Tanzania's GDP: Hivi tunajua hili?

Tanzania's GDP: Hivi tunajua hili?

Hizi analysis nyingine!... Pengine ndio maana hatufiki.

Sasa wewe ndugu yangu unaona kuwa population ndogo au land area ndogo(tena Arable land) ni disadvantage!... Hii mbona ndivyo sivyo. Watu na Ardhi ni rasilimali nyeti sana kwenye maendeleo. Jinsi gani unaziendeleza na kuzitumia hizo rasilimali ndio tatizo letu, lakini huwezi kuziita ni disadvantages when it comes to maendeleo. Hata hao China, sasa hivi wamarekani wenyewe wanawatamania soko lao la ndani la 1.3billion. Sembuse sisi 40million.

Tuwe makini na utetezi wetu...

As far as GDP ranking is concerned,population ndogo ni advantageous
 
NINADHANI Watanzania wameshiba porojo, visingizio na sababu hii au ile ya kutoweza kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa.

Simply, kwa sababu hii ni nchi ya wababaishaji. Kila mtu anajifanya anajua. Na kwa sababu kila mtu anajua ni sawa na wote hatujui.

Nilipoanzisha mada hii nilidhania tutaichukulia kwa uzito wake. Hapa cha muhimu ni kujiuliza kwanini miaka karibu 50 baada ya uhuru nchi yetu iliyokuwa mkiani wakati wa uhuru hadi leo bado iko palepale mkoani.

Wanaobisha wanakumbuka India, Malaysia, South Korea, Japan yenyewe, Singapore, Mauritius, Botswana na kadhalika zilikuwa wapi. Na sasa ziko wapi.

Hii ina maana moja tu. Kwamba kuna kitu wanachokijua na walichokifanya ambacho sisi hatukijui na hatujakifanya. Ukichunguza viongozi wetu wengi wametoka kwenye umasikini mkubwa, iwe Nyerere mwenyewe, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na usiseme hao wa Zanzibar!!! Hawa kazi yao kwanza ilikuwa kujineemesha wenyewe, kisha familia zao na kisha ndugu, jamaa na marafiki zao. Sasa hatujui maana Kikwete sio masikini kiasi hicho kama na yeye atakwenda njia hiyo hiyo au atataka kwanza awatajirishe Watanzania kisha ndio ajifikirie yeye mwenyewe [kama atajitenga na wafadhili wake na maswahiba zake wakubwa walioichafua nchi kiasi ilichochafuka leo pamoja na kukwanya na Baba wa taifa kabla hajafariki!]. Hilo ni shauri lake. Akiachia na yeye zawadi ya Mo Ibrahim hata kwa Muumba hatakuwa na sababu ya kujietetea! Akumbuke Kurani takatifu inasema mke, mali na watoto [na marafiki-ongezo langu] ni MTIHANI mkubwa! Akipita huu tu kafaulu!

Turejee kwenye pointi, ili tuendelee ni lazima tufanye mambo haya:
. Kwanza tutambue kuwa kelele zetu za kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu hazijatusaidia kitu,
. ujenzi wa viwanda umetushinda,
. fedha na mitaji hatuna,
. njia rahisi ya kupata fedha na mtaji ni biashara na sisi tunailegezea, wakati wenzetu Dubai wanapaa,
. sekta nyingine ya kujilimbikizia ni huduma lakini serikali yenyewe legevu inaachia uchafu kila mahala na hakuna anayelalamika wala kujali. Tumeshazoea. Kampuni za usombaji taka ni chafu kuliko taka zenyewe!
Usiseme kuhusu bustani na maua-utadhani Ikulu imepiga marufuku tusiwe na bustani na maua majumbani kwetu, maofisini na hasa sisi waswahili-angalau wageni na mabenki yao wanajitahidi,
. tuna wizara kebekebe lakini zinakanyagana vidoleni na inaelekea mawaziri wakubwa kwa wadogo ukiwauliza wanalipwa mshahara kwa ajili gani watakuwa hawana majibu. Kinachotakiwa management by objectives, decentralization, delegation of authority na lean government. Hebu mmoja afanye analysis ya goverment expenditure compared to GDP utakuta seirkali yetu ina ratio kubwa kuliko hata serikali zenye uwezo! Kichaa tupu!
. mama lao ni kwamba hakuna wizara yenye vision yake yenyewe, mission yake na strategic objectives au malengo ni wapi wanakotaka kuipeleka nchi na watu wake kufikia muda fulani. Vipo? Ninaomba iwe huu ni uzushi wangu. Nambieni basi wizara zina vision, mission na strategic objective jamanai? Katika karne hii , miaka hii ikiwa tunakwenda sawasawa na kina Mzee Malecela, Kawawa,Waryuba, Msuya na kadhalika tumekwisha!

. Kubwa na baya zaidi ni kule watu wa CCM kujiona wao ndio wana akili kuliko Watanzania wote [siku hizi ninasikia tuko milioni 40 latest UN figure-2007] tukiwekwa pamoja. Hakuna njia ya mkato ya kuikwamisha nchi kimaendeleo kama ubaguzi wa kivyama. Yaani chama kimoja kubagua vyama vingine na watu wake na kuwapa hata wababaishaji na wajinga nafasi ya uongozi ingawa wanajua fika hao ni wajinga na kazi hiyo hawataiwezea. Mfano mzuri ni Zanzibar na hali iliyofikia sasa.

Zanzibar yenye watu milioni 1 tu ina kila sababu ya kuwa na GDP per capita ya dola za Kimarekani tena 5,000 hadi 10,000. Lakini wameishia kuwa na gomvi za kuku na bata huku wakigharamia ng'ombe na ngamia eti kwa kuwa huyu ni CUF hafai, sasa wanakufa na vikoi vyao kiunoni na hakuna chochote kilichoviringishwa kwenye kunjo lake!

KUJENGA UCHUMI pamoja na hayo yote pia kwahitaji kwanza kutoa elimu ya:
-UCHUMI
-MENEJIMENTI
-BIASHARA
-UHASIBU
-RASILIMALI WATU

kwa lugha ya Kiswahili. Pungufu ya hapo mwaka 2010 nchi duniani zitaongezeka na kufikia 250 na nina hakika Tanzania itakuwa ya 249! Poleni wanangu na wajukuu wangu! Mbona mnalo!

Mkuu naona umeongea mambo mengi ya maana sana, ila ni ukweli uliyo wazi kuwa watanzania tunaendekeza siasa kwenye kila jambo na hatuko serious na mambo yetu mengi.

Tuanze na suala la viwanda, kumbukumbu zangu zinanikumbusha kuwa wakati wa aamu ya kwanza tulikuwa na viwanda vingi lakini vingi ya hivyo kwa sasa vimekufa. Lakini ili uwe na uchumi wa viwanda inabidi uhakikishe upatikanaji wa uhakika wa umeme na kwa bei ambayo watu wanaimudu. Sisi nadhani kwenye hili tumefeli ...jinsi miaka ilivyokwenda mbele ndio umeme wetu umezidi kuwa wa kutoaminika.

Kuhusu suala la service industry, nadhani kwenye hotuba ya mwaka huu wamepitisha bajeti ya ICT fiber backbone $170 million kwa nchi nzima kwa kutarajia EASSy na SEACOM cable pia zitafika by 2010. Sijui nchi kama nchi kuna mkakati wowote kisera, kodi, umeme wa uhakika n.k.... kwa kutumia hii kama njia ya maendeleo au tunafanya tu kwa sababu dunia inaelekea huko au tumepata ufadhili. Kwa Kenya wenzetu wako busy kuhakikisha kuwa watatumia nafasi hiyo kuanzisha 'calling centres' ili waweze kupata asilimia fulani ya hii biashara ambayo ni India ndio inachukua kiasi kikubwa.

Ukija kilimo na nianze kwa mfano mdogo. Hapa UK nilipo kwa sasa nikiwa nasoma, ukiingia supermarkets utakuta 'organic fruits & vegetables' zinapata bei kubwa kweli ukilinganisha na GM products or non-organic, na mwelekeo ni kuwa watu wanapenda zaidi organic products. Zaidi ya hilo matunda yenyewe..(mfano embe) ukiangalia majority unakuta hayana uzuri kama matunda ya nyumbani TZ. Hii ina maana kama tungejipanga sawasawa kisera, vifaa, ujuzi kwa wakulima wetu ni opportunity kubwa kwetu kuuza kwenye haya masoko. Tusingumzie kuhusu nyama..tuna ng'ombe wengi kushinda Botswana lakini wenzetu wako mbele kuuza nje zaidi yetu.

Tunaweza kuongelea mengi zaidi ambapo opportunities za sisi kama nchi kuendelea kwa kasi ya ajabu zipo ila tumelala kama nchi na kukubali hali tuliyonayo kama ndio destiny yetu kama taifa. Nadhani umefika wakati wa kukaa na kujiuliza tupo kwenye njia sahihi kweli ...na sidhani kama viongozi wetu huwa wanajiuliza hilo swali au wamebakia kukubali tu Tanzania ni nchi maskini miaka nenda miaka rudi.
 
Sasa Mtarajiwa, weka vigezo vyote hivyo ulivyosema na unavyovijua na uviorodheshe na kisha utuambie sisi tuko nafasi ya ngapi. Chukua kuanzia Rwanda kwenda mashariki hadi Kenya, na kushuka chini hadi Africa Kusini (Ondoa MAlawi iliyotajwa hapo). Je, kuna nchi gani yenye hali mbaya Kiuchumi, Miundombinu, na hayo ulosema kuliko Tanzania?

Ibrah we unafikiri hiyo kazi ni ya robo saa,unapata data unabandika ripoti mara moja?
Waulize hao wa GDP,iliwachukua muda gani mpaka wakakamilisha hayo mahesabu yao?
 
Jamani, wakati mwingine siasa tuweke pembeni. Kwa ukweli ni aibu kwa Tanzania kuweka kundi moja na Somalia, Sierra Leone, Gaza Strip na nyinginezo.

Leo hii Tanzania tunazidiwa na nchi kama Msumbiji, ambayo mpaka mwaka 1992 walikuwa wanapigana wao kwa wao. Sierra Leone pia walikuwa na vita muda mrefu. Somalia, mpaka leo hawana serikali kuu.

Sisi tunajifunza nini ? Hivi tunaposhindwa kuwa na wivu wa maendeleo, ni nini hasa kinatusukuma (What is our drive, as a country) ? Nchi zetu za jirani, mfano Kenya, Rwanda na Malawi, wanaunganishwa na barabara za lami kwa trunk roads zao. Sisi hilo bado.

Lazima tufikie mahali tujuilize kwa nini sisi tu ?

Tanzania tuna rasilimaliwatu kubwa tu na iliyo bora, lakini mbona nchi haisongi mbele ?

Hii ni mada nzuri sana, na nilitegemea JF kama a respected Thinktank tungeweza kuichangia kwa mapana na marefu.

Binafsi naona yafuatayo:

1. Tuhamasishe ubora wa bidhaa kila sekta ya kilimo ili kuweza kukidhi soko la ndani na hatimaye la nje. Hii ina maana hatuna haja ya kuingia bidhaa kama matunda, mboga za majani, kuku n.k. Hivi vyote vizalishwa nchini kwa ubora kwa ajili ya soko la ndani na baadae la nje.

2. Tuhamasishe ubora wa huduma katika viwango vya kimataifa (world class) na kuwawezesha wazawa kuendesha huduma hizo. Kwa mfano, makampuni ya Utalii, mahoteli n.k. Wazawa wapewa kipaumbele. Hivi ndivyo nchi za wenzetu zinavyoendelea.

3. Kuwe na uchocheo(stimulus) kwa ajili ya vijana/wazawa wenye haiba ya ujasiriamali na uthubutu. The daring souls wapewe misamaha ya kodi na wasaidiwe katika kupata na kukuza mitaji yao katika biashara/ujasiriamali.

4. Rasilimali zote (ambazo ndio haswa nguzo kuu yetu kwa uchumi wa baadae) zitumike vizuri kwa sababu rasilimali hizi zinakwisha (depletable resources). Lazima kuwa mlinganyo kati ya mwekezaji na mwenyenacho (nchi). Lazima tuwe na win-win situation na hii inakubalika duniani kote. Return kubwa itakayopatikana katika rasilimali/madini iwekezwe kwenye kujenga na kuendeleza miundombinu na mageuzi ya kilimo. Ni aibu kwamba bonde letu la Rufiji lina uwezo wa kulisha nchi nyingi za Afrika, lakini sisi kama nchi hatujaweza kulitumia na kutuwezesha kutupa akiba walau ya mwaka mmoja.

5. Lazima tufikie mahali tuchague viongozi wetu kutokana na merits zao na si vinginevyo. Tutakapokuwa na uongozi mzuri wenye uthubutu, wenye uchu wa maendeleo, huku ukipata support ya wananchi, nchi itasonga mbele. Lazima viongozi wetu wawe ni watu wenye kupenda kuleta maendeleo katika nchi yao au jamii inayowazunguka, na kuacha kumbukumbu ya mambo mazuri waliyoyafanya kwa miaka mingi ijayo.

Yangu machache.
 
asante kwa muanzisha thread......lazima tupelakana shule hapa ili tuelewane,ooyi

Kuna mdau kasema GDP sio kigezo cha kupima utajiri wa nchu husika....lazima aelewe GDP ni nini,ooyi....GDP au GDI I for income is one of the measures of national income and output for a given country's economy.

Pia you can say that as the total market value of all final goods and services produced within the country in a given period of time (usually a calendar year)

In simple mathematics GDP=consumption + gross investment + government spending + (exports − imports)
 
Ninukuu wapi niliposema Tanzania ni Dar Es Salaam tu
Ndiyo mana nikasema usome na uelewe dhana nzima ya mtoa hoja,usichukue kipengere kimoja ambacho ni mfano tu na ukasema ndiyo hoja yenyewe

Mkuu Ndio maana nakwambia utoe siasa zako, hii typical siasa tunakuomba evidence ya kitaalam huna haya lete ubishi tuu au ndio kudesa huko
 
As far as GDP ranking is concerned,population ndogo ni advantageous

Haya mkuu tupangie ya kwako maana hiyo East Timor ina population ndogo kuliko Tanzania
Tukirudi kwenye hoja yako mbona China Ipo JUU ?
 
Ibrah we unafikiri hiyo kazi ni ya robo saa,unapata data unabandika ripoti mara moja?

Waulize hao wa GDP,iliwachukua muda gani mpaka wakakamilisha hayo mahesabu yao?

Mkuu naona unajijibu kama wenzako imewachukua miaka mingi ku compile information sasa wewe mbona unatupa cheap solution hayo unayodai kila mtu anajua kama una kipya tupe barazani hapa
Sifa moja ya Jamiiforums ni we dare open sasa kama ni makosa ya viongozi wetu lawama na zao kama sifa ni za Tanzania nzima

West Bank $ 800 2002 est.
218 Niger $ 800 2003 est.
219 Afghanistan $ 700 2003 est.
220 Ethiopia $ 700 2003 est.
221 Eritrea $ 700 2002 est.
222 Comoros $ 700 2002 est.
223 Congo, Republic of the $ 700 2003 est.
224 Burundi $ 600 2003 est.
225 Congo, Democratic Republic of the $ 600 2003 est.
226 Tanzania $ 600 2003 est.
227 Malawi $ 600 2003 est.
228 Gaza Strip $ 600 2003 est.
229 Sierra Leone $ 500 2003 est.
230 Somalia $ 500 2003 est.
231 East Timor $ 500
Hizi nchi zote zina matatizo yanayoeleweka je Tanzania in Tatizo gani linaloeleweka ? (UFISADI)
 
Wanajamii ....unajua yote tunaweza kuongea na kumwaga sera na kadhalika lakini nadhani tatizo kubwa ni uongozi wetu....kama Kikwete mwenyewe kwa kinywa chake alishawahi kukiri kuwa hajui kwa nini Tanzania ni maskini sijui
kama kuna kuendelea hapo zaidi ya usanii au kama ni kuendelea ni kwa kudra za Mwenyezi Mungu.

"......Akihojiwa na kujibu maswali kwa Kiingereza fasaha, Rais wetu aliulizwa: "There's a sense from what you're saying of this tremendous potential in Tanzania. You have great agricultural potential, mining potential, tourism potential, but it's taking a long time to realize this potential. What do you think is holding Tanzania back?"

Rais Kikwete alijibu: "I don't know. Of course this is precisely the question that I ask every day, what is it that we have not done? I think we have been leading the continent in terms of attracting mining investments in the mining sector. But we are still working (on attracting investment to other sectors). Maybe the message has not quite reached home".

Kwa tafsiri isiyo rasmi ya mahojiano hayo yaliyotundikwa kwenye mtandao wa internet, Rais Kikwete aliulizwa kwa nini nchi yake bado iko nyuma kimaendeleo na inachukua muda mrefu kugeuza rasilimali zake kuwa maendeleo wakati imejaliwa rasilimali nyingi ambazo ameshazitaja.

Rais alijibu: "Hata mimi sielewi. Hili ni swali ambalo hata mimi huwa najiuliza kila siku, ni nini ambacho hatujafanya. Nafikiri tunaongoza barani Afrika katika kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini... Lakini bado tunaendelea kuvutia uwekezaji katika sekta nyingine. Labda ujumbe bado haujafika vilivyo."

Kiongozi Mkuu wa taifa, CCM na Serikali amekiri katika jukwaa la kimataifa kwamba hajui sababu za taifa lake kuendelea kuwa maskini wakati juhudi za kila namna zimefanywa kutokomeza maadui watatu wa maendeleo (Ujinga, Umaskini na Maradhi). Rais wetu mwenye shahada ya uchumi ya chuo kikuu amekiri wazi kwamba hajui sababu za Tanzania kushindwa kutumia watu wake (milioni 36+) na ardhi yake (kilomita za mraba 886,037) yenye rutuba na madini kemkemu kuleta maendeleo....."

source: Makala -Umaskini hauishi Tanzania Kutoka Tanzania Daima



Kwa maana ya hapo juu inawezekana yeye aliomba uongozi ili,

1. Aridhishe hitaji lake la moyoni kuwa aliwahi kuwa rais wa Tanzania

2. Atumie nafasi hiyo yeye binafsi, familia na kundi lake kujinufaisha na rasilimali na fursa zozote zilizopo

3. Au alikuwa anatest zali kuona kama atapata au atakosa ......ambayo sina uhakika nayo sana.
 
Ninakubaliana na wewe kuhusu nchi yetu kuwa chini japo supporting link yako ipo outdated kidogo ni ya 2003, ila kama hiyo uliyotoa ni kweli basi kunaprogress in the next 5 years from 2003 to 2007. Ila ukweli ni kwamba Watanzania tumejawa zaidi na ubinafsi na greed ndiyo maana hatuendelezi nchi. Wizi wa mali ya umma imekuwa ni kasumba ya watendaji wengi wakishirikiana na wafanyabiashara tapeli wa taifa letu. muingiliano wa siasa na biashara pia ni adui mkubwa wa maendeleo yetu. Mfano watendaji wengi wa chama tawala(CCM) mikoani ambao wengi ni illiterates wamekuwa kama miungu watu, wanalazimisha wafanya biashara kuchangia siasa badala ya kuajiri zaidi wananchi ili wapate kipato na ku catalyse consumption ambayo itachochea production na kuongeza ajira zaidi. Tusitarajie maendeleo ya haraka kama watu wetu hawana hela za kununua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu. Chukulia issue za EPA, RICHMOND and many many many many insider dealings of the Top politicians. Hawa ndiyo maadui wakubwa wa maendeleo kama hela zile zingegawiwa kwa wajasiliamali wakaajili watu na kutoa ajira nyingi zaidi leo tungekuwa mbali, badala ya vijisenti hivyo kuwekwa offshore na walafi wanaojiita viongozi ndani ya CCM huko offshore vikisubiri interest na wengine wanakufa na kuacha account nje ya nchi without the notice of the country and ending up losing a lot of money for our country.

Ila kwa recent data on GDP unaweza kucheki below halafu uta-conclude

http://siteresources.worldbank.org/DATASTATISTICS/Resources/GDP.pdf
 
Ninakubaliana na wewe kuhusu nchi yetu kuwa chini japo supporting link yako yako ipo outdated kidogo ni ya 2003, ila kama hiyo uliyotoa ni kweli basi kunaprogress in the next 5 years from 2003 to 2007. Ila ukweli ni kwamba Watanzania tumejawa zaidi na ubinafsi na greed ndiyo maana hatuendelei. Wizi wa mali ya umma imekuwa ni kasumba ya watendaji wengi wakishirikiana na wafanyabiashara. muingiliano wa siasa na biashara pia ni adui mkubwa wa maendeleo yetu. Mfano watendaji wa chama tawala mikoani wamekuwa kama miungu watu, wanalazimisha wafanya biashara kuchangia siasa badala ya kuajiri zaidi ili ku catalyse consumption, na hivyo production increase. Chukulia issue za EPA, RICHMOND and many many many many insider dealings in the Top politicians. Hawa ndiyo adui mkubwa wa maendeleo.

Ila kwa recent data on GDP unaweza kucheki below halafu uta-conclude

http://siteresources.worldbank.org/DATASTATISTICS/Resources/GDP.pdf

Mkubwa
Tatizo la msingi la watanzania sio ubinafsi na uchoyo; bali ujinga na ulimbukeni. Wabinafsi, wachoyo, na wezi wanapigiwa magoti na saluti, badala ya kufikishwa mahakamani au selo.
 
Nilikua napitia ilani ya uchaguzi ya CCM......sijui kama wenzangu mmeshawahi kuipitia inaonekana 'theoritically' wanajaribu ku-address issues lakini sio kwa kiwango cha kutosha kwa mimi ninavyoona...sijui wenzangu. Tuipitie tuone kama kweli inauwezo wa kutupeleka kule tunakokata...

ccm_flag_anim.gif View attachment Ilani ya CCM.pdf
 
Granted GDP is not a good indicator of development, but the yardstick is the same for all countries, then the question that begs to be asked is, under this uniform yardstick, why are we ranking this low.

This circumvent the "GDP is not an accurate kipimo" argument.

Ni sawa na kusema "Kuwepo kwa maji si kipimo kizuri cha maendeleo" OK, sawa, lakini kama nchi yetu ina utajiri mkubwa wa mito na maziwa, kwa nini tukose maji? Mpaka wa Saudi Arabia na Mauritania walio jangwani wanatupita? (The maji mfano is hupothetical to illustrate the validity of the outrage, even if it is based on GDP)
 
Nilikua napitia ilani ya uchaguzi ya CCM......sijui kama wenzangu mmeshawahi kuipitia inaonekana 'theoritically' wanajaribu ku-address issues lakini sio kwa kiwango cha kutosha kwa mimi ninavyoona...sijui wenzangu. Tuipitie tuone kama kweli inauwezo wa kutupeleka kule tunakokata...

View attachment 2719 View attachment 2718

Mkuu sikudanganyi kuisoma hii kitu mimi naona na waste of time, kama wao hawaifuati means it is not practical na wanatudanganya tu. Ila mimi kinachonifanya nipate mashaka ni wao kung'ang'ania madaraka kwa slogan yao wanayoiita "KUSHINDA KWA VYOVYOTE", hili ndio la kujadili hapa. wawaache wananchi wachague viongozi wao na sio kuwalazimisha kwa kuwaibia kura zao na kubadili priorities zao.
 
Mkuu sikudanganyi kuisoma hii kitu mimi naona na waste of time, kama wao hawaifuati means it is not practical na wanatudanganya tu. Ila mimi kinachonifanya nipate mashaka ni wao kung'ang'ania madaraka kwa slogan yao wanayoiita "KUSHINDA KWA VYOVYOTE", hili ndio la kujadili hapa. wawaache wananchi wachague viongozi wao na sio kuwalazimisha kwa kuwaibia kura zao na kubadili priorities zao.

Kuisoma na kuijua kipengele kwa kipengele pia inaweza kuwa silaha yako unapokuja uchaguzi mwingine....kwa sababu utakuwa unajua waliahidi nini na hawakutekeleza au wametekeleza kwa kiwango gani, vile vile ujuzi huo wa kuijua hii ilani ndani na nje unaweza kuutumia kumconvince jirani yako anayeishabikia CCM bila kujua lolote......Kutokusoma na sio ilani tu ndio kosa kubwa watu wengi tunalolifanya.
 
Haya file hilo wakuu
Labda litatuongezea ufahamu kidogo kuhusu GDP na economic indicators nyingine
NB;Tuko pamoja katika hopa za kujiletea maendeleo na kuondokana na umasikini.
 

Attachments

Mkuu Ndio maana nakwambia utoe siasa zako, hii typical siasa tunakuomba evidence ya kitaalam huna haya lete ubishi tuu au ndio kudesa huko

Mkuu file hilo hapo juu labda litakupa mwanga kidogo na ninachokitetea
 
Mkuu file hilo hapo juu labda litakupa mwanga kidogo na ninachokitetea

Mtarajiwa, ni sawa lakini GDP ndio mara nyingi inatumika kama proxy indicator ya 'human development and well-being'. Kwa maana hiyo mimi kama investor au social-scientist kwanza nitaanza simply kuangalia GDP kabla sijazama kwenye other indicators ili kupata picha kubwa zaidi.

Kwa hiyo kama ni investor, GDP tu ikiwa ovyo inaweza kunikatisha tamaa sana kuinvest kama natarajia kuinvest with big capital......kwa sababu ukiwa na low GDP ni likely, kuwa na huduma mbovu za afya, miundombinu mibovu, limited skilled labour n.k.....

The opposite ya hili (GDP kubwa au inayoonekana kukua kwa kasi) inacreate interest especially kwa investor kuona kuwa kuna opportunity kwenye specific country.
 
Mkuu file hilo hapo juu labda litakupa mwanga kidogo na ninachokitetea

Sasa mkuu mbona unaleta mambo ya shule sasa data ni za nchi tatu dunia ina nchi zaidi ya 230

1.Kama utakubali GDP ni formula in the economic perspective wewe utaweka figure tu na chombo kinacho aminika ni World Bank nd IMF to give you fair results kwani hata Watanzania wapo wanafanya kazi kule
2. sasa ukiltaka ranking ya mortality rate or maternal death, and life expectancy for each country WHO wanazo na wanatumia sama rules na nchi zipo ranked
3. kama ukitaka iliterate rate kuna UNICEF
4. Wakimbizi ipo UNHCR na hii sisi ndio tunaongoza

na vitu vyote vipo ranked separately na hao walioderive hivyo vitu wamabobea kwenye fani hiyo sio wanafunzi
Kwa kuwa mtu anaanza kutambaa halafu kutembea ndio akimbie lazima walisoma hiyo attachment Shuleni
Na wameweka nchi tatu kwa sababu ya kurahisisha kuelewa
Huwezi kuweka mambo ya life expectacy kwenye GDP every thing was considered well before agreed by every country sasa kama hutaki hutaki tuu
 
Back
Top Bottom