KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,893
- 3,145
Ugali wa muhogo usiokuwa mweupe kabisa(Nyange/Makopa),utokana na njia moja ya kutengenezwa.Umekuwa mtu wa kwanza kwenye uzi huu kuutambua ugali huu, tafadhali tuelezee kama unafahamu maandalizi yake mpaka kupelekea muhogo huo kuwa na rangi hiyo, pia unaweza kututanabaisha ugali huu ni maarufu kwa wenyeji wa mkoa gani.
Kwanza ni aina ya muhogo wenyewe,mara nyingi muhogo unaotengezwa unga huwa ni muhogo mchungu usioweza kuchemshwa na kuliwa ukitolewa tu shambani.
Ugali huu wa muhogo wenye rangi za weusi,utengenezwa kwa njia ya KUVUNDIKA.
Muhogo utolewa shambani na kumenywa na kisha kuwekwa juani kwa siku kadhaa kulingana na uhitaji wa rangi.
Muhogo ukaa juani kati ya siku 2 hadi 5 kutegemea mapenzi ya mtumiaji na kiwango cha jua.
Ili muhogo uwe mweusi sana utaanikwa kwa siku 2 au 3 tu.
Kisha uandaliwa sehemu ya kuvundikia kwa kutumia majani ya mzima au mgomba kwa kutandazwa chini kwa urefu usiopungua nchi 3 toka chini,kisha unyunyiziwa maji hayo majani na kupangwa muhogo juu yake,kisha unyunyiziwa maji huo muhogo uliopangwa na kisha unafunikwa na majani juu na pembeni kiasi cha kuweza kutengeneza joto kali,na unyunyiziwa maji tena juu ya hayo majani funikia.Baada ya hapo usubiriwa kwa siku 5 hadi 7 ndiyo unakuwa tayari.Utolewa na kuanikwa juani mpaka unakauka kabisa na unakuwa tayari kwa kuhifadhiwa,kuchemshwa kama kitafunwa au kusagwa kuwa unga.
Mikoa wanaofanya hivi ni Tabora,Shinyanga,Mwanza na Mara.