Tumepokea kwa mshtuko juu ya kifo cha mcheza filamu nchini Stev Kanumba. Suala la kifo si geni kwani kila nafsi itaonja mauti. Jambo hapa la kujifunza, je Stev ameonja mauti kwa mazingira gani?. Ndugu vijana wenzangu, nimeshuhudia mara nyingi hususani hapa Tz mtu akiishakuwa maarufu hujisahau kidogo. Kashfa za mapenzi na starehe luluki humwandama. Ajali za magari huwakumba mara nyingi tena usk wanapotoka katika burudani zao. Sikatazi kutoka outing jamani...La hasha. Nilishawahi mshuhudia star mmoja amelewa kupindukia wanambeba kumpeleka kwenye gari lake. Walipomuacha tu akaliwasha na kuondoka!. Complex, Dandu ni miongoni mwao walioaga dunia kwa ajali ya magari. Walionusurika ni karibu wote. Sasa twende katika visa vya mapenzi, kuna mmojawao alishachomwa kisu na kufariki hapohapo (jina nimesahau). Kupigana na wapenzi wao imeishakuwa fasheni. Biff za kipuuzi kabisa huendekezwa. Dhuluma, utapeli, lugha chafu, uzinzi na anasa ndio nguzo zao kuu. Mliona ya T.I.D kusweka jela, KAJALA naye anamfwata. WEMA mahabusu ndio kwao. Nia yangu hapa ndugu zangu vijana ni kuwashauri tuwe makini pindi unapokuwa maarufu. Yawezekana mauti yaliyompata ndugu yetu ni bahati mbaya na kama kawaida yetu "mapenzi ya mungu" ila iwe fundisho kwetu.