbona Kuna namna Fulani wanatengeza mazingira kuvunja Muungano?

Hawatofanikiwa.

NDOA sie ni Moja, HATUACHANI Hadi kifo kitutenganishe🙏🙏🙏

For BETTER for WORSE.
 
Mafuta sio madini ?....maana huitwa dhahabu nyeusi....yakipatikana huko Zenji huenda yakajumuishwa kwenye hayo makubaliano ?

Nguruvi3 Kalamu Pascal Mayalla zitto junior
Mafuta siyo madini! Ndiyo sababu zamani tulikuwa na wizara moja inaitwa "Maji, Nishati na madini. Kwa maana hiyo mafuta yako kwenye kundi la Nishati.

Pili Biteko hashughuliki na mafuta, yeye ni Waziri wa madini yaani kwa maneno mengine anashughulika na vitu vyenye asili ya mawe!

Zanzibar haina madini ya kutosha zaidi ya kuwa na kiasi kidogo cha mawe na mchanga ambavyo havitoshelezi kwa matumizi yao.

Kwa hiyo mkataba huu wa Zanzibar na Tanganyika unahalalisha Wazanzibari waje huku Tanganyika kujichotea mchanga na mawe bure! Huu ni wizi mwingine tuchukue tahadhari!

Wizi! Wizi! Wizi! Tuchukue hatua!
 
Tanzania, Zanzibar? Siyo Tanganyika, Zanzibar?

Huu muungano mugumu kuutafsiri.
Kweli maana hii ni Jamhuri ya Muungano WA Tanzania kwa maana pana nchi mbili humo ila ingelikuwa Jamhuri ya Muungano YA Tanzania hapo ingekuwa na maana nyingine kabisa.
 
Hapo siyo kuna njia inatengenezwa kwamba Zanzibar ikianza kuuza dhahabu au Tanzanite nje ya nchi ionekane kuna mashirikiano na ni kitu kimoja? Au huko Zanzibar napo kuna madini?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Hapo siyo kuna njia inatengenezwa kwamba Zanzibar ikianza kuuza dhahabu au Tanzanite nje ya nchi ionekane kuna mashirikiano na ni kitu kimoja? Au huko Zanzibar napo kuna madini?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Nadhani Zanzibar itaomba kupewa baadhi ya migodi. Hata wakipewa mgodi mmoja tu unatosha kuwalisha wote 1.8ml idadi yao. Ila ni aibu ka-nchi kama tarafa tu kale kuipigisha kwata Tanzania ya watu 61ml (Zanzibar kuikolonisha Tanzania).

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
wakati tukiendelea kustaajabu kwamba iliwekana vipi zimwi hili lilipata ithibati timilifu kutoka ofisi tukufu na nyeti ndani ya JMT, kwa mkataba wa kimangungo wa aina yake katika karne ya 21. huku wapiga debe na wasemaji wakuu wa DPW wakiwa wametapakaa Tanganyika nzima, kutuelimisha sisi tusiojua umuhimu wa uwekezaji, na tusiojua kutafsiri mikataba na tunaopotosha watu, na kujinasibu kuwa tutapata trilioni 26, tukiingia kwenye mkataba huu na vifungu na vifungu vya mkataba havina shida kabisa.

Sasa tunayaona makubwa mengine ya Mkataba wa Kizimkazi, yaani Tanzania imeingia mkataba na Tanzania, kwenye sekta ya madini ili kuinufaisha Tanzania.

tuendeleeni na tution mitihani ipo karibu|||

Mungu Ibariki Tanganyika na watu wake
 
Hatupoi kwenye DPW, hata waingie mkataba wa kilimo dar na mwanza sisi ni mbele kwa mbele, hawatutoi nasema Tena hawatutoi, pumbavu
 
Hivi ni kwanini kuitaja Tanganyika km ni kosa wakati huohuo kuitaja Zanzibar ni fahari?
Tuachane na hayo.
Zanzibar wanamadini gani hadi tuingie mkataba wa kushirikiana nao?
 
Sijui hawa wanajeshi wanangoja nini ?!?!?
Haa haa haa haa haaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Wapindue?
Wewe kweli poyoyo.
Tanganyika imeolewa na Zanzibar ndio maana Jina lake limepotea.
mfano Grace akiolewa na John.
Grace ataitwa Mrs. John na John Ataendelea kuitwa John.

Eleweni Musio kuwa na Macho.

Vya Tanganyika Ni vyetu wote , Vya Zanzibar Vyao peke yao.
Hivi ndivyo alivyotaka Nyerere.
 
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya wizara hizo mbili zilizopo katika upande wa Muungano ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari, 2023 jijini Arusha ya kushirikiana kwa lengo la kufanya madini yaliyopo katika maeneo husika yaweza kuleta manufaa kwa pande zote mbili.

Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo ya Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam Dkt. Biteko amewataka watendaji wa wizara hizo kusimamia utekelezaji wa makubaliano

“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalitupa dira mpya katika kuendeleza mashirikiano yetu, hivyo tulichosaini leo sio kwa ajili ya kupiga picha bali ni kwa ajili ya kazi tuliyojipatia, natamani kuona mambo tuliyosaini hapa yanakuwa mfano na yanafanyika kwa weledi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili,” amesema Dkt. Biteko

Aidha, Dkt. Biteko amewataka watendaji wakuu wa pande zote mbili kusimamia masuala hayo ili yaweza kutokea huku akitaka kuanza kusimamia masuala ambayo hayahitaji rasilimali fedha kubwa ikiwemo kufanya tafiti hivyo yale yanayowezeka yaanziwe kufanyiwa kazi leo na sio kungoja.

Pia, amewataka Makatibu Wakuu wa pande zote mbili kutengeneza timu ndogo ya kusimamia makubaliano hayo ili kuhakikisha ushirikiano huo unadumu na kuwa wa mafanikio katika pande hizo mbili.

Naye, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaibu Hassan amesema utiaji wa saini wa makubaliano hayo usiishie kwenye makaratasi bali ufanisi na utendaji unaotakiwa kuonekana ukaonekane.

“Kitendo kinachofanyika leo ni kitendo muhimu sana kwa kwa pande zote mbili ambapo viongozi wetu wa juu wamekuwa wakitusisitiza kuendeleza mashirikiano ambapo tunategemea kushirikiana hasa katika suala la utaalamu hususan katika kufanya tafiti kwa pamoja,” amesema Hassan.

Pia, Hassan amesema ushirikiano huo utazaa toka kwa pande zote mbili za muungano na kuwataka watendaji wa wizara yake kufanya kile kinachowezekana kunyika leo na wasingoje kesho.

Jumla ya Hati Tano za Makubaliano zimesaniwa kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara ambazo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Mafuta, Madini na Gesi Asilia, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Kituo cha Jemolojia na Tanzania (TGC)
Kumbe wanao dai Tanganyika wapo na haki hakuna muungano hapa nchi moja msaini mkataba kivipi?
 
Zenji kuna mgodi wa ngisi na pweza tutabadilishana na dhahabu na tanzanite. Stupid
 
Back
Top Bottom