NINADHANI Watanzania wameshiba porojo, visingizio na sababu hii au ile ya kutoweza kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa.
Simply, kwa sababu hii ni nchi ya wababaishaji. Kila mtu anajifanya anajua. Na kwa sababu kila mtu anajua ni sawa na wote hatujui.
Nilipoanzisha mada hii nilidhania tutaichukulia kwa uzito wake. Hapa cha muhimu ni kujiuliza kwanini miaka karibu 50 baada ya uhuru nchi yetu iliyokuwa mkiani wakati wa uhuru hadi leo bado iko palepale mkoani.
Wanaobisha wanakumbuka India, Malaysia, South Korea, Japan yenyewe, Singapore, Mauritius, Botswana na kadhalika zilikuwa wapi. Na sasa ziko wapi.
Hii ina maana moja tu. Kwamba kuna kitu wanachokijua na walichokifanya ambacho sisi hatukijui na hatujakifanya. Ukichunguza viongozi wetu wengi wametoka kwenye umasikini mkubwa, iwe Nyerere mwenyewe, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na usiseme hao wa Zanzibar!!! Hawa kazi yao kwanza ilikuwa kujineemesha wenyewe, kisha familia zao na kisha ndugu, jamaa na marafiki zao. Sasa hatujui maana Kikwete sio masikini kiasi hicho kama na yeye atakwenda njia hiyo hiyo au atataka kwanza awatajirishe Watanzania kisha ndio ajifikirie yeye mwenyewe [kama atajitenga na wafadhili wake na maswahiba zake wakubwa walioichafua nchi kiasi ilichochafuka leo pamoja na kukwanya na Baba wa taifa kabla hajafariki!]. Hilo ni shauri lake. Akiachia na yeye zawadi ya Mo Ibrahim hata kwa Muumba hatakuwa na sababu ya kujietetea! Akumbuke Kurani takatifu inasema mke, mali na watoto [na marafiki-ongezo langu] ni MTIHANI mkubwa! Akipita huu tu kafaulu!
Turejee kwenye pointi, ili tuendelee ni lazima tufanye mambo haya:
. Kwanza tutambue kuwa kelele zetu za kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu hazijatusaidia kitu,
. ujenzi wa viwanda umetushinda,
. fedha na mitaji hatuna,
. njia rahisi ya kupata fedha na mtaji ni biashara na sisi tunailegezea, wakati wenzetu Dubai wanapaa,
. sekta nyingine ya kujilimbikizia ni huduma lakini serikali yenyewe legevu inaachia uchafu kila mahala na hakuna anayelalamika wala kujali. Tumeshazoea. Kampuni za usombaji taka ni chafu kuliko taka zenyewe!
Usiseme kuhusu bustani na maua-utadhani Ikulu imepiga marufuku tusiwe na bustani na maua majumbani kwetu, maofisini na hasa sisi waswahili-angalau wageni na mabenki yao wanajitahidi,
. tuna wizara kebekebe lakini zinakanyagana vidoleni na inaelekea mawaziri wakubwa kwa wadogo ukiwauliza wanalipwa mshahara kwa ajili gani watakuwa hawana majibu. Kinachotakiwa management by objectives, decentralization, delegation of authority na lean government. Hebu mmoja afanye analysis ya goverment expenditure compared to GDP utakuta seirkali yetu ina ratio kubwa kuliko hata serikali zenye uwezo! Kichaa tupu!
. mama lao ni kwamba hakuna wizara yenye vision yake yenyewe, mission yake na strategic objectives au malengo ni wapi wanakotaka kuipeleka nchi na watu wake kufikia muda fulani. Vipo? Ninaomba iwe huu ni uzushi wangu. Nambieni basi wizara zina vision, mission na strategic objective jamanai? Katika karne hii , miaka hii ikiwa tunakwenda sawasawa na kina Mzee Malecela, Kawawa,Waryuba, Msuya na kadhalika tumekwisha!
. Kubwa na baya zaidi ni kule watu wa CCM kujiona wao ndio wana akili kuliko Watanzania wote [siku hizi ninasikia tuko milioni 40 latest UN figure-2007] tukiwekwa pamoja. Hakuna njia ya mkato ya kuikwamisha nchi kimaendeleo kama ubaguzi wa kivyama. Yaani chama kimoja kubagua vyama vingine na watu wake na kuwapa hata wababaishaji na wajinga nafasi ya uongozi ingawa wanajua fika hao ni wajinga na kazi hiyo hawataiwezea. Mfano mzuri ni Zanzibar na hali iliyofikia sasa.
Zanzibar yenye watu milioni 1 tu ina kila sababu ya kuwa na GDP per capita ya dola za Kimarekani tena 5,000 hadi 10,000. Lakini wameishia kuwa na gomvi za kuku na bata huku wakigharamia ng'ombe na ngamia eti kwa kuwa huyu ni CUF hafai, sasa wanakufa na vikoi vyao kiunoni na hakuna chochote kilichoviringishwa kwenye kunjo lake!
KUJENGA UCHUMI pamoja na hayo yote pia kwahitaji kwanza kutoa elimu ya:
-UCHUMI
-MENEJIMENTI
-BIASHARA
-UHASIBU
-RASILIMALI WATU
kwa lugha ya Kiswahili. Pungufu ya hapo mwaka 2010 nchi duniani zitaongezeka na kufikia 250 na nina hakika Tanzania itakuwa ya 249! Poleni wanangu na wajukuu wangu! Mbona mnalo!