Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Unapojua wajibu wako hapa Duniani unapaswa kujiandaa na safari hii ndefu zaidi kuliko safari yoyote!
Namuomba M/mungu anipe mwisho mwema.
 
We Gamba hujamsikia Mnyika alifika huko toka mapema toka asb akiwa mbunge wake!!
 
Ivi hili ni jukwaa la nin vile..mods mpo wap

Mods wamealikwa kula Zanzibar kwenye shughuli ya "Karume". Wanarudi na boti ya jioni kwahiyo post mbofumbofu watazimuvuzisha usiku
 
Ndio nani huyo jamani?





Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi, na kisha kujiunga na sekondari ya Mwadui mkoani Shinyanga na baadaye alihamia Dar Christian Seminary.
Aliendelea na masomo ya kitado cha tano na sita katika shule sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam.
KUANZA KWA SHUGHULI ZA SANAA
Akiwa katika Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa ndani ya Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.


Baada ya kupata uzoefu wa kutosha na kundi la Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake ya filamu ambayo alikuwa anaiongoza mpaka umauti unamkuta. Umahiri wa uingizaji wake ulimfanya afahamike kila pembe ya bara la Afrika.


WASANII WA KIMATAIFA ALIOSHIRIKIANA NAO
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria. Mbali na hao marehemu pia alibahatika kucheza filamu na mastaa wengine kadhaa kutoka nchini Nigeria.
Miongoni mwa filamu alizocheza Kanumba na kumpa umaarufu ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na nyingine nyingi.


SIASA KIDOGO
Kanumba alikuwa anajihusisha na mambo ya siasa chini kwa chini na hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

 
Mwanaume unazimia msibani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! hii kweli ni ajabu

Mwanaume lazima uwe strong until your death
 
Mbunge wa Ubungo, alishapita kwenye msiba mapema leo asubuhi kabla ya kuelekea kwenye maandalizi ya mkutano wake wa hadhara!
 
Haaaa, stop being judgemental.
Unaposema mnafiki sema na sababu zinazokufanya useme hivyo....its not fair to the dead!!

imani bila matendo hakuna kitu,huyu ni kama Prezoo. Wanadini binafsi,nadhani umenielewa
 
Back
Top Bottom