Kifo cha Kanumba kimenishtua sana, ilifikia mahali nakashindwa kunywa chai asubuhi. Hata sasa siamini kama kweli huyu gwiji wa sanaa ya filamu ametutoka.
Siyo kwamba ninamfahamu sana Kanumba, personally sijawahi kukutana naye uso kwa uso.
Nimemjua Kanumba kupitia kwenye filamu alizowahi kuigiza.
In general kama jamii ya kiafrica nimejifunza mambo mengi kuhusu maisha na kimaadili kupitia filamu zake. Yapo mengi ya kuigwa kutoka kwenye filamu zake.
Sipendi kuzungumzia maisha yake nje ya filamu kwakuwa sijui, na hata kama ningejua ningefananisha kama maisha ya watumishi wa mungu, ambao siku zote wanafundisha habari za wokovu kupitia maandiko ya biblia, lakini maisha yao nje ya kanisa hayaendani na jinsi wanavyofundisha.
Kanumba amesaidia sana kuibua changamoto nyingi za maisha ya kitanzania kupitia filamu, kwa mfano nakumbuka fulamu moja aliyowahi kuigiza iliyokuwa inazungumzia mfumo dume ambayo aliigiza na akina wema sepetu, ilisaidia jamii kujua kuwa mtoto hupatikana kwa mapenzi ya mungu na si vinginevyo.
Pia kuna filamu aliigiza yeye na familia yake kuwa wachawi na wanaishi kwa kunywa damu za watu, lakini baadaye kupitia hiyo filamu ikaonekana kuwa Mungu ni Mkuu, hakuna aliyejuu yake.
Hivyo nadhiriki kusema kwa jinsi nilivyoshtuka, nisingeshtuka ningesikia kuwa Muikulu ndiyo katutoka.
Samahani kama nimewaudhi, ni mtazamo zamo mc usivunje majungu!