Tanzanite iliyonunuliwa na Serikali yavunja rekodi kwa ukubwa duniani | Inaweza kutumika kukuza Sekta ya Utalii

Mmasai kapigwa, hao jamaa wakienda kuuza nje wanatoka na billion 50 minimum.
15 kgs=75,000 carat
1 carat tanzanite= $ 300
75,000 X $ 300= $ 22,500,000
22,500,000 X 2,300= Tshs 51,750,000
 
K Kabisa, wakiuza wao hawakosi billion 50
 
Reactions: BAK
Mmasai kapigwa, hii ndio serekali ya wanyonge ati
 
Reactions: BAK

Hapana. Bei hiyo ni kwa a finished cut and polished stone.

Serikali imenunua rough stone ambayo bado haijakatwa wala kuwa polished. Lakini maswali ni mengi.

1. Nani Mnunuzi?
Tunaambiwa mnunuzi ni Serikali kupitia Wizara ya Madini na Benki Kuu ya Tanzania. Wizara ya Madini haijawahi kuwa mnunuzi wala muuzaji wa madini. Leo wamebeba jukumu hilo.

Imekuaje leo miezi michache kabla ya Uchaguzi, wizara hii imenunua Tanzanite ikisindikizwa na simu kutoka kwa Raisi kutoa pongezi? Je, kuna bajeti katika wizara hii inayoruhusu wizara kununua madini kutoka kwa wachimbaji wadogo na wakubwa?

Ni muhimu hili swali likajibiwa ili DEALERS na BROKERS wajue wana ushindani mpya kwenye soko la ununuzi wa madini.

Ni muhimu pia utaratibu huu wa wizara kununua madini ukawekwa wazi ili WAUZAJI na WACHIMBAJI wakajua soko lao ni pana. Inaonekana Wizarani bei ni nzuri.

2. Thamani ya Tanzanite
Thamani ya Tanzanite inatokana na ubora wa jiwe kwenye rangi, uchongaji wake na mwisho mwelekeo wa soko (demand and supply).

Swali ni, nani kathaminisha Tanzanite iliyouzwa? Ni muhimu kujua thamani hiyo ilizingatia jiwe ambalo limeshakatwa na linahitajika sokoni na kwa grade ipi?

Uthaminishaji huu ndiyo umezaa Bilionea. Uthaminishaji huu umefanywa na Wizara kuzingatia hii ni rough stones au cut & polished?

3. Muuzaji Laizer
Kama kuna makosa ya makusudi kwenye udhaminishaji na muuzaji huyu akalipwa bei ya juu zaidi, ni vizuri kufahamu na kufuatilia transactions za kwenye account itakayoingia hiyo Shilingi 7.8 bilioni.

4. Wizara inamuuzia nani na kwa bei gani?
Wizara imenunua jiwe kwa thamani ya Shilingi 7.8 bilioni. Ili ipate faida, inapaswa kuliuza kwa zaidi ya bei iliyonunulia. Hili ni jiwe ambalo bado halijakatwa wala kuwa polished.

Wizara itamuuzia nani na kwa bei gani? Ikipatikana hasara na kama kuna wizi katika biashara hii, nani anawajibika?
 
Kapigwa vibaya sana Mkuu! Yaani toka 51 billions hasi bilioni 7 na ushee na hapo ndiyo kwa bei ya chini kabisa. Kama Tanzanite yake ilikuwa ni ya daraja la juu basi KAPIGWA zaidi ya bilioni 60 kwenda juu.

Mmasai kapigwa, hii ndio serekali ya wanyonge ati
 

Halafu aliwekeza miaka 17, kila siku alikuwa akiuendesha mgodi kwa laki 6, pia tokea aanze kuchimba hakuwahi kuambulia chochote!
Sasa ikiwa alikuwa anauendesha huo mgodi kwa wastani wa laki 6 kwa siku kwa huo muda wa miaka 16, ina maana ni kama alishatumia wastani wa zaidi ya Billion 3 kwa muda huo wote!

Kwake yeye anaona ni faida tu, isitoshe hadi rais anampigia simu halafu anambwa namna ile, sidhani kama aliwahi kuwaza atakuja kukutana na gavana wa B.O.T! So ukimweleza kapigwa anaona kama unamzingua tu, hizo alizopata zinamtosha!
 
Reactions: BAK
Mkuu hata kwa rough/unpolish Tanzanite bado kapigwa sana tu.

Buy Tanzanite Rough Online | Gem Rock Auctions

 
Ni Malisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…