Tanzania's Tundu Lissu recovering well at Aga Khan Nairobi

Haki za binadamu ndio nini? Ujinga na utoto anaofanya Tundu mimi ndio ningekuwa Rais ningeshamuondoa siku nyingi.
Naona hotuba za mkuu zimeku-Hemsha na umepata Mhemko mpaka kufikia kutoa uhai wa binadamu mwenzako!!Kama umeumia basi jaribu kutoa uhai wa waliosaini hiyo mikataba!!!!
 
Matibabu kenya ni bora kuliko Tanzania.
Katika suala hili japo sina ushahidi lakini ninaweza bila wasiwasi kwamba huna taarifa za kutosha katika hili, Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika eneo la tiba, hasa katika specialized medicine, hivi hujui kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee katika east and central Africa ambayo haipeleki tena wagonjwa wa moyo nje ya nchi na badala yake inapokea wagonjwa wa moyo toka, Kenya, Uganda, DRC, Malawi, Comoro na Zambia?, hivi hujui kwamba Tanzania ndiyo yenye Hospital kubwa na well equiped ya kutibu cancer kuliko zote kanda hii(Ocean road cancer institute)?, Hivi hujui kwamba the most ultra morden Hospital ipo Tanzania?(Mloganzila teaching Hospital)

This is most beautiful comment ever
 
Reactions: Oii
I thought the amount of hatred that you spew on Kenyans arose from some warped fear of something. I had no idea you would despise a fellow Tanzanian with similar zeal; u clearly a wasted sperm
 
Sasa ni zamu ya Wakenya kutusaidia kwa kutushauri na kutupatanisha kama sisi tulivyowashauri na kuwapatanisha kwenye yale mauaji yaliyotokana na uchaguzi. Please its your turn now Kenyans to help us. We cant pretend that we are that much safe, while the reality on the surface shows the opposite! Rais Uhuru Kenyata tafadhali usikae kimya kama jinsi ambavyo Mkapa hakukaa kimya wakati mlipokuwa kwenye matatizo wakati huo. Mgonjwa huwa haulizwi dawa! Jamii yetu inelekea kufarakana, tunahitaji sana jamii yetu ipatanishwe. Tusiendelee kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Kwani mnataka mpaka wapigwe risasi wangapi ili tuhitaji msaada wa matengamano? Haiwezi kukanushika kuwa motive ya jaribio hili la mauaji ni ya kisiasa! Tanzania is bigger than politics! Tanzania and by then Tanganyika was there even before she was assigned the name Tanganyika! She was there even before Nyerere! leave alone TANU, CCM, CHADEMA, CUF and many others with their previous and current leaders! This "blood thirsty" politics is quite new to our society! We even got independence without shading a single atom (leave alone a single drop) of blood! What has happened to my beloved country Tanzania! Hata tukiwa maskini sawa lakini tuwe matajiri wa amani. Simhukumu yeyote maana sijui, lakini Mungu anamjua aliyezalisha moyoni mwake hili wazo la kudai damu ya Tundu Lisu, kisha akaliwekea ratiba ya utekalezaji kwa namna moja au nyingine. Niwakumbushe tu kuwa damu ina kawaida ya kudai kisasi mbele za Mungu! Nawaomba wahusika muogope kitu kinachoitwa kumwaga damu kwa sababu yoyote ile! Utawala wa sheria upewe nafasi ya kuchukua mkondo wake! Na usiombe kisasi cha MUNGU kikushukie, yeye hupatiliza hadi kizazi cha tatu! Mwogopeni Mungu! maana wote tunategemea uhai kutoka kwake.
 
Umeandika na kupambanua vizuri sana mkuu, ila sehumu moja tu ninadhani sio sawa, kuomba msaada toka Kenya sidhani kama Kenya wananguvu wa uhalali wa kukemea mauaji popote pale Afrika, hasa baada ya ripoti ya transparency international ya mwaka 2016 kuitaja Kenya kuwa ni kinara Afrika kwa mauaji ya kiholela yanayofanywa na polisi na wanasiasa, kwa Kenya vifo vya watu 24 baada ya uchaguzi kwao sio habari ya kutisha hata kidogo, wao wanahesabu uchaguzi ulifanyika kwa amani
 
Ni sawa kabisa. Lakini unajua katika desturi za kawaida tu, kama nyumbani kwako kuna hatari, ni jambo la kawaida kuita majirani ili watoe msaada, bila kujali hao majirani wana maadili kiasi gani. Ni vizuri na heshima kuhitaji msaada kwa jirani kabla ya kutafuta msaada wa mbali. Ina faida ya kuimarisha ujirani mwema na kumpa nafasi jirani kujiamini katika kusaidia wenzake hata kama na yeye ana matatizo ya kwake makubwa zaidi.
Lakini pia tuwe wakweli, kiwango cha demokrasi kwa Kenya na kiwango cha kuheshimu utawala wa sheria wametuzidi! Wanacho kitu cha kutuambia hata kama wana mapungufu mengine. Tuachane na kiburi na kuhitaji msaada mapema kabla mambo hayajaharibika zaidi. Unajua ukigombana na mkeo halafu jirani akaja kuwasuluhisha, siku nyingine utajiepusha kugombana na mkeo kwa aibu ya kuja kusuluhishwa na jirani!
 
Katika hili mkuu nitapingana na wewe, hivi pale mtaani unapoishi umezungukwa na marafiki na majirani kama nane, ila kati yao karibu wanne ni walevi sana, na kuna mmoja ni mlevi kupita wote na mara kwa mara anampiga mkewe na wewe ndiye uliyeenda kusuluhisha ugomvi asiendelee vitendo hivyo, lakini hajaacha tabia hiyo anaendelea nayo, hivi kweli wewe ukianza tabia ya kumpiga mkeo na ulevi wa pombe unahisi huyu anafaa kuwasuluhisha?, sana sana atasema kimoyomoyo, wewe si ndiye uliyejiona mtakatifu na kunikosoa mimi?, Kama ni majirani mbona tunao wengi wenye sifa angalau nafuu kuliko Kenya?, Msumbiji kwa mfano, lakini tukioana wote hawafai kwanini tusiwaombe Botswana au Mauritius ambao tutawaiga kwa vitendo sio maneno matupu wakati wenyewe wana hali mbaya kuliko sisi?,

Kenya wakianza kuchinjana, hakuna mkenya atakayekimbilia Somalia, na atakayeingia Somalia lengo lake litakuwa ni kama njia tu ili aende ama Djibout au zaidi ya hapo, sio Somalia, kwa sababu hali ya usalama Somalia ni mbaya kuliko ya Kenya
 
Kuhusu demokrasia na uhuru wa kujieleza, unajua ni kama vile mtu aliyezoeleka kuwa msafi muda wote, ikitokea amevaa shati chafu siku moja, kila mtu atashangaa, pamoja na kwamba Magufuli anakandamiza wapinzani na vyombo vya habari, lakini bado tunawaacha Kenya kwa mbali tu katika demokrasia. www.rsf.org
 
Nimeona kuna wasiojitambua wanajitahidi kukosoa uamuzi wa familia ya Lisu na CHADEMA kumpeleka Nairobi ati serikali ilistahili kumhudumia! Sijaona ujinga kama kuruhusu selo na rumande za wahisani kutinza maisha na uhai wa Lisu! Huko nilichokiona siku zote ni umahiri wa kuzuia dhamana kumtaka Lisu kuumia rumande na si kingine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…