Pamoja na yote hayo, Jumbe nae alikuwa mnafiki kwenye Suala hili la Muungano,
Kwanza, Karume kabla ya Kifo chake, alishaona mapungufu makubwa ya Muungano huu na alianza kufikiria kutoka ndani ya muungano au kubadirisha mfumo wa Muungano,
baada ya Kifo chake (Karume), Abdul Jumbe akachukua Kijiti, lakini akaua kabisa hoja za Karume za kurudi kwenye serikali tatu au shirikisho,
Abdul jumbe alifikia mpaka hatua ya kukubali kuunganisha vyama ASP-TANU kuwa CCM, kwa makubaliano ya kutofuta dhana nzima ya Mapinduzi hivyo chama kipya kiwe na neno Mapinduzi, hiyo yote inaonyesha dalili kuwa Jumbe, hakuwa muhumini halisi wa serikali tatu,
kutokana na kuhuisha hoja za Karume zilizokuwa zinauquestion Muungano, Pamoja na kujenga nyumba yake bara (Kigamboni) Jumbe akakosa mvuto kwa wana Zanzibar na akaonekana si mwenzao, na ili kurudisha trust yake alibidi aanze kutafuta uungwaji mkono tena na alianza kampeni zake kupitia nyumba za ibada.
Kwa sasa Jumbe ataonekana ni muungwa na mtetea Muungano lakini kwa uhakika toka 1972-1984 hakuwa hivyo
Cc:
Pasco ,
Malafyale