Unaongea kinyume bwana mdogo. Wakenya ndio mnajipendekeza kwa Tanzania na kufuatilia mambo ya Tanzania. Angalia magazeti yenu yanavyoandika kuhusu Magufuli kila siku, hakuna gazeti likaandika mambo ya Uhuru Tanzania. Jambo lolote akisema Magufuli lazima magazeti yenu yaandike.
Ukienda mitandaoni, Wakenya wengi wanachangia maoni kwenye youtube channels za Tanzania kuliko Watanzania wenyewe. Angalia video za nyimbo za Tanzania youtube lazima utakuta register ya +254, huwezi kukuta Watanzania wanachangia kwenye youtube channels zenu wala video za nyimbo zenu.