Kama kawaida yetu Watanzania, hatuna busara ya kutaka kujua ukweli, bali akili zetu zinatumiwa na wachache, pia tuna Tabia ya Chuki na Fitina. Japokuwa siungi mkono namna serekali ya chama changu kinavyo tekeleza hili janga la Covid19, Lakini tunahitaji kuwa watu makini.
1. Je, tunajua marehemu Mzee wetu Mahiga amefariki kwa Corona au maradhi mengine na siku yake imefika? Hakuna hata Mchangiaji mmoja aliyelizungumzia hili, kwani hatuna uhakika na kama kawaida tunadandia pickup nyuma na tunajifanya tumechukua usukani wa gari.
2. Tuna Tabia za kuufanya uongo wetu kuwa ukweli, Wakati kama huu vifo vya haya maradhi ni mengi, lakini pia vifo vya maradhi mengine na ajali pia zinatokea. lakini kila kifo kitokeacho utasikia tukisem ni Corona, bila hata kupepesa macho.
Kwenye hichi kifo cha Mahiga,Ninawashauri tusubiri tupate ukweli wa kifo chake, kwani hata kama Serekali watataka kuuficha, ukweli haufichiki.