Tanzanian traditional local foods

Loshoro, Kitalolo, Makukura, gongo na buzaa kwa upande wa Wamasai sijaona picha.

Kiburu, kitawa na kimantine kwa Wachagga nazo sijaona.

Yote kwa yote vyakula vya asili ni vizuri na vina afya.
Chagga nation[emoji23]kiburu a.k.a kiumbo, mtori, loshoro, ngararimu, ndizi za kuchoma na mbege
 
[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]
 
Tumeona vindege, mishkaki ya panya ila sijaona wale ndg zetu Wahehe na ile nyama yao ya asili.
 
Hakika hii nchi ina vyakula vingi vya asili, hivyo vindege ni biashara na watu wa Kondoa wanazipenda sana.. Ila ugali mweusi sijapata kula wala kushuhudia.
Vyakula vya asili ni vingi na vingine havijawahi kuappear kokote pale kwenye picha au maandishi hivyo ni rahisi kizazi kijacho kikakosha kujua au kupata kumbukumbu ya vyakula vyetu vya jadi, mfano ni chakula maarufu cha wakurya almaarufu KIMORO au kipande cha nyama ya mnyama pori kama nyumbu au swala kilichokaushwa juani hiki ukipikiwa na ugali pamoja na mlenda utamu wake pilau au nyama ya kuku unaiweka kando.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…