Umepambanua uhuru wako vyema
jambo ambalo ni zuri na ni haki yako,
lkn nimemaizi ya kwamba moyo wako una vidonda vikubwa sana na regime hii.....
but there is nothing you can do....
Mimi naongelea principles tu, naisema regime ya Magufuli kama ninavyoisema regime ya Trump.
Kwa fact. Si kwa vidonda vya tumbo. Tumbo langu halijapata vidonda kwa Scotch Whisky, double double single malt from the Scottish Highlands. Haliwezi kupata vidonda kutokana na siasa, not for the foreseeable future.
Sasa, mtu mwenye kuelewa principles ataelewa kwamba sababu zangu za kuisema regime ya Magufuli ni za kutoka kwenye first principles.
Ndiyo maana naweza kumsema Magufuli, licha ya Magufuli kuipa familia yangu nyumba ya mamilioni ya dola Oysterbay.
Sina sababu ya kumchukia Magufuli.
Magufuli alikuwa rafiki wa Mzee wangu kabla ya kuwa rais.
Yani Mkapa akiharibu, wakati huo Magufuli Waziri, na kafungwa kwa kanuni za "collective responsibility" kusema, Mzee wangu akimpaka Mkapa, kwa maamuzi mabovu ya kuuza mashirika ya umma, kesho yake mtu wa kwanza kumpigia simu Mzee wangu ni Magufuli.
Magufuli akimpongeza na kumwambia mzee wangu "maneno yako uliyosema jana wengi tulitaka kusema, lakini tumeogopa kwa kuwa tupo serikalini".
Sasa mimi ninavyomuongelea Magufuli si kwa kumsoma kwenye magazeti.
Nikimsema vibaya, si kwa chuki.
Ni kwa sababu najua anaweza kuongoza vizuri zaidi ya anavyoongoza sasa.
I am disappointed. Magufuli could do much better than this.
Sasa utaniambia vipi habari za kuwachukia hawa watu ambao nawajua at a personal level? Hawa ni wazee wangu wote. Watu ambao nawajua na wao wananijua.
The only reason I don't tell you more personal stories about Mkapa, Magufuli and Mufuruki is because I respect privacy, mine, theirs, yours.
Nikisema ukweli wangu utasemaje nasema kwa sababu ya chuki?
Leo nimetoka kusoma article ya New York Times Maureen Dowd kaandika kuhusu chuki, inatokana na maneno ya Kikatoliki ya kukataa chuki aliyoyatoa Speaker Pelosi.
Miss Dowd kasema kwamba kila alivyokuwa akiwachana wanasiasa, kwake ilikuwa Rais Bush, watu wenye akiki ndogo walimsimanga kwa kumuuliza "kwa nini unawachukia hawa wanasiasa?".
Akaona swali hili ni censorship tu.
The New York Times articke is here, if you can read the language at all.
Habari ya chuki ni kumwambia mtu kwamba hatakiwi kukosoa, akikosoa sababu pekee ni chuki tu.
Wewe unawezaje kusema mimi nina chuki na mtu aliyeipa familia yangu nyumba ambayo ilikadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni tatu hapo Oysterbay Dar es salaam?
Mtu kama huyo, kama mimi naendeshwa na chuki tu, naanzaje kumchukia?
Huyo marehemu Ali Mufuruki kafanya biashara kubwa sana na familia yangu Tanzania zilizopitishwa na Magufuli.
Sasa wewe unaweza kuniambia vipi kwamba mimi namchukia Magufuli?
Mimi nampenda sana Magufuli.
Na kwa sababu nampenda, nataka afanye vizuri zaidi. Sipo katika praise team na "Yes men" team.
Namkosoa.
Wewe unataka kukana kwamba Mufuruki hajailalamikia serikali ya Magufuki kuwa na ukiritimba katika kukusanya kodi? Mufuruki hajawahi kulalamika magari yake yalivyokamatwa kijinga kama vile yeye ni mtu asiyelipa kodi kipuuzi Tanzania?
Lets talk facts, not just vague emotions.
Ningekuwa na moyo mdogo, ningekuwa sehemu ya praise team sasa hivi. Ningeshindwa kumchana Magufuki kwa shavu aliloipa famikia yangu.
Lakini mimi naangalia mbali zaidi.
Na inawezekana kama wewe unaangalia karibu tu, kuelewana mimi na wewe ikawa vigumu.