TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

RIP DR. Mahiga,
Ulikuwa humble sana, tutakukumbuka daima.

Kipindi hiki cha Bunge ulikuwa ndo wakati mzuri wa kuwa kitu kimoja kujadili mambo ya msingi kuhusu ugonjwa wa corona, lakini kwa bahati mbaya sana wabunge wa ccm wamefanya Bunge kuwa la mipasho kupasha ushauri mbalimbali mzuri unaotolewa na wabunge wa upinzani.
 
Kama kawaida yetu Watanzania, hatuna busara ya kutaka kujua ukweli, bali akili zetu zinatumiwa na wachache, pia tuna Tabia ya Chuki na Fitina. Japokuwa siungi mkono namna serekali ya chama changu kinavyo tekeleza hili janga la Covid19, Lakini tunahitaji kuwa watu makini.

1. Je, tunajua marehemu Mzee wetu Mahiga amefariki kwa Corona au maradhi mengine na siku yake imefika? Hakuna hata Mchangiaji mmoja aliyelizungumzia hili, kwani hatuna uhakika na kama kawaida tunadandia pickup nyuma na tunajifanya tumechukua usukani wa gari.

2. Tuna Tabia za kuufanya uongo wetu kuwa ukweli, Wakati kama huu vifo vya haya maradhi ni mengi, lakini pia vifo vya maradhi mengine na ajali pia zinatokea. lakini kila kifo kitokeacho utasikia tukisem ni Corona, bila hata kupepesa macho.

Kwenye hichi kifo cha Mahiga,Ninawashauri tusubiri tupate ukweli wa kifo chake, kwani hata kama Serekali watataka kuuficha, ukweli haufichiki.
 
Mkirindi,
Nikupongeze tu kwa kujua kuwa serikali inafichaficha vitu hasa kwenye hili janga LA corona.. Asante sana hayo mengine yachukuwe mwenywe
 
RIP Mahiga.
Serikali chukueni hatua tuko katika kipindi kigumu,msidharau gonjwa tulilonalo na kuhadaa wananchi kwa kivuli cha kufanya kazi na kukusanya kodi ambayo haina maana kama nguvu kazi inapotea.
 
Naomba mtuwekee CV ya Marehemu hapa, hata sie vijana tupate kumjua huyp mzee wetu mpambanaji
 
Kichuguu,
Asante sana kwa pole; nadhani inakua na tabia tofauti tofauti..ninazo case tatu tofauti ambazo watu wamebanwa na homa kali..mafua makali..kikoozi kikali na kavu mwili kuchoka na kuanza kuharisha yaani ndani ya nusu saa zote hizi zinatokea.

Kibaya zaidi mnapoanza huduma ya kwanza ndo shida ya kupumua inaanzia hapo..nakwambia ndugu kabla ya saa kutimia mnaweza kumpoteza ndugu yenu na hizi nyakati za mvua ndiyo balaa kabisa.

Unajiuliza flani si alikua mzima kabisa? kwakweli bado tafiti zinatakiwa kuhusu hili gonjwa.

Mzee wetu lala salama japo ulikua sehumu ya uzembe wa serikali.
 
Shetani atuma salamu!
Mimi sitatangazwa kwa amri ya magufuli, lakini nikiwa kaburini nitatoa amri kifo cha magufuli kitangazwe na kila mtu ajue kuwa NONDO MLA WATU KALAMBA MCHANGA.
(sio kama napenda kuandika hivi bali naomboleza kimila)
 
Kwa kifo cha Balozi Mahiga kwanza ninampa pole Rais wetu kwa kuondokewa na mtu muhimu katika uongozi wake. Ninawapa pole Watanzania wote jamani kumpara mtu kama Balozi Mahiga itatuchukua muda mrefu sana. Famila ya Dr Mahiga poleni sana, huu ni msiba wenu lakini ni msiba pia wa Taifa.
 
Watoa matusi haraka haraka ni watu wenye akili ndogo sana hasa wanapokuwa wanafanya hivyo kwa hisia bila kuwa na taarifa kamili. Kwa maoni yako sasa wewe unaamini kuwa kila kifo kinachotokea Tanzania ni kwa sababu ya korona na ni makosa ya serikali.
Prove them wrong.
 
Kwa kifo cha Balozi Mahiga kwanza ninampa pole Rais wetu kwa kuondokewa na mtu muhimu katika uongozi wake. Ninawapa pole Watanzania wote jamani kumpara mtu kama Balozi Mahiga itatuchukua muda mrefu sana. Famila ya Dr Mahiga poleni sana, huu ni msiba wenu lakini ni msiba pia wa Taifa.
Kwani MEMBE unamuweka kundi gani?

Live Long Bernad Camilius Membe.
 
Back
Top Bottom