Tanzania's China-backed $10bn port plan stalls

Tanzania's China-backed $10bn port plan stalls

Kwa nini waliokuwa wanaendeleza mazungumzo na kukubaliana na mapendekezo ya Wachina majina yao yasiwekwe wazi?. Hao ni watu wa hovyo kweli kweli. Awamu zilizopita walikuwa wanasema eti mikataba ni siri kama ni siri wanaolipa deni ni wananchi na kwa nini wasifahamu mikataba inasemaje?.
 
Acha ubishi,kurekebishwa au kuvunja inategemea vipengele vilivyo kwenye mkataba vinasemaje ?kama ujauona mkataba kaa kmya.Mikataba ya Tanzania naijua wewe hakuna mtu anayesoma .Hapa nilipo ninamikataba nime signisha na halimashauri Zaidi ya 50 na ukimwuliza mtu kwenye halmashauri inasemaje hata mwanasheria wao hajui na una vipengele Zaidi ya 100 am telling you na kuna mali yeye hawezi kuvunja mkataba every thing nadectate mimi ndio ushangae sasa

Eeehee, unaona sasa unavyojitia ujuaji?

Kama umekalia mikataba hapo, hiyo mibovu ulikuwa unafanya nini. Mbona hata siku moja hujasikika ukipaza sauti yoyote?
Wewe ni kati ya wale niliowazungumzia hapo juu. Mnapiga pande zote zote. Sasa unashabikia, huko nyuma ulikuwa mpigaji wa hiyo mikataba mibovu.

Huwezi kusema wewe pekee yako ndiye unayejua kusoma hiyo mikataba. Utamzidi Mzee 'Visenti' wewe? Au hata humjui?

Si unaona sasa hivi hiyo ya akina Acacia inavyofanywa, au hujui kunatokea nini?
 
Nyiye ndiyo uwa mnaingiza mkenge serikali kwa kutokusoma, narudi kama veteran lawyer, unaweza vunja mkataba wowote kama ikigundulika sehemu ya pili haijatendewa haki, kama rushwa imetuka, insane, masilahi siyo sawa. Kama Ridhwani kikwete alikamatwa uko China, hiyo mikataba ndo ikawa suruhu yake kukatwa shingo kwa expense ya watanzania. Hiyo mikataba inaweza futwa.
Anazungumzia mikataba ya "Halmashauri" na anaifanya ionekane hata hiyo hakuna njia ya kuivunja au kuirekebisha kwa vile anaogopa kushitakiwa! Can you imagine?

Halmashauri 50, yeye pekee ameshikilia mikataba yao iliyosainiwa kimakosa? Tuna watumishi kweli ama huu ni mzaha wa aina yake?
 
Futa uone, kilengele kitakutaka ulipe kitu kikubwa au pesa Kiasi kwamba na idi upoe
 
Anazungumzia mikataba ya "Halmashauri" na anaifanya ionekane hata hiyo hakuna njia ya kuivunja au kuirekebisha kwa vile anaogopa kushitakiwa! Can you imagine?

Halmashauri 50, yeye pekee ameshikilia mikataba yao iliyosainiwa kimakosa? Tuna watumishi kweli ama huu ni mzaha wa aina yake?
Usipanick mjini hapa. Tunalipa kodi
 
Shida ilishasainiwa, Sasa implementation itafanyika tu SiSiM ilishatuingiza chaka. Mkataba ni mkataba ukishawekwa sahihi. Watasubiri Magufuli atoke madarakani au watakwenda mahakamani hapo ndio panaogopesha anyway big up awamu hii
Haukusainiwa soma uzi uelewe
 
time will tell
Ajizi ni nyumba ya njaa
Utawala wa awamu hii ni rahisi sana kucriticize miradi iliyowekwa na tawala zilizopita lakini hauna ubavu wa kuvutia nchini miradi yoyote ya maana

Kwa mawazo haya mkuu ukibahatika kupata uongozi wa nchi yetu utaradusha ukoloni kwa mgongo wa uwekezaji. Kweli ujanja ni kuona mbali.
 
Eenh Hee, hilo li-Mkataba si nachana tu hilo likaratasi? Nenda kashitaki unakopenda, utajenga hiyo biashara yako utaipitisha wapi hadi ifike au itoke bandarini kwako?
Baadhi ya wanaopinga mradi huu walikuwa katika Baraza LA Mawaziri mnamo mwaka 2013 mradi huu uliposainiwa. Hatukusikia sauti zao. Huu ni ukigeugeu
 
Kama anavyosema Upopo, ni wazi kuwa viongozi wetu na wanasheria wao hawasomi mikataba na ndiyo maana tumesaini mingi inayouza nchi. Mze Vijisenti alisoma mkataba wa gesi ya Mtwara? Mkataba wa kuuza NBC ulisomwa na kueleweka kabla ya kusainiwa? Mikataba ya madini iliyotupa mrahaba wa asilimia 3 ya faida ilisomwa na kueleweka?

Watu wanafanyiwa PowerPoint presentation na upande wa pili kama ilivyotokea kwa Spika Ndungai, na hiyo inatosha kushabikia mkataba? Ni ajabu na kweli!

Kama mikataba mikubwa mibovu ilisomwa kwa uangalifu basi walioshauri isainiwe bila shaka walipewa hongo na wakauza nchi, huku wakijidai ni wazalendo.

Tushukuru kwamba kipindi hiki tuna timu inoyosoma mikataba. Huyu Mwalimu Jiwe anavyosema anakuwa na mafaili kitandani labda ni kweli; anasoma na kuelewa.

Wachina wa leo sio wale wa kipindi cha Mao. Ni wanyonyaji kuliko hata mabepari ya Ulaya na Marekani. Si mmeona uwekezaji wao kiwandani Urafiki?

Uwekezaji wenye masharti mabaya ya kikoloni ni kuuza nchi. Ni sawa kabisa kukataa hata kama kuna makubaliano ya awali. Si lazima ukubali kifo eti kwa vile umeshaanza kuugua.
 
Baadhi ya wanaopinga mradi huu walikuwa katika Baraza LA Mawaziri mnamo mwaka 2013 mradi huu uliposainiwa. Hatukusikia sauti zao. Huu ni ukigeugeu
Huo ukigeugeu ndio janga kuu sana la taifa letu.
Wakati wakiwa ndani ya baraza hilo nadhani huwa wanakuwa kama wanafunzi, au hata wafungwa hivi. Hawana sauti!
 
Yet there are practical difficulties, not least that Bagamoyo’s port, unlike Dar es Salaam’s, would most likely need regular, extensive dredging.

LET US LEAVE THE BAGAMOYO PORT PROJECT ALONE. IT WILL MORTGAGE OUR ECONOMY AND OUR COUNTRY TO FOREIGN INTERESTS INDEFINITELY. IT IS NOT A LIFE OR DEATH PROJECT AND SMELLS OF GRAFT. WE SHOULD SCALE UP INVESTMENT IN TANGA PORT WHICH IS ALREADY FUNCTIONAL AND VIABLE. DEVELOP A STRATEGIC PLAN FOR TANGA AND INCORPORATE SOME OF THE REASONABLE ELEMENTS FROM THE BAGAMOYO PROJECT. WE CAN IMPLEMENT THE PROJECT IN PHASES DUE TO LIMITED RESOURCES. COMPARE THE TANGA OPTION AND THE BAGAMOYO OPTION. THE TANGA OPTION IS MUCH BETTER, MORE SO WITH THE OIL PIPELINE PROSPECTS. PLENTY OF LAND AND INVESTMENT OPPORTUNITIES. TANGA IS THE WAY TO GO !
 
Tumelishwa propaganda za Uzalendo

Huu mradi ni mzuri na una manufaa sana.

Sisi hatuingizi senti hata moja kwenye mradi bali hii ni investment ya moja kwa moja yaani tunaleta pesa nchini!, Siyo mkopo huu
Tunashindwa kuona the big picture, Trickle down benefits za mradi, ajira, kodi, kuongeza volume ya mzigo kwa ajili ya reli zetu ambapo kuna fee wasafishaji watatozwa, kuifanya TZ kuwa hub ya mzigo wa china kuingia ndani ya africa, yaani badala ya wafanyabiashara wa Africa kwenda China mzigo wataukuta hapo bagamoyo!, INA MAANA YOTE HAYA HATUYAONI TUMENG'ANG'ANIA BANDARI TU?

Hili dili likiporonyoka, Tutakuwa tumejibania sisi wenyewe, na gharama ya kuijenga hiyo bandari miaka 50 ijayo tutlipa gharama mara tano zaidi ya leo

Tunaacha kujenga bandari tunajenga airport Chato, kweli sisi wa ajabu sana
Mm mwenyewe nilijiuliza maswali mara mbilimbili hivi kweli serikali yetu imeshindwa kuona picha kubwa Na faida za mradi wakaamua kuupiga chini.

Mm naona mradi pamoja na design ya mkataba uliokuwepo ila bado wanufaika tungekuwa sisi zaidi.

Ule mradi ulikuwa unafungua gate la tanzania kuwa soko huria na nchi nyingi za africa zingekimbila hapa kuja kuchukua bidhaa.
 
Tuna bahati mbaya watu wanalishwa upepo wa Uzalendo, ila kiukweli hii ni fursa njema tumeiacha

Hebu angalia, sisi tunawapa muda waendeshe bandari waliyoijenga wao wenyewe kwa pesa yao wenyewe kwa miaka 40 LAKINI kuna Wapakistan ambao wamewapa Wachina bandari ya Gwador kwa miaka 100!- Hii ni kwa sababu Wapakistani wamegundua kuwa ishu siyo jengo linaloitwa bandari , ishu ni CHAIN NZIMA YA INPUT KWENYE UCHUMI itakayochangia kwenye uchumi
 
Back
Top Bottom