Asante sana mkuu, sijui nikushukuru vipi kwa darasa lako maridhawa maana masomo kama haya hatuyapati shuleni bali ni maarifa tunayoyaishi na kuyaacha yaishilie zake pasipo kunukuliwa mahali popote pale kwa vizazi vijavyo, mwisho wa siku sayansi hii ya asili ya uandaaji vyakula ya kiafrika kabisa ambayo ni niyakuvutia na yenye kuakisi uasilia wetu tunaipoteza na kuifukia kabisa, kizazi kijacho kitaishia kutusoma kama mababu ambao hawakuwaachia urithi wowote vizazi vyao kuhusu asili na tamaduni zao, licha ya kwamba walikuwa wasomi na siyo kama kizazi cha enzi za ukoloni.