Tanzanite iliyonunuliwa na Serikali yavunja rekodi kwa ukubwa duniani | Inaweza kutumika kukuza Sekta ya Utalii

Mtu mmoja mwenye shamba alipanda viazi akachimbachimba chimba akapata alumasi looo loo bahaatii looloo bahati ya mtu mwenye shambaaa huu wimbo alitungiwa baba yoyoo yaaani ingekuwa mimi hapo ningetembea kama napaa vile bichwa hilo na ningempigia bill gate nilonge nae bilionea mwenzangu.
 
Nakuunga mkono na miguu hili wazo ila serikali ishayachukua mbona hata Trump atakuja kupiga nalo picha
 
Katika vijana makini wachambuzi na wenye uelewa mkubwa ,basi Malisa GJ ni namba 1.

Nimesoma hii artcle yake juu ya Tanzanite, hadi nimetamani vijana kama hawa wawe msaada kwenye kuweka mikakati ya Taifa hili.

Ivi huyu Kijana ni mbongo kweli?

Kwa kweli sijawahi mwona ila inaonekana ni bonge la genius.

Na #Malisa_GJ
----
Saniniu Laizer mchimbaji mdogo wa madini huko Mererani ameamka Bilionea baada ya kupata mawe mawili ya Tanzanite moja lenye uzito wa 9.2KGs na jingine 5.8KGs yenye thamani ya TZS 7.8 Bilioni.

Watu wengi wanajadili kuhusu Tanzania kumpata Bilionea mpya. Ni jambo zuri lakini kuna jambo jingine ambalo halijadiliwi. Na pengine ni la msingi zaidi kuliko Ubilionea wa Laizer.

Hii Tanzanite ya 9.3KGs inaweza kuwa ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana duniani. Hii ndio "angle"ya habari, ambayo inaweza ikabreak (as breaking news) ikatoa day 2 story na ikatengenezewa developing story hata kwa mwezi mzima.

Kabla ya Laizer kuushangaza ulimwengu kwa kuchimbua ardhi na kupata madini haya makubwa kabisa, Tanzanite kubwa zaidi duniani ilikua na uzito wa 3.3KGs na 16,839 carat. Hii ilichimbwa na kampuni ya TanzaniteOne mwaka 2005.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.mining.com Tanzanite hiyo yenye uzito wa 3.3KGs ipo Thailand katika mji wa Bangkok. Wathai wameamua kuifanya fursa ya utalii. Wanatangazia dunia kwamba "karibu Thailand uone Tanzanite kubwa zaidi". Na watu wanasafiri kila pembe ya dunia kwenda kuona hicho kinachoitwa Tanzanite kubwa zaidi na kupiga nayo picha. Utalii wa aina yake.

Kwa kufanya hivyo Thailand iliweza kurudisha fedha ilizotumia kununua Tanzanite hiyo ndani ya miaka minne tu. Na kuanzia 2010 wanapata faida (super normal profit). Mradi huo umeiingizia Thailand pesa nyingi sana na kutoa ajira kwa watu wengi.

Sasa ni wakati wa kibao kugeuka. Na sisi tutengeneze kituo tuweke haya mawe ya Laizer na tuiambie dunia kuwa Tanzanite kubwa zaidi ipo Tanzania na si Thailand tena. Watu waje washangae hayo mawe wapige nayo picha watulipe 'dollars" wakamalizie picknick Serengeti. Wakitaka kumuona na mchimbaji ruksa.

Hii itatulipa zaidi kuliko kuyauza haya mawe kama tulivyofanya 2005. Pia itafungua fursa mpya ya utalii wa madini ambayo hatujawahi kuwa nayo. Tuige kwa Wathai lakini tufanye kwa ubora kuliko wao (ujasusi wa kiuchumi).
_
Kama watu waliweza kusafiri kutoka Marekani, China, UK etc kwenda kushangaa Tanzanite ya 3KGs kule Bangkok, sisi tukisema tunayo ya 9KGs hata shetani si anaweza kuja kushangaa kidogo akapate cha kusimulia kuzimu?
 
Bilion 7.4 akiweka deposit bank tyfanye akipewa 10% ni milion 740.
ukigawa kwa mwezi ni milion 60
ukigawa kwa siku 30 ni = na milion 2 kwa kila siku.
Dah wazeee wa kukokotoa ila angetakiwa apewe mtaalamu wa saikolojia akae mahali hata mwezi kupumzisha akili na mwili akirudi aitumie hela yake kwa hekima na maarifa bila hivyo anaweza pata kihoro.
 
Hivi mmiliki halali wa hii article ni nani? Maana kuna mwanajf nae kaeleza hivihivi kama vile ni yake ila jamaa fulani akamwambia ameikopi fb kutoka kwa xxx sijui. We nae unasema ni ya Malisa.

Hoja nzuri sana ila mmiliki halisi wa makala sijamjua bado na ningependa nimjue.
 
Mkuu apo mwisho umenifrahisha Sana🤣🤣 anyway najua ni umeka Kama msisitizo. Hoja yako nzuri pia
 
Katika vijana makini wachambuzi na wenye uelewa mkubwa ,basi Malisa GJ ni namba 1.

Nimesoma hii artcle yake juu ya Tanzanite, hadi nimetamani vijana kama hawa wawe msaada kwenye kuweka mikakati ya Taifa hili.

Ivi huyu Kijana ni mbongo kweli?

Kwa kweli sijawahi mwona ila inaonekana ni bonge la genius...
Ushauri mzuri Sana mkuu, Ila alikomalizia tayari kaweka utani tena
 
Kituo cha uchunguzi wa anga za juu cha kimarekani kiitwacho NASA kina kituo kinachohifadhi mawe na miamba iliyokusanywa kutoka mwezini, mawe hayo pamoja na vifaa vilivyotumika kwenye safari iliyofanikiwa ya kutua kwenye mwezi, ni kivutio cha utalii kwa huko USA.

Utaratibu huo unaweza kuigwa na taasisi za maliasili na utalii kwa lengo la kuongeza mapato badala ya kutegemea sana mlima Kilimanjaro na mbuga za wa wanyama tu.
 
Nauhalika malisa hawezi weka jina lake kama hajaandika.
Hivi mmiliki halali wa hii article ni nani? Maana kuna mwanajf nae kaeleza hivihivi kama vile ni yake ila jamaa fulani akamwambia ameikopi fb kutoka kwa xxx sijui.We nae unasema ni ya Malisa.

Hoja nzuri sana ila mmiliki halisi wa makala sijamjua bado na ningependa nimjue.
 
Hivi mmiliki halali wa hii article ni nani? Maana kuna mwanajf nae kaeleza hivihivi kama vile ni yake ila jamaa fulani akamwambia ameikopi fb kutoka kwa xxx sijui.We nae unasema ni ya Malisa.

Hoja nzuri sana ila mmiliki halisi wa makala sijamjua bado na ningependa nimjue.

Ameiiba kwa Malisa na kui paste huko JF bila hata kumshukuru Malisa kwa kumnukuuu.
 
Serikali hii IMEMDHULUMU huyo jamaa mabilioni mengi sana. 15kg ni sawa na 75,000 carats (1 carat is equal to .0002kg)
Na bei ya carat moja kutokana na daraja la Tanzanite ndiyo hiyo hapo chini.

Tukichukia hata bei ya chini kabisa ya $300 kwa carat moja. Kwa 75,000*$300 angepata $22,500,000 times conversion rate ya 2,300 angestahili kupata shilingi 51.7 billions.

For richly colored AAA Tanzanite, 1ct is approximately worth $300-$425 per carat. 2ct sizes reach $450-$650 per carat. 3 carats and up will reach $650-$750 per carat. The changes taking place in Tanzania makes tanzanite a very good investment stone.

Katika vijana makini wachambuzi na wenye uelewa mkubwa ,basi Malisa GJ ni namba 1.

Nimesoma hii artcle yake juu ya Tanzanite, hadi nimetamani vijana kama hawa wawe msaada kwenye kuweka mikakati ya Taifa hili.

Ivi huyu Kijana ni mbongo kweli?

Kwa kweli sijawahi mwona ila inaonekana ni bonge la genius.

Na #Malisa_GJ
----
Saniniu Laizer mchimbaji mdogo wa madini huko Mererani ameamka Bilionea baada ya kupata mawe mawili ya Tanzanite moja lenye uzito wa 9.2KGs na jingine 5.8KGs yenye thamani ya TZS 7.8 Bilioni.

Watu wengi wanajadili kuhusu Tanzania kumpata Bilionea mpya. Ni jambo zuri lakini kuna jambo jingine ambalo halijadiliwi. Na pengine ni la msingi zaidi kuliko Ubilionea wa Laizer.

Hii Tanzanite ya 9.3KGs inaweza kuwa ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana duniani. Hii ndio "angle"ya habari, ambayo inaweza ikabreak (as breaking news) ikatoa day 2 story na ikatengenezewa developing story hata kwa mwezi mzima.

Kabla ya Laizer kuushangaza ulimwengu kwa kuchimbua ardhi na kupata madini haya makubwa kabisa, Tanzanite kubwa zaidi duniani ilikua na uzito wa 3.3KGs na 16,839 carat. Hii ilichimbwa na kampuni ya TanzaniteOne mwaka 2005.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.mining.com Tanzanite hiyo yenye uzito wa 3.3KGs ipo Thailand katika mji wa Bangkok. Wathai wameamua kuifanya fursa ya utalii. Wanatangazia dunia kwamba "karibu Thailand uone Tanzanite kubwa zaidi". Na watu wanasafiri kila pembe ya dunia kwenda kuona hicho kinachoitwa Tanzanite kubwa zaidi na kupiga nayo picha. Utalii wa aina yake.

Kwa kufanya hivyo Thailand iliweza kurudisha fedha ilizotumia kununua Tanzanite hiyo ndani ya miaka minne tu. Na kuanzia 2010 wanapata faida (super normal profit). Mradi huo umeiingizia Thailand pesa nyingi sana na kutoa ajira kwa watu wengi.

Sasa ni wakati wa kibao kugeuka. Na sisi tutengeneze kituo tuweke haya mawe ya Laizer na tuiambie dunia kuwa Tanzanite kubwa zaidi ipo Tanzania na si Thailand tena. Watu waje washangae hayo mawe wapige nayo picha watulipe 'dollars" wakamalizie picknick Serengeti. Wakitaka kumuona na mchimbaji ruksa.

Hii itatulipa zaidi kuliko kuyauza haya mawe kama tulivyofanya 2005. Pia itafungua fursa mpya ya utalii wa madini ambayo hatujawahi kuwa nayo. Tuige kwa Wathai lakini tufanye kwa ubora kuliko wao (ujasusi wa kiuchumi).
_
Kama watu waliweza kusafiri kutoka Marekani, China, UK etc kwenda kushangaa Tanzanite ya 3KGs kule Bangkok, sisi tukisema tunayo ya 9KGs hata shetani si anaweza kuja kushangaa kidogo akapate cha kusimulia kuzimu?
 
Anafaa kuwa mwenyekiti wa CDM
Bado ana njaa atanunulika.

Yafaa awe na pesa au awe ameshaumizwa Sana yaani kujengewa usugu Kama Mdude.
Mtu yeyeto aliyeumizwa na shetani katu hawezi msujudia shetani.
 
Back
Top Bottom