Swali gumu hili Kwa uongozi wa nchiNikawazaaaa nikashindwa kujiuliza, ni lini Tanganyika nao watasaini mkataba au Makubaliano yoyote tu na serikali ya Tanzania??[emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali gumu hili Kwa uongozi wa nchiNikawazaaaa nikashindwa kujiuliza, ni lini Tanganyika nao watasaini mkataba au Makubaliano yoyote tu na serikali ya Tanzania??[emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana hii mada ya utanganyika wa Tanzania umeanza kuijua kwenye mada hii lakini subiri nikupe mwangaza kidogo.Jinga hilo. Halijui Nyerere alipewa uhuru wa Tanganyika na hao anaodai Waingereza?
Kwa maana kwamba chochote kinachotoka au kuzalishwa Tanganyika ni cha Zanzibar..hata yasiporudishwa wana mrija wa kufyonza kwasababu mafuta yaliyoko Tanganyika ni ya serikali ya muungano.
Najaribu kuwaza kwamba Zanzibar Iliungana na Tanzania Kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au Zanzibar Iliungana na Tanganyika Kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?Inaonekana hii mada ya utanganyika wa Tanzania umeanza kuijua kwenye mada hii lakini subiri nikupe mwangaza kidogo.
Wenzako wanaotaka uwepo wa Tanganyika au Serikali ya Tanganyika msingi wa hoja yao ni kwamba Tanganyika ndio nchi iliyopewa uhuru na Kwa msingi huo ni mwingereza ndio anaplay part kubwa kwenye mjadala wa nchi ya Tanganyika.
Ndio maana nikauliza swali, ni mwingereza ndio aliyeipatia uhuru nchi ya Tanganyika na angetamani kuiona nchi ya Tanganyika kuliko Tanzania, je akiulizwa Sasa hii nchi Gani atajibu ni ipi? Kama Sasa akijibu ni Tanganyika basi nitakubaliana na wanaotaka serikali ya Tanganyika lakini kama watajibu ni Tanzania basi kudai serikali ya Tanganyika ni uhaini.
Mwingereza ndio aliyemsaidia mzanzibar kuondoa utawala wa kisultani katika mapinduzi matukufu 1964. Kama unadhani Tanzania Ipo Kwa bahati mbaya na jaribu kutafakari hicho kitu.
Achana na kukosa kupinduliwa, John Kennedy anayetambuliwa kama Rais kipenzi wa wamarekani aliuawa ndani ya nchi yake Tena publicly.Nyerere hakuwa akili kubwa
Ndio maana alikosa kupinduliwa mara kadhaa.
Nyerere alikuwa ni muota ndoto wa mchana na Kuna mtaalamu aliwahi kumuelezea hivyo.
Kifupi katupa dhahama ambayo tusipoikabili Sasa basi baadae itatupasa
Bila Muungano huu Sultani angerudi Zanzibar na pengine Sasa kungekuwa na Usultani visiwani humo. Kama angerudi Zanzibar uhuru uliopata Zanzibar 1963 usingekuwa na maana na haukuwa na maana mpaka yalipofanyika mapinduzi mwaka 1964.Najaribu kuwaza kwamba Zanzibar Iliungana na Tanzania Kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au Zanzibar Iliungana na Tanganyika Kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama Iliungana na Tanganyika na Zanzibar inasaini mkataba na Tanzania basi na Tanganyika inaweza kusaini mkataba na Tanzania.
Labda kama waingereza waliipata Uhuru Tanzania halafu hiyo Tanzania ikaungana na Zanzibar ila kama walipata Uhuru Tanganyika basi inabaki iliyopewa Uhuru ni Tanganyika sio Tanzania.
Muungano wetu unamambo ambayo bado ni magumu yanahitaji utatuzi au kuurekebisha muundo na Mimi napendekeza tubaki na serikali moja ili tuwe wamoja zaidi lasihivyo tutabaki na umoja wa makaratasi ila nafsi hazina umoja.
Zanzibar hawataki au wajukuu wa Sultan ndo hawataki?..Znz hawataki ushirikiano ktk mafuta ndio maana walishinikiza yaondolewe ktk masuala ya muungano.
Sijui ni nani ambaye ni mwasisi wa mamikataba ya hovyo. Moja ya mkataba wa hovyo (kama upo) basi ni pamoja na muungano usiokosa kero. Shuleni tuliambiwa Tanganyika + Zanzibar = Tanzania. Wakati huohuo tunaambiwa Tanzania na Zanzibar zimesaini... Tanganyika yangu. Kwanini ulihadaiwa na ukakubali kufa?.Tanzania, zanzibar? Siyo Tanganyika, Zanzibar?
Huu muungano mugumu kuutafsiri.
Kwanini unafikiri angekuwa na tamaa yakuikalia Tanganyika? Kwanini hufikiri angetamani Kenya, Mozambique au Comoro? Huu muungano ni wakulazimishana. Sababu zilizopelekea muungano 1964 zilishapitwa na wakat. Kwa sasa sio wazanzibar wala watanganyika wanaoupenda. Nashauri iitishwe kura ya maoni kuhusu muungano huu. Muungano na mwenge ndiyo mambo yanayonishangaza sana.Mwarabu ana tabia ya kujitanua Zaidi, asingeridhika kuikalia Zanzibar angekusanya nguvu ya kuikalia Tanganyika pia. Sidhani kama wote wanaowaza ya Tanganyika wanaangalia yote hayo.
Unataka kutuambia Zanzibar imekuja kuwekeza Tanganyika?Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya wizara hizo mbili zilizopo katika upande wa Muungano ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari, 2023 jijini Arusha ya kushirikiana kwa lengo la kufanya madini yaliyopo katika maeneo husika yaweza kuleta manufaa kwa pande zote mbili.
Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo ya Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam Dkt. Biteko amewataka watendaji wa wizara hizo kusimamia utekelezaji wa makubaliano
“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalitupa dira mpya katika kuendeleza mashirikiano yetu, hivyo tulichosaini leo sio kwa ajili ya kupiga picha bali ni kwa ajili ya kazi tuliyojipatia, natamani kuona mambo tuliyosaini hapa yanakuwa mfano na yanafanyika kwa weledi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili,” amesema Dkt. Biteko
Aidha, Dkt. Biteko amewataka watendaji wakuu wa pande zote mbili kusimamia masuala hayo ili yaweza kutokea huku akitaka kuanza kusimamia masuala ambayo hayahitaji rasilimali fedha kubwa ikiwemo kufanya tafiti hivyo yale yanayowezeka yaanziwe kufanyiwa kazi leo na sio kungoja.
Pia, amewataka Makatibu Wakuu wa pande zote mbili kutengeneza timu ndogo ya kusimamia makubaliano hayo ili kuhakikisha ushirikiano huo unadumu na kuwa wa mafanikio katika pande hizo mbili.
Naye, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaibu Hassan amesema utiaji wa saini wa makubaliano hayo usiishie kwenye makaratasi bali ufanisi na utendaji unaotakiwa kuonekana ukaonekane.
“Kitendo kinachofanyika leo ni kitendo muhimu sana kwa kwa pande zote mbili ambapo viongozi wetu wa juu wamekuwa wakitusisitiza kuendeleza mashirikiano ambapo tunategemea kushirikiana hasa katika suala la utaalamu hususan katika kufanya tafiti kwa pamoja,” amesema Hassan.
Pia, Hassan amesema ushirikiano huo utazaa toka kwa pande zote mbili za muungano na kuwataka watendaji wa wizara yake kufanya kile kinachowezekana kunyika leo na wasingoje kesho.
Jumla ya Hati Tano za Makubaliano zimesaniwa kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara ambazo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Mafuta, Madini na Gesi Asilia, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Kituo cha Jemolojia na Tanzania (TGC)
Sasa sijui umejibu nini?Achana na kukosa kupinduliwa, John Kennedy anayetambuliwa kama Rais kipenzi wa wamarekani aliuawa ndani ya nchi yake Tena publicly.
Mfano wa pili, Mungu ambaye ni mkamilifu kwenye Kila kitu na uwezo juu ya Kila kitu hakukubalika Kwa viumbe alivyoviumba mwenyewe na wakafanya uasi wa kutaka kumpindua.
Nimetumia mifano hiyo miwili ili utambue matamanio na tamaa ya mtu inapokuwa kubwa anaweza kujaribu kufanya lolote. Mwalimu kukosa kupinduliwa na hakupinduliwa ni jambo kubwa Kwa sababu majaribio ya mapinduzi au mapinduzi yamemaliza na kuharibu tawala nyingi mno duniani.
Hii ni hofu isiyo na mantikiBila Muungano huu Sultani angerudi Zanzibar na pengine Sasa kungekuwa na Usultani visiwani humo. Kama angerudi Zanzibar uhuru uliopata Zanzibar 1963 usingekuwa na maana na haukuwa na maana mpaka yalipofanyika mapinduzi mwaka 1964.
Ili kuondoa uwezekano wa Usultani kurudi Zanzibar Muungano wa aina uliopo ndio ukaonekana unafaa Zaidi.
Mwarabu ana tabia ya kujitanua Zaidi, asingeridhika kuikalia Zanzibar angekusanya nguvu ya kuikalia Tanganyika pia. Sidhani kama wote wanaowaza ya Tanganyika wanaangalia yote hayo.
KaribuMaalim nakuja huko
Mpaka sasa wajenzi wa Zanzibar wanatoa mchanga Dar ambayo ni madiniNdio mtajua Yule mama interest zake zimelalia Zanzibar, anaona Zanzibar I milk tanganyika kwa kigezo cha muungano
Ushirikiano ktk utafiti wa madini kaka ikiwemo gesi nk. Hujaelewa nini mkuu. Kumbuka Zanzibar haijawahi kufanyiwa geological survey ya madini kwa undani zaidi. Yapo madini yanapatikana kwenye fukwe za bahari na mengine deep Sea. Sasa huku bara TAASISI ziko vizuri zaidi kuliko visiwaniHizo Saini Sawa...., Je tunaweza kuona tunacho-sign ?!!! Kama wanasign kwa niaba yetu ni vema tukafahamu tunakubaliana nini ?
Yaani kama tukijiuliza the Begging of an End ya Huu Muungano ni mambo kama haya....