Tanzanian traditional local foods

Tanzanian traditional local foods

Duh! Kumbe kuna mikoa ina utajiri wa maarifa katika uhifadhi salama na asili wa chakula na hatufahamu chochote kile kuihusu, umenifumbua macho kuanza kuifuatilia mikoa hii hususani Tabora kujifunza kitu katika tamaduni na njia bora za uhifadhi vyakula kwa kipindi kirefu pasina gharama kubwa kitu ambacho ni muhimu kwa taifa katika nyakati mbaya au za dharura kujihakikishia utoshelevu na usalama wa vyakula, siyo tu wananchi kuitegemea serikali kwa kila kitu linapokuja suala la akiba ya chakula katika nyakati ngumu yenyewe tu ndiyo iwatunzie kisha iwagawie bali hata wao kuwa na maarifa muhimu kama haya yakuweza kuwavusha ni msaada mkubwa kwa nchi na kipimo tosha kwa jamii iliyostaarabika ya kiafrika.
Hakika wazee wetu walitufunza njia hizi na zingine mbali japo vizazi vya sasa udharau ujuzi huo.Na kadri siku zinavyo kwenda ndiyo maarifa haya ysnapotea.
 
Asante sana mkuu, sijui nikushukuru vipi kwa darasa lako maridhawa maana masomo kama haya hatuyapati shuleni bali ni maarifa tunayoyaishi na kuyaacha yaishilie zake pasipo kunukuliwa mahali popote pale kwa vizazi vijavyo, mwisho wa siku sayansi hii ya asili ya uandaaji vyakula ya kiafrika kabisa ambayo ni niyakuvutia na yenye kuakisi uasilia wetu tunaipoteza na kuifukia kabisa, kizazi kijacho kitaishia kutusoma kama mababu ambao hawakuwaachia urithi wowote vizazi vyao kuhusu asili na tamaduni zao, licha ya kwamba walikuwa wasomi na siyo kama kizazi cha enzi za ukoloni.
Asante kwako pia mkuu kwa uzi huu.
 
Hakika wazee wetu walitufunza njia hizi na zingine mbali japo vizazi vya sasa udharau ujuzi huo.Na kadri siku zinavyo kwenda ndiyo maarifa haya ysnapotea.

Kweli mkuu, ni vyema tukapambana kuhifadhi urithi huu adhimu kwa ajili ya kizazi kijacho huwezi jua ikiwa nyuzi kama hizi zitakuja kuwafikia walengwa nyakati hizo siye hatupo.
 
wadau wakuwe wanafanya festival kubwa ya vyakula vya asili kila kwota ya mwaka.
Ikibidi paongezwe na mbinu za asili za kujamiiana.
Kuna wanawake watakufa bila kupigwa katerero hivi hivi jaman! Hebu fikiria ufe hujawai kufika climax wala kusquirt!
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    39.1 KB · Views: 9
wadau wakuwe wanafanya festival kubwa ya vyakula vya asili kila kwota ya mwaka.
Ikibidi paongezwe na mbinu za asili za kujamiiana.
Kuna wanawake watakufa bila kupigwa katerero hivi hivi jaman! Hebu fikiria ufe hujawai kufika climax wala kusquirt!
[emoji23][emoji23][emoji23]eti Katerero[emoji125][emoji125][emoji125][emoji1787]
 
wadau wakuwe wanafanya festival kubwa ya vyakula vya asili kila kwota ya mwaka.
Ikibidi paongezwe na mbinu za asili za kujamiiana.
Kuna wanawake watakufa bila kupigwa katerero hivi hivi jaman! Hebu fikiria ufe hujawai kufika climax wala kusquirt!
Nakuunga mkono kwenye hilo wazo la kuanzisha festival ya vyakula vya asili na tamaduni zetu ikiwemo ngoma, unyago, mila, desturi,mahusiano, n.k walahu kwa kila ukanda katika kipindi fulani cha mwaka na pia tutumie vyema mwanya wa maadhimisho ya utalii na Nanenane kuonyesha na kuvitangaza vyakula vyetu vya asili na tamaduni zetu.
 
Dunia ya leo watu wengi ufanya utalii wa ndani au wa nje ya nchi zao si kwa ajili ya vivutio vya asili vya mazingira na majengo tu bali kwa ajili ya kufurahia utalii wa vyakula vya asili na tamaduni za jamii mbalimbali.

Kama watanzania ni fursa kwetu pia kutangaza na kujivunia vyakula vyetu vya asili na vya kitamaduni, kwani Tanzania tumejaaliwa sana kuwa na vyakula vingi vya asili na vyenye ladha nzuri pengine kuliko nchi yeyote ile barani Afrika, ningeomba kupitia uzi huu yeyote yule mwenye picha nzuri ya chakula cha asili cha kitanzania na jina la chakula chenyewe iwe ni kiswahili au kikabila asisite kutupia hapa hili tusaidiane katika kuutangaza utamaduni wetu.
Siasa mpaka kwenye mapishi!
 
Siasa mpaka kwenye mapishi!
Mapishi ni sanaa inayopaswa kupewa nafasi ya kutambuliwa kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha afya zetu na kutupatia sababu moja wapo ya kuishi.

Tunaposema tujivunie tamaduni zetu kama watanzania ni pamoja na vyakula vyetu vya asili, hivyo hapa hatuzungumzi SIASA hapa tunaongelea utanzania na urithi wetu utakaofanya watanzania wathamini vya kwao zaidi na wasio watanzania wavutiwe kuzuru kwetu kwa nia ya kujionea na kufurahia pamoja nasi.
FB_IMG_16918584558006057.jpg
 
Back
Top Bottom