TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

Lakini posho wamwachie nani? Ndugai anapoona wenzake wanakufa anafkiri posho zao zinaenda kwa waliobaki......IT IS ALL ABOUT POSHO.
Wnajadili bajeti ambayo ni very irerevant compared to the current situation.
Basi wawapime wabunge wote,,sio kuwapima joto,wapimwe,wenye vimelea waanze dose na watengwe
 
Basi wawapime wabunge wote,,sio kuwapima joto,wapimwe,wenye vimelea waanze dose na watengwe
Amna acha waendelee kwanza....Huu ushauri wameutoa wabunge wa upinzani km mara nne lkn ndugai anasikiliza kwanza jiwe kasemaje asipomruhusu hawezi kufanya chochote.....

TUNDU LISSU ANGETUVUSHA VIZURI SANA WKT KM HUU
 
REST IN PEACE.SIO KILA KIFO NI CORONA ,UKICHEKI UMRI NAO NI FACTOR NA PIA KWA UMRI HUO MAGONJWA NYEMELEZI NI MENGI KWA KWAKUWA KINGA IPO CHINI.
Basi nenda ukaage mwili mwili wake na uuguse tuone kama utaendelea kuandika humu tena.
 
Kweli vijana pia tunakufa, na sikua na lengo la kumaanisha kua vijana hawafi ila nawaza tu busara tutapata wapi wakati wazee wote wenye hekima zao wanaondoka, Kwikima, Augostino, Mahiga......
Busara ni zao la ufahamu.
Wazee wenye ufahamu wenye kaliba ya mzee wa chato ni hasara.
 
View attachment 1436171

Rais Magufuli anatangaza kifo cha Waziri wake wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga aliyefariki leo alfajiri Mei 01, Jijini Dodoma

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema Waziri huyo aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake na alifikishwa hospitalini akiwa tayari ameshafariki dunia

View attachment 1436100

WASIFU:

View attachment 1436154


Dk Augustine Mahiga alizaliwa Agosti 28, 1945 huko Tosamanganga, Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa (atatimiza miaka 70 ifikapo Agosti mwaka huu). Amesoma elimu ya msingi katika shule za Serikali enzi ya mkoloni na alihitimu darasa la VIII muda mfupi baada ya uhuru. Safari ya elimu ya Dk Mahiga ilikuwa ya umaskini uliopitiliza, alishindwa kuendelea na elimu ya sekondari kwa kutokuwa na fedha za kulipia mashuka na mablanketi hadi aliposaidiwa na msamaria mwema kutoka Shirika la Kennedy wakati huo.

Aliendelea na masomo ya sekondari hapahapa nchini na mwaka 1968, alijiunga katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Dar es Salaam na kuhitimu Shahada ya Sanaa akibobea kwenye elimu mwaka 1971.

Mwaka huohuo, Dk Mahiga alipata ufadhili na kuendelea na masomo ya juu nchini Canada katika Chuo Kikuu cha Toronto ambako alihitimu Shahada ya Uzamili. Aliendelea na masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika chuo hichohicho akijikita katika Uhusiano wa Kimataifa na kuhitimu mwaka 1975.

Mwaka huohuo 1975 (akiwa na miaka 30), Dk Mahiga alirejea nchini akiwa daktari wa falsafa kitaaluma na alipangiwa kazi ya kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mhadhiri katika Idara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kikanda. Alifanya kazi hiyo hadi mwaka 1977 alipohamishiwa katika Ofisi ya Rais kuwa Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo na alidumu hapo akifanya kazi pamoja na Mwalimu Julius Nyerere hadi mwaka 1980.

Kati ya mwaka 1980 hadi 1983, Dk Mahiga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Nafasi hii aliitumikia kwa weledi mkubwa katika historia ya watu waliowahi kuitumikia, aliweza kuifahamu nchi vizuri na mifumo yake kwa mtizamo wa ndani na nje.

Mwaka 1989 hadi 1992, aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Kimataifa akifanyia kazi Geneva, Uswisi na mwaka 1992 hadi 1994, Balozi Mahiga aliteuliwa kuwa Kiongozi (Mwakilishi) wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) mjini Monrovia, Liberia na huu ndiyo wakati aliponusurika kuuawa na Majeshi ya Rais Charles Taylor, kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Kuna wakati akiwa katikati ya operesheni ya wakimbizi hapo Monrovia, Serikali ya Tanzania ilimteua kuwa Balozi na kumuongezea jukumu jingine zito.

Mwaka 1994 -1998, Balozi Mahiga alihudumu akiwa Mratibu na Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni ya Dharura ya Ukanda wa Maziwa Makuu akifanyia kazi hiyo kutokea Geneva, Uswisi na kati ya mwaka 1998 - 2002 aliteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu (Mwakilishi) wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) huko mjini Delhi India kabla ya kuteuliwa tena kuwa mwakilishi wa shirika hilo katika nchi za Italia, Malta na Jamhuri ya San Marino kati ya mwaka 2002 - 2003.

Balozi Mahiga amepata pia kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2010 na alishiriki kikamilifu katika mipango ya kimataifa pamoja na kusimamia mazungumzo ya kuanzishwa kwa Kamisheni ya Ujenzi wa Amani (mwaka 2005). Pia kushiriki kwenye masuala ya maingiliano ya serikali mbalimbali na makundi yanayofanya kazi zisizo rasmi, maendeleo, amani, usalama na ujenzi wa ushirikiano wa uhakika kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Balozi Mahiga alirejesha heshima ya Tanzania hadi kuwa mojawapo ya nchi zilizounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi yetu ilipopata heshima hiyo, yeye aliteuliwa kuwa mkuu wa ujumbe wa Tanzania katika Baraza hilo, hii ilikuwa ni mwaka 2005.

Mwaka 2015 mwezi Disemba, Rais Magufuli alimteua Balozi Mahiga kuwa Mbunge na baadae kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Naibu wake akiwa Dr Suzan Kolimba.

Machi 03, 2019 Rais Magufuli alimhamisha Wizara na kumteua kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, nafasi aliyoitumikia hadi mauti yanamkuta.


MACHACHE KUHUSU DKT. MAHIGA: Augustine Mahiga: Mwanadiplomasi anayeheshimiwa kuliko wote Tanzania - JamiiForums
RIP kiongozi Maiga
Aisee. Apumzike kwa amani mzee.

Mazishi yake yatakua ya watu 10 tu?

Hii kitu ikipiga juu ndio labda watachukua hatua. Mshikaji kakimbilia kijijini kwao huku wenzake wanateketea. Yule kumuona mjini labda mwezi wa 8.

Uzuri wa hii kitu ndio huo, na vile wakubwa wengi ni wazee na most volnerable and prime suspect ya hii kitu, ikiwaanza wataisha. Labda hii itasababisha tuchukue hatua madhubuti ingawa tumechelewa tayari.
R.I.P kiongozi Maiga
 
Yaani RIP waziri.Poleni familia.Nawaza kuna mahali nilituma ushauri kuwa raisi angezuia mukusanyiko isiyo ya lazima kama kanisani na misikitini ile pasaka ndio outbreak imeanza.Sasa let us swallow our pride now
Saa hizi Hawa asymptomatic ndo wanaeneza kimya kimya,yaani mwizi anafukuzwa kimya kimya ....
 
[Sasa mbona huyo magufuli wenu amejilokdown huko chato halafu anawaambia wananchi waendelee kujichanganya kuchapa kazi? Huyu so anataka kutuua huyu kiongozi gani sasa huyu]

Ji-lockdown wewe mwenyewe na wapendwa wako. Huu ni wakati wa Yarabi nafsi...
 
Nimeshajua kwa nini kamanda kajificha chocho kumbe amenusa harufu mbaya ya panya aliyeoza magogoni! Duh, hewa imechafuka jamani. Sasa kamanda mbona ananguruma wakati yuko chobingo, yaani yeye anashuhudia tu jumba bovu linavyowaporomokea wenzie. Ila hiyo harufu haishi leo kwa jinsi tunavyokwenda, ajue hiyo.
 
R.I.P Baba .Imeniuma sana.Magufuli anawatoa wenzake kafara kwa Covid 19. YEYE KATULIA CHATO. Dr Mchembe nakulaumu sana kwa nini ulimshauri Rais aende Chato ?Angebaki Dodoma akajua jinsi" kaugonjwa kadogo " Kangemplekesha.
 
Kwa kweli hali inatisha. Poleni sana Wanafamilia.
 
Back
Top Bottom