Tanzanialeaks apuuzwe, Hazina haijafilisika

Tozo na kodi ndio vinaendesha nchi.hata Ulaya wanalipa sana kodi na tozo kwa maendeleo yao.
Nadhani hata hati ya kusafiria huna achilia mbali ulaya unayoisikia kwenye redio kijijini kwenu.

Unajua kodi zinavyosimamiwa ulaya na sheria kali zilizopo kwenye kubana matumizi yasiyo na tija kama tulivyoona jana msafara wa magari 150 + pesa hizo kodi ambazo zingeweza kutatua matatizo ya Rukwa badala ya kutumiwa kwa anasa za misafara isiyo na tija

Angalia hapo Ulaya wanavyobana matumizi viongozi wa Africa walipokuja walitupiwa kwenye minibus na huko ndio mnakopa sasa.

Sasa mkopeshaji minibus moja mkopaji magari 150+

Lini mara ya mwisho Tanzania mtu kafikishwa mahakamani kwa ubadhirifu wa kodi , wale wanaotajwa na CAG pia ni utani kama wa Nape na Ndumbaro?
 
Nimekua chawa mwaka wa kumi huu mkuu....
Mwigulu Nchemba oyeeeeee.....🤣
 
Inawezekana nchi haijafilisika kwa sababu ya kukopa ovyo. Jiulize wakati Magufuli anaondoka madarakani deni la taifa lilikuwa shilingi ngapi na wakati anaingia Samia chini ya uwaziri wa Mwigulu nchi imeishakopa kiasi gani.

Na cha ajabu zaidi sehemu kubwa ya keki ya taifa inatafunwa na wanasiasa wanaojilipa mabilioni ya shilingi ka kutafuna fedha za umma kama mchwa huku wananchi wengi wakizidi kutopea kwenye umasikini na kuishi maisha yanayosikitisha sana. Mungu anawaona na atawalipa kwa kadri ya uovu wenu.
 
Tatizo huwa hauaminiki wewe, wiki si nyingi zijazo tutamsikia rais akiongea kitu tofauti kabisa na hiki ulichoandika hapa.
 
Jibu hoja zote umejibu mbili tu na hiyo ya pili umeficha, kama Kampuni YAPI walikuwa na changamoto gani hizo ? Kwanini serikali ikubali kurudishwa nyuma na changamoto za ndani ya kampuni si muwafukuze kama hawalipi wafanyakazi wao maana inakwamisha shughuli
 
Hakuna nchi yenye watawala wa ovyo hapa Ulimwenguni kama Tanzania. Hii nchi bora tu mkoloni arudi kuitawala.
 
Mafao Kwa viongozi wastaafu Rais, makamu wa Rais, mawaziri wakuu, majaji, na mafao ya wapenzi wao yapunguzwe au yaondolewe Kwa kiasi kikubwa
 
Mwigulu ume panic, hao Tanzania Leaks mimi siwapuuzi kwasababu nikiunganisha dots zangu napata majibu hii serikali yenu inapumulia mashine.

Unaleta thread halafu unakimbia kuogopa maswali, kama unajiona uko busy usiwe unaleta thread JF kujisafisha kiuoga, kama unajiamini uko vizuri leta uzi usimame kuutetea uzi wako.

Huchezi na watoto hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…