Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa mujibu wa Adam Smith yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayoweza kusaidia nchi kuzalisha mali au utajiri kwa wingi zaidi na hivyo nchi kuwa na hali bora zaidi ya kiuchumi na maisha kwa watu wake:
1. kuongezeka kwa rasilimali zilizopo nchini (lakini pale tu rasilimali hizo zinapoingia kwenye Mfuko au Hazina ya nchi na sio kwenda nje),
2. Ugunduzi au uvumbuzi wa teknolojia mpya ( hili linawezekana kwa nchi iliyo na fungu la Research and Development na linalowasaidia na kuwanyanyua watu waliosoma na wasiosoma mara wanapogungua kitu fulani badala ya kuwakwaza kwa kisingizio chochote kile),
3. kuongezeka kwa mgawanyo wa kazi na uzamili au ubingwa katika shughuli mbalimbali ( pale ambapo mwalimu inampasa awe mkulima, mfugaji, mfanyabiashara na kadhalika ni vigumu hili kuwezekana),
4. kuongezeka kwa njia bora za mgawanyo na matumizi ya rasilimali katika nchi (kama asilimia kubwa ya rasilimali za nchi inakwenda katika kununua magari ya kifahari, au kulipia mafuta -kitu ambacho kinaendelea na ghali zaidi- au safari na misafara ya kwenda nchi za nje haiishi basi rasilimali zinakosekana katika kuwekeza kwenye maeneo ambayo yangelichangia kuondoa umasikini nchini), na
5. kuongezeka kwa kiwango cha matumizi ya rasilimali zilizopo (katika lugha ya menejimenti kuna maneno mawili muhimu. Nayo ni 'effectiveness' na 'efficiency'. 'Effectiveness' ni kuzalisha kile kinachotakiwa na kukubalika na soko, wakati 'efficiency' ni kuzalisha kwa usahihi au kwa gharama inayokubalika.
Tuna matatizo katika yote mawili. Na maneno haya mawili yatakuwa yakijirudia tena na tena kadri tunavyoendelea na mazungumzo yetu ya uchumi. La muhimu hapa ni kwamba watu wawili wanaweza kuwa na rasilimali kiasi kile kile lakini mmoja akawa more effective and more efficient na hivyo kutajirika na mwenzake akabaki palepale. Japan haina rasilimali yoyote ya maana ukilinganisha na Tanzania zaidi ya watu wake. Hivi leo ukiwatoa Wajapani wote toka Japani na kuwapeleka Watanzania wote Japani na Wajapani wote wakaja Tanzania kwa sababu ya Watanzania kutomudu effectiveness and efficiency Japan itamasikinika na Tanzania (Ya Wajapani wakati huo ) itatajirika.
Tanzanian families getting richer, report says
DASSU STEPHEN
Daily News; Wednesday,November 19, 2008 @21:15
Income poverty at the household level has significantly decreased among Tanzanians over the past six years, Deputy Minister for Finance and Economic Affairs Jeremiah Sumari has said. Sumari quoted recent studies in Dar es Salaam yesterday indicating a significant segment of the local population who could not afford basic needs had gone down to 33.2 per cent - from 35.7 per cent between 2001 and 2007.
The deputy minister was speaking during an official opening of a three-day consultative meeting on a National Strategy for Growth and Reduction of Poverty (NSGRP) and Public Expenditure Review (PER). Mr Sumari also said the studies had also shown that food availability was also rising: some 19 out of 100 people in 2007 were able to cater for their food needs as compared to 16 out of 100 people in 2001.
Local experts also say the Gross Domestic Product (GDP) in the country is reported to have increased from 6.7 to 7.1 per cent within the same period of time. The other sectors which have in recent past witnessed a significant improvement included education, health, tourism, infrastructure and communication, said Mr Sumari.
He reiterated that the government through the 2025 development vision will continue to improve living standards among its people in all aspects of life. Speaking in the same occasion, a representative of development partners, Ambassador Tim Clarke, stressed a need for people's participation and good governance as a requisite in fighting poverty among the grassroots. It very important to make effective and efficient use of public resources .. Dialogue that includes all key stakeholders is also very important in promoting peoples development and public ownership, he noted.
GDP kisiwe kipimo pekee cha kusema nchi gani ni tajiri zaidi duniani na nchi gani ni masikini wa kutupa.
Watu wa development studies wana kitu wanaita INDICATORS OF DEVELOPMENT,ambayo ina vitu vingi ma hiyo GDP ikiwa ni kasehemu tu ambavyo kwa pamoja ndivyo vinapima uwezo wa kimaendeleo wa nchi tofauti.
Kuna vitu kama huduma za kijamii kwa mfano shule,hospitali,zahanati,maji safi na salama,kuna walimu wangapi katika nchi,uwiano wa madaktari na wagonjwa,vitanda hospitalini nk
Kuna vitu kama miundombinu,barabara,reli,,anga,simu,mzunguko wa pesa,upatikanaji wa ajira,nk nk
Mambo yako mengi.Kwahiyo unaposema GDP pekee ndiyo kipimo cha maendeleo,si kweli.Inabidi uziangalie hizo indicators zote halafu ndiyo utupangie list ya matajiri na masikini.
Halafu hiyo GDP yenyewe inatafutwaje?iko even?Nchi kama Luxembourg ina watu wasiozidi 500,000(laki tano),hiyo population ni kama mara sita ndiyo ifikie population ya watu wa jiji la Dar Es Salaam kwa mfano.Sawasawa na Rwanda na Burundi ambazo nazo zina idadi ndogo ya watu.
Manake kanchi kenye watu wadogo kama Luxembourg,ni sawa na mkoa fulani wa Tanzania au mji fulani wa Marekani au nchi nyingine kubwa.ukikafanyia hiyo GDP ni sawa labda kwa mfano ufanye GDP kwa sehemu nyingine kwa uwiano huohuo.Kwamfano ukifanya GDP ya mkoa wa Dar Es Salaam,utapata nzuri sana zaidi ya hiyo 600.
Kwahiyo point hapa ni hiyo uneven distribution of incomes in different parts of different populations in a big country like Tanzania.
Ndiyo utaona bajeti ya ulinzi ya Marekani ni zaidi ya bajeti ya nchi tano za ulaya lakini kwenye GDP inashika nafasi ya 2/3/5
Kwahiyo usidanganyike na hizo figure mkuu[/QUOTE
NAKUUNGA MKONO MZEE
Mimi pia sikubaliani na matumizi ya GDP kama kipimo pekee cha umaskini/utajiri. Utafanya kazi kubwa sana kunishawishi kuwa hicho ni kipimo sahihi cha hali nzuri ya maisha. Ethiopia ni nchi iliyochoka sana ukiangalia hali ya maisha kwa sababu taarifa za watu kufa yaani kudead kwa njaa ni ya kawaida sana. Huku mashuleni tunasoma nao na wanaonekana na hali mbaya sana na wanasema wazi jinsi ambavyo hali kimaisha nchini kwao ni duni. Mshahara wa university graduates kwenye public sector mshahara wao ni dola 250 kwa mwezi, hela ambayo si kwamba itanunua vitu vingi kuliko vile amabavyo inenunua Tanzania. Kimsingi tusidumazwe akili na kujiona hatuwezi kabisa eti kwa sababu ya GDP. Hizo ni hadithi za mila za kishenzi tulizoletewa na wakoloni.
Hivi leo duniani kuna takriban nchi 231 duniani. Kiuchumi, Tanzania, Malawi, Gaza Strip, Sierra Leone, Somalia na East Timor ndio nchi sita hoibintaaban za mwisho ulimwenguni.
Hadi kufikia sasa katika nchi yetu ilipofikia ni sawa Gaza Strip ya Wapalestina ilipo? Sisi , Gaza na Malawi wote tuna GDP per capita ya dola 600 za Kimarekani. Waliopo chini yetu ni nchi zilizoathirika sana na vita na misukosuko ya kijamii nazo ni Somalia, Sierra Leone na East Timor. Sierra Leone na East Timor baada ya mwaka huu, hata hivyo, lazima ziwe juu yetu kwa hiyo nchi itakayokuwa ya mwisho kabisa itakuwa ni Somalia ikifuatiwa na Tanzania. Tujiulize ni wapi tulipokosea, tunapokosea na tutakapoendelea kukosea? Ya kwamba pamoja na kugundulika utajiri mkubwa wa dhahabu na madini mengine hali ya Watanzania ndio imezidi kuwa mbaya kuliko ya watu wote duniani isipokuwa Somalia.
Unataka ushahidi nenda hapa:
World Facts and Figures - GDP per capita by country
Hivi leo duniani kuna takriban nchi 231 duniani. Kiuchumi, Tanzania, Malawi, Gaza Strip, Sierra Leone, Somalia na East Timor ndio nchi sita hoibintaaban za mwisho ulimwenguni.
Hadi kufikia sasa katika nchi yetu ilipofikia ni sawa Gaza Strip ya Wapalestina ilipo? Sisi , Gaza na Malawi wote tuna GDP per capita ya dola 600 za Kimarekani. Waliopo chini yetu ni nchi zilizoathirika sana na vita na misukosuko ya kijamii nazo ni Somalia, Sierra Leone na East Timor. Sierra Leone na East Timor baada ya mwaka huu, hata hivyo, lazima ziwe juu yetu kwa hiyo nchi itakayokuwa ya mwisho kabisa itakuwa ni Somalia ikifuatiwa na Tanzania. Tujiulize ni wapi tulipokosea, tunapokosea na tutakapoendelea kukosea? Ya kwamba pamoja na kugundulika utajiri mkubwa wa dhahabu na madini mengine hali ya Watanzania ndio imezidi kuwa mbaya kuliko ya watu wote duniani isipokuwa Somalia.
Unataka ushahidi nenda hapa:
World Facts and Figures - GDP per capita by country