Mugizi
Member
- Aug 14, 2008
- 18
- 2
Nakubaliana kabisa na wale wanaosema kwamba GDP haiwezi kutoa picha halisi ya utajiri au umaskini katika nchi, na hasa kama nchi ni Tanzania ambapo sehemu kubwa ya uchumi wetu haiwi haionekani katika takwimu kutokana na ukubwa wa sekta isiyo rasmi huku kwetu. Kwa mawazo yangu kipimo tulicho nacho hapa kinachoweza kukaribia hali halisi ni Household Budget Survey (2001/2 and 2007/8 version found at National Bureau of Statistics Tanzania Official Website) kwa sababu hapa tunapima consumption na siyo production kwa hiyo hata sekta isiyo rasmi inazingatiwa.
Kwa maoni yangu wakati mwingine umaskini wetu unatokana na maamuzi tunayo ruhusu yachukuliwe na viongozi wetu. Nimeambatanisha presentation inayoelezea uchambuzi wa bajeti uliyofanyika katika sekta ya maji hivi karibuni nikijaribu kuelezea point yangu. Tukiendelea kupanga bajeti kila mwaka bila kufuala muelekeo unaoeleweka sijui kama tutafika kweli.