antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 47,274
- 126,778
Hilo ndiyo lengo.ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari, 2023 jijini Arusha ya kushirikiana kwa lengo la kufanya madini yaliyopo katika maeneo husika yaweza kuleta manufaa kwa pande zote mbili.
Zanzibar hawataki au wajukuu wa Sultan ndo hawataki?
Na kwa bahati mbaya ni kwamba majority hain ufikiri mzuri kuliko minority...majority ya Waznz bila kujali wana Uarabu au Utanganyika hawautaki muungano.
..Tume ya Warioba ilitoa pendekezo la serikali 3 kupooza madai ya Zanzibar huru, au muungano wa mkataba.
Jaribu kujiheshimu kwanza. Vivyohivyo kuwapa mababu zako sifa zao stahiki. Uhuru wetu ulipiganiwa. Na ulipiganiwa kwa kumwaga damu, yaani kulikuwepo na umwagaji damu....wacha kupotosha, wacha kujidhalilisha na kujishusha na kuwashusha waliomwaga damu zao/yao ati "Tulipewa"Najaribu kuwaza kwamba Zanzibar Iliungana na Tanzania Kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au Zanzibar Iliungana na Tanganyika Kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama Iliungana na Tanganyika na Zanzibar inasaini mkataba na Tanzania basi na Tanganyika inaweza kusaini mkataba na Tanzania.
Labda kama waingereza waliipata Uhuru Tanzania halafu hiyo Tanzania ikaungana na Zanzibar ila kama walipata Uhuru Tanganyika basi inabaki iliyopewa Uhuru ni Tanganyika sio Tanzania.
Muungano wetu unamambo ambayo bado ni magumu yanahitaji utatuzi au kuurekebisha muundo na Mimi napendekeza tubaki na serikali moja ili tuwe wamoja zaidi lasihivyo tutabaki na umoja wa makaratasi ila nafsi hazina umoja.
Wewe vipi? Yaani hujui hilo baraza la wawakillishi jinsi lilivopatikana au wewe ni mgeni? Huu mfumo uliopo wa Muungano ndio unaoiweka CCM madarakani Zanzibar au wewe hufahamu hilo baraza ni moja katika chombo kinachotumika kuulinda huu mfumo uliopo wa MuunganoNa kwa bahati mbaya ni kwamba majority hain ufikiri mzuri kuliko minority.
Kwa mfano , wangetumia BLW kama walivyotumia kuvunja katiba mwaka 2010
Wazuie Wabunge wao wasije Dodoma. Waondoe wafanyakazi wao katika JMT , wawaambie wenzao walioko bara warudi Zanzibar. Muungano utakuwa umefikia tamati kama wanavyotaka.
Sasa akina Duni wapo bara wakieneza sera za ACT kuhusu tume huru. Hutawasikia wakisema mamlaka kamili.
Hayo ya mamlaka kamili utasikia wakisema kule pumbawe, demani, mchambawima, mfereji maringo na kojani.
Hawa wanahitaji kura ya maoni si tume huru ya uchaguzi. Waamue kama wanataka au la! ikiwa yes ni 3.
Hii habari ya kujibanza halafu watie saini makubaliano ya madini kati ya Tanzanite na magugu maji, ni upuuzi tu
Upuuzi wa kutaka kujenga uhalali wa kuhamisha mapato ya madini.
tukiwaambia ccm huu muungano haufai wanakuja juu. Tanzania inawekeanaje mkataba na zanzibar il hali ndani ya Tanzania kuna zanzibar?Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya wizara hizo mbili zilizopo katika upande wa Muungano ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari, 2023 jijini Arusha ya kushirikiana kwa lengo la kufanya madini yaliyopo katika maeneo husika yaweza kuleta manufaa kwa pande zote mbili.
Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo ya Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam Dkt. Biteko amewataka watendaji wa wizara hizo kusimamia utekelezaji wa makubaliano
“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalitupa dira mpya katika kuendeleza mashirikiano yetu, hivyo tulichosaini leo sio kwa ajili ya kupiga picha bali ni kwa ajili ya kazi tuliyojipatia, natamani kuona mambo tuliyosaini hapa yanakuwa mfano na yanafanyika kwa weledi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili,” amesema Dkt. Biteko
Aidha, Dkt. Biteko amewataka watendaji wakuu wa pande zote mbili kusimamia masuala hayo ili yaweza kutokea huku akitaka kuanza kusimamia masuala ambayo hayahitaji rasilimali fedha kubwa ikiwemo kufanya tafiti hivyo yale yanayowezeka yaanziwe kufanyiwa kazi leo na sio kungoja.
Pia, amewataka Makatibu Wakuu wa pande zote mbili kutengeneza timu ndogo ya kusimamia makubaliano hayo ili kuhakikisha ushirikiano huo unadumu na kuwa wa mafanikio katika pande hizo mbili.
Naye, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaibu Hassan amesema utiaji wa saini wa makubaliano hayo usiishie kwenye makaratasi bali ufanisi na utendaji unaotakiwa kuonekana ukaonekane.
“Kitendo kinachofanyika leo ni kitendo muhimu sana kwa kwa pande zote mbili ambapo viongozi wetu wa juu wamekuwa wakitusisitiza kuendeleza mashirikiano ambapo tunategemea kushirikiana hasa katika suala la utaalamu hususan katika kufanya tafiti kwa pamoja,” amesema Hassan.
Pia, Hassan amesema ushirikiano huo utazaa toka kwa pande zote mbili za muungano na kuwataka watendaji wa wizara yake kufanya kile kinachowezekana kunyika leo na wasingoje kesho.
Jumla ya Hati Tano za Makubaliano zimesaniwa kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara ambazo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Mafuta, Madini na Gesi Asilia, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Kituo cha Jemolojia na Tanzania (TGC)
Mafuta, Gesi ni Nishati iko Wizara tofautiMafuta sio madini ?....maana huitwa dhahabu nyeusi....yakipatikana huko Zenji huenda yakajumuishwa kwenye hayo makubaliano ?
Nguruvi3 Kalamu Pascal Mayalla zitto junior
Kama huelewi ndio nini rudi kwenye makubaliano ya muungano ndio utaelewa.Tanzania na Zanzibar?
Wameshajua bara hatuna akiliTunaburuzwa haswa awamu hii.