Pundit
JF-Expert Member
- Feb 4, 2007
- 3,733
- 141
Come on man, what is this now? What exactly do you mean, sir? I'm finding it harder to understand what you are saying because you use "big" words. Can you use small words?
You can get very convincing.
Kifupi mtu wangu hapo juu kai break down vizuri anakupa picha halisi kwamba umasikini wetu bongo watu wanashindwa kulipa kodi ya chini ya dollar mbili kwa mwaka, kiasi cha kuwafanya wakimbie miji yao na kwenda maporini. Granted we do not have a very money based economy, lakini dollar mbili? Kwa mwaka? Hata kama unataka kuiangalia katika mtazamo wa shilingi, kwa maana ya kuwa purchasing power ya dollar mbili ni pipi na shilingi elfu mbili inaweza kununua lunch nzuri Dar au mlo wa wiki kwingineko, bado ni kiasi kidogo sana kumkimbiza mtu nyumbani. HApo ina maana huyu mtu anayekimbia kodi ya elfu mbili hana uzalishaji wa kufikisha elfu mbili, kwa sababu angekuwa na uzalishaji angejikakamua na kuilipa ili asiendelee kupoteza muda. Hapo kuna maswala ya elimu, uchumi, historia siasa utamaduni yanaingiliana.
Sasa hapo kuna GDP ya 1500 kweli? na hata kama ipo ni kwa sababu Chenge na mabilioni yake anaushikia hizo namba za wastani za mkoa mzima, kwa hiyo swala lingine la kuangalia ni mgawanyo wa mapato. Akija Bill Gates kuwa mtanzania na billioni 60 zake GDP yetu itapanda zaidi ya mara mbili overnight, hii haina maana kuwa watanzania watazidisha kipatao zaidi ya mara mbili overnight.