TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

R.I.P Mahiga

Ama kwa Hakika Taifa limepoteza mtu makini na mwerevu.


Sasa ni wakati kwa Serikali itambue kwamba viongozi wa Juu ambao tunaamini wao ndio wapo katika nafasi nzuri ya kupata matibabu na kinga wanapopoteza maisha wakati huu huku Serikali kutoonesha nia ya dhati kupambana na hili Janga basi huu ni Ujumbe tosha kwa Dunia kwamba Mamlaka zimeshindwa kulinda watu wake na hivyo Nchi haipo salama sasa hivi na siku zijazo hata majanga mengine yatakapotokea.

Swala si uwezo wa Matibabu!
Yeyote mwenye mgogoro wa Afya , janga hili halimuachi salama!
 
kama huyo jamaa amenyosha goti basi yule jamaa yake kichwa maji hawezi kupona hata ajifiche wapi au ajifukize vipi.

Sent from my SM-G975F using Tapatalk
 
Kwani umelazimishwa kutoka kwako wewe si jilock down mwenyewe asee
Sasa mbona huyo magufuli wenu amejilokdown huko chato halafu anawaambia wananchi waendelee kujichanganya kuchapa kazi? Huyu so anataka kutuua huyu kiongozi gani sasa huyu.
 
nenda mahiga

ulishindwa kumshauri jiwe
Unajua hawa Wa kubwa linapokuja swala la kulinda RAIA wao hujitoa akili kuwa hawataguzwa Mimi siyo nabii lakini kwa hii hali niliyoiona masokoni kuhusu mkusanyiko hata kama serikali itaficha sana taarifa kweli kipindi hiki tutazikana sana hii tabia yakuogopa njaa kuliko maradhi ni upofu Wa hali ya juu kabisa.

Bora uchumi uporomoke ila RAIA tupone nimempoteza dada yangu na Rafiki zangu wawili huu ukimya ni Wa kishetani siyo wakimungu corana. Ni pandemic siyo tatizo LA kuchekwa bora kila kitu kiwekwe wazi tupate wakutusaidia hata chaina ilisaidiwa hata italy imesaidiwa je sis I masikini tunaogopa mini?
 
Rais Magufuli anatangaza kifo cha Waziri wake wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga aliyefariki leo alfajiri Mei 01, Jijini Dodoma

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema Waziri huyo aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake na alifikishwa hospitalini akiwa tayari ameshafariki dunia

View attachment 1436100

WASIFU:

View attachment 1436154


Dk Augustine Mahiga alizaliwa Agosti 28, 1945 huko Tosamanganga, Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa (atatimiza miaka 70 ifikapo Agosti mwaka huu). Amesoma elimu ya msingi katika shule za Serikali enzi ya mkoloni na alihitimu darasa la VIII muda mfupi baada ya uhuru. Safari ya elimu ya Dk Mahiga ilikuwa ya umaskini uliopitiliza, alishindwa kuendelea na elimu ya sekondari kwa kutokuwa na fedha za kulipia mashuka na mablanketi hadi aliposaidiwa na msamaria mwema kutoka Shirika la Kennedy wakati huo.

Aliendelea na masomo ya sekondari hapahapa nchini na mwaka 1968, alijiunga katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Dar es Salaam na kuhitimu Shahada ya Sanaa akibobea kwenye elimu mwaka 1971.

Mwaka huohuo, Dk Mahiga alipata ufadhili na kuendelea na masomo ya juu nchini Canada katika Chuo Kikuu cha Toronto ambako alihitimu Shahada ya Uzamili. Aliendelea na masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika chuo hichohicho akijikita katika Uhusiano wa Kimataifa na kuhitimu mwaka 1975.

Mwaka huohuo 1975 (akiwa na miaka 30), Dk Mahiga alirejea nchini akiwa daktari wa falsafa kitaaluma na alipangiwa kazi ya kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mhadhiri katika Idara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kikanda. Alifanya kazi hiyo hadi mwaka 1977 alipohamishiwa katika Ofisi ya Rais kuwa Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo na alidumu hapo akifanya kazi pamoja na Mwalimu Julius Nyerere hadi mwaka 1980.

Kati ya mwaka 1980 hadi 1983, Dk Mahiga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Nafasi hii aliitumikia kwa weledi mkubwa katika historia ya watu waliowahi kuitumikia, aliweza kuifahamu nchi vizuri na mifumo yake kwa mtizamo wa ndani na nje.

Mwaka 1989 hadi 1992, aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Kimataifa akifanyia kazi Geneva, Uswisi na mwaka 1992 hadi 1994, Balozi Mahiga aliteuliwa kuwa Kiongozi (Mwakilishi) wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) mjini Monrovia, Liberia na huu ndiyo wakati aliponusurika kuuawa na Majeshi ya Rais Charles Taylor, kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Kuna wakati akiwa katikati ya operesheni ya wakimbizi hapo Monrovia, Serikali ya Tanzania ilimteua kuwa Balozi na kumuongezea jukumu jingine zito.

Mwaka 1994 -1998, Balozi Mahiga alihudumu akiwa Mratibu na Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni ya Dharura ya Ukanda wa Maziwa Makuu akifanyia kazi hiyo kutokea Geneva, Uswisi na kati ya mwaka 1998 - 2002 aliteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu (Mwakilishi) wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) huko mjini Delhi India kabla ya kuteuliwa tena kuwa mwakilishi wa shirika hilo katika nchi za Italia, Malta na Jamhuri ya San Marino kati ya mwaka 2002 - 2003.

Balozi Mahiga amepata pia kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2010 na alishiriki kikamilifu katika mipango ya kimataifa pamoja na kusimamia mazungumzo ya kuanzishwa kwa Kamisheni ya Ujenzi wa Amani (mwaka 2005). Pia kushiriki kwenye masuala ya maingiliano ya serikali mbalimbali na makundi yanayofanya kazi zisizo rasmi, maendeleo, amani, usalama na ujenzi wa ushirikiano wa uhakika kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Balozi Mahiga alirejesha heshima ya Tanzania hadi kuwa mojawapo ya nchi zilizounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi yetu ilipopata heshima hiyo, yeye aliteuliwa kuwa mkuu wa ujumbe wa Tanzania katika Baraza hilo, hii ilikuwa ni mwaka 2005.

Mwaka 2015 mwezi Disemba, Rais Magufuli alimteua Balozi Mahiga kuwa Mbunge na baadae kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Naibu wake akiwa Dr Suzan Kolimba.

Machi 03, 2019 Rais Magufuli alimhamisha Wizara na kumteua kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, nafasi aliyoitumikia hadi mauti yanamkuta.


MACHACHE KUHUSU DKT. MAHIGA: Augustine Mahiga: Mwanadiplomasi anayeheshimiwa kuliko wote Tanzania - JamiiForums
What a Roving Journalist!
....kazaliwa mwaka 1945 atatimiza miaka 70 mwezi wa nane 2020!
Inawezekana ni chapchap ya kukimnilia kuwa mtu wa kwanza kutoa taarifa.
 
Dah alikuwa mtu poa sana yan hana majivuno wala kejeli kama mawazir weng na wabunge wa ccm walivyo nakumbuka hata mh sugu alimtabiria kama kungekua na tume huru ya uchaguz ni mmoja wa wabunge wa ccm ambao wangerejea bungeni....... RIP... bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe...wote ni njia yetu.....see you again baloz Mahiga

Its not over until its over...[emoji769]
 
Back
Top Bottom