TANZIA: Aliyekuwa Mume wa Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia

TANZIA: Aliyekuwa Mume wa Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia

Aliyekuwa mume wa zamani wa Irene Uwoya ,Hamad Ndikumana Kataut ambaye pia alikuwa kocha msaidizi wa Rayon Sports amekutwa amefariki dunia ingawaje mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijawekwa bayana kwa kuwa hata jana alishiriki vizuri mazoezi na alikuwa bukheri wa afya.

Mwili wake kwa sasa umehifadhiwa mochwari ya Rwampala huku taratibu nyingine za mazishi zikiendelea kufanyika

Screenshot_2017-11-15-08-39-57.jpg
 
Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia. Alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda. Uongozi wa timu hiyo umesema jana Katauti alifanya mazoezi na wachezaji wake akiwa buheri wa afya. Mwili wake umekutwa nyumbani kwake mjini Kigali akiwa amefariki dunia. Haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajafanya ajali.

Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake kwani miili ya waislamu haihifadhiwi katika monchwari za kawaida kwa mujibu wa imani zao.

Mungu ampe malazi mema peponi.
Sorry huyu ndo ndiku wa uwoya?
 
Itakua cardiac arrest tu..alikua anahangaika sana recently huko instagram na inaelekea aliumia mnoo kuhusu the so called ndoa ya dogo janja..si kwa caption zile..
Wanamichezo wako vulnerable to cardiac arrest kwa sababu ya kudhoofika kwa misuli ya moyo kutokana na moyo kufanya kazi sana.. Mara nyingi heart attack au blood pressure ndo huendana na stress ingawaje ni nadra sana kwa Wanamichezo kufa kwa blood pressure/heart attack kwa sababu ya stress isipokuwa tu kuwe kuna tatizo la moyo limesabisha hivo
 
Back
Top Bottom