Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Mwigulu ni mwiziiiiiii anayemiliki machine za kubet,anayemiliki bus za esta,anayemiliki singida united
 
Nchi mmeiharibu kwa mikono yenu
Ni muda muafaka mtafakari tutatokaje hapa, na tutaendaje mbele

Mkunbuke Kuna watu mil 60 wako nyuma wahahitaji kula, kutibiwa kulindwa nk.

Kwenye vikao vyenu Mmshauri mama yenu akubali kuahirisha uchaguzi tupate katiba mpya.

Kubalini tuanze upya kama nchi huku mtaani Kuna vichwa siyo ccm na haviko serikalini vitasaidia akili ya kutukwamu tuvitumie

Acheni ubinafsi wa kichama mambo ya siyo mwenzetu yakome hii nchi yetu sote, watu wazuri wapo lakini mfumo unawakataa, kubalini tu ambao hawajaiba imetoka hiyo

Dili la mwisho kabla ya kuanza upya
liwe la sukari na bandari inatosha

Katiba mpya iondoe monopoly ya kisiasa, kiuchumi, ajira na nk.

Katiba mpya itupe mgombea binafsi
Haya mavyama Yana shida zake

Ushauri Wetu wazalendo unaweza uchukua au uacha lakini huko mbeleni utatukumbuka mambo yakiwa magumu.
Hata Nyerere aliuliza mgombea binafsi anaogopwa kwa nini?
Nadhani ni ugumu wa kumdhibiti kupitia Msajili na vyama. Vyama vipo zaidi kwa ajili ya kutekeleza ajenda za watawala.
 
Nyie ndio watoto wa juzi na mmeharibu sana JF hii. Awali JF ilikuwa uwanja mpana sana wa majadiliano bila woga na kuheshimiana na karibu Mawaziri wote senior walikuwa humu, wanasiana wote mashuhuri na watendaji wa taasisi zote uzijuazo na taasisi zenyewe zikawa na page zake.
Lakini vijana wa kitanzania wa hovyo mkaingia humu na matusi na kejeli hivyo jukwaa likadharaulika.
Kulikuwa kukishushwa nondo zilizoshiba za kina DR Slaa na ma profesa kadhaa hadi unasahau kazi ili usome hoja.
Sasa wamejaa kina Lucas Mwashambwa & company JF imekuwa kikundi cha kwaya ya mapambio na kuabudu utadhani watu tumekatwa vichwa!
Poppy Hatonn leo anaitwa mtoto wa juzi ama kweli JF uwanja wa fujo
 
Waziri wa fedha tuambie zile gharama mlizotumia kuwapeleka Bongo movie kule Korea zingetosha kujenga zahanati ngapi pale Kakonko na Kazuramimba?
 
Punguzeni magari kwenye misafara yenu, mnatuumiza.

Swala la ajira kwa vijana litawagharimu sana kama Kenya, muulizeni JK aliwezaje kuajiri kila mwaka, nyie mnafeli wapi?

Na mbona hakuna mradi mpya wa maana mnaoanzisha? Mnatembelea alipopita mwendazake, hamna vision au hamna hela?

Mwisho,mbona tukiwaombea dua mbaya kwa mnavyotutesa haziwashiki ndio kwanza mnazidi kupeta,mnafanyafanyaje
Aaahhaaa
 
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW).

Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa, Malipo yameendelea kulipwa kwenye Sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa Fedha. Puuzeni ni wale wale wenye kututakia mabaya.

Acha hizo mkuu.
TANROADS choka mbaya, hawana hela!
 
Mchemba madelu,, Habari ya Dodoma Bwana! Nitakuja siku moja tupate chai na karanga! Ila mdogo wangu kuhusu mengine sijui Ila Yepi markez ni kweli watu wanadai sana na kuna mgogoro unatakiwa kutatuliwa haraka!

Suala la pili kuna mambo ya makato mtu anapohamisha Pesa inakatwa kwa Siri bila kujuzwa, Mfano mtu anayetuma sh 180,000 toka Vodacom Mpesa Kwenda BENK wanakata 2,000 Kama fee Ila pia kule BENK inafika pungufu ya sh elfu 1 Tena
Yaan unatuma 180,000 kamili Ila inapokelewa 179,000 nje ya makato ya kutuma

Tatu kuhusu kwenye Luku na kodi ya Pango na kwenye Vocha mbona mnatupiga? Vocha ya 500 imepandishwa Bei kuwa 600 Lakin value ya muda wa maongezi haijaongezeka, kwenye luku wanakata 1500 kila inapowekwa!

Suala la Mwisho nikupongeze kwa kuwa uwa unakanusha tuhuma bila vitisho kwamba askari akamate waliozusha, pili uwa una engage sana kwenye majadiliano bila jazba,

Britanicca
 
That's very true mkuu. Huyu waziri kwa maelezo yake tunamtofautisha vipi na jamaa wa TanzaniaLeaks? Unapinga uongo kwa kutuletea porojo tena msomi wa PhD, unataka tukuelewe vipi?
Anataka tumuamini kwa porojo ni aheri angekaa kimya kabisa, huu hauwezi kuwa utetezi.
 
Mheshimiwa heshima kwako asee mtu wangu wa nguvu. Nachokuomba mwanangu mtu wangu wa nguvu usinisahau 2030 kuendelea kwenye ufalme wako hata ubalozi ama UDC.

Mungu akulinde kwenye majukumu yako. Mfikishie mama salamu zangu za dhati muambie tupo pamoja hadi 2030.
Kalime viazi upate hela huyo unaempigia chapua ikulu ataisikia tu kama wewe unavyoisikia atakwenda kusalimia tu lakini hana hata chembe ya presidential material, ni huyo huyo alituambia tuhamie burundi na ni huyo huyo aliyemshukuru magufuli baada ya kupona ajali, hivyo ukae ukijua ikulu atakwenda kunywa chai au asubiri rais wa US akija hapo ikulu atapata mwaliko
 
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW).

Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa, Malipo yameendelea kulipwa kwenye Sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa Fedha. Puuzeni ni wale wale wenye kututakia mabaya.

Sawa mkuu
 
Unalalamika tozo wakati hata tin namba huijui, punguza ulevi mkuu
Punguza uchawa, aliyekwambia tozo zinawapata wenye tin peke yao nani??
Hiyo simu unayotumia kupokea miamala ya buku 7 ya mapambio haina makato??

Halafu mwenzio hizo tin ninazo kama tano
 
Punguza uchawa, aliyekwambia tozo zinawapata wenye tin peke yao nani??
Hiyo simu unayotumia kupokea miamala ya buku 7 ya mapambio haina makato??

Halafu mwenzio hizo tin ninazo kama tano
Kwahyo bila tozo hzo ruzuku wanazopata ufipa zitatoka wapi au wakzipokea wanazirudisha Tena hazina kuu? Nawalivyo walafi wa hela🤣🤣
 
Kwahyo bila tozo hzo ruzuku wanazopata ufipa zitatoka wapi au wakzipokea wanazirudisha Tena hazina kuu? Nawalivyo walafi wa hela🤣🤣
Umeona ulivyo na mihemko??
Mimi naongelea habari za wananchi ww unaingiza habari za vyama.!! Punguza uchawa basi.
 
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW).

Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa, Malipo yameendelea kulipwa kwenye Sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa Fedha. Puuzeni ni wale wale wenye kututakia mabaya.

Wooow, Leo umekuja jukwaani..welcome. kiti kimekuwa Cha moto huko jikoni...pambanaa
 
Back
Top Bottom