TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

AISEE HALI NI TETE TUNAKWISHA JAPO WANASEMA HIVI VIFO SIO VYA CORONA ILA KWA NINI IWE WAKATI HUU WA CORONA NDO VIFO VINAZIDI?!
.... vile ndo tumekuwa na mda makini zaid kuskiliza vifo na kuripoti vifo...imechukua nafasi ya betting daily...vifo vilikuepo na vitazid kuepo ata bila covid -19
 
Ni kitendo cha usalamawa Taifa na jeshi kumsogeza pembeni Magufuli kwa sasa ili maamuzi yafanyike ya maana kuokoa maisha ya Watanzania wakimuachia huyu jamaa aendelee tutaangamia nna wasiwasi kama ni mtanzania mwenzetu unaeza kuta kinachoendelea anasherekea.
 
Party caucus ya chama fulani itakuwa matatani,pia ministers na wabunge
 
Nimekuwa nikishuhudia watu wakiwa na hisia tofauti tofauti pindi itokeapo misiba ya viongozi wa kisiasa hapa nchini, watu huhuzunika, wengine huchukulia poa na wengine hufurahia kabisa na kusema bora ameenda alikuwa mtu mbaya sana.

Lakini Hali imekuwa tofauti kwa msiba wa Balozi Mahiga, watu wote ninaowafahamu Mimi ambao walikuwa wanamfahamu pia Balozi Mahiga wameguswa, wanahuzunika na kuomboleza msiba huu wa mwanadiplomasia nguli tofauti kabisa inavyokuwa kwenye misiba ya wanasiasa wengine.

Bila shaka wema na siasa za kistaarabu za Mahiga ndo chanzo cha haya yote. Tujitahidi kuwa watu wema katika jamii zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichobaki sasa ni kila mmoja kuchukua tahadhari binafsi ili kujikinga dhidi ya Covid-19 na siyo kutegemea serikali peke yake ikusaidie kuchukua tahadhari.

Hii ni vita halisi, na kila mmoja wakati huu anaishiriki.

Hii serikali imeshalemewa tayari, tahadhari walishindwa kuchukua tangu awali hivyo saiv watu wanapukutika tuu.
Umenena mkuu, kila mtu apambane na hali yake, japo ni kweli tumechelewa sana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee! Bunge liwekwe karantine, hakuna namna mdudu yupo mule

Apumzike mahali panapo stahili Steven mahiga
 
Waziri mpya akiteuliwa ataapishiwa wapi...... Chato!? Naona muda wa kurudi mjini umewadia. RIP Mzee Mahiga.
 
Tuliwaambia mjilinde mkasema muombe. Sasa nchi pekee duniani ambayo mmekaa mkafunga kuomba ndiyo imepoteza viongozi wengi ndani ya muda mfupi.

Bado tu mnahisi huyu mungu wenu wa wakoloni yupo? 😂 endeleeni kuomba tena mzidishe vizuri sa hivi nendeni makanisani muongeze bidii nyambaf ndiyo kwanza trailer inaanza.

Ningekaa kuwaonea huruma watu wanaojilinda alafu hii kitu ikawasumbua ila watu mnaojifanya wajuaji hata huruma siwaonei, nyambaf kabisa. Hii kitu inaua balaa wengi wenu afya mgogoro endeleeni kuchekacheka
 
Waterloo! Ume-panic ndugu yangu, jitulize kidogo maana unakoelekea, utakufuru! Hili ni janga, limetukumba wote, tupo hatarini, lakini tuki-panic hatutajenga chochote! Can I repeat? Tujitulize, tutafakari, alafu tuchukue hatua staiki, hata kama ni comment hapa!
Huu siwakati wakujishauri hatua zakuchukua zinajulikana. santesandy
 
Uhai ndio kila kitu hivyo vyeo mnakufa mnaviacha, kama kiongozi mkubwa hataki kufuata ushauri wa wataalamu ni kumwachia serikali aongoze peke yake.
Hili ni la muhimu lakuzingatia.
 
Halafu anasema endeleeni kuchapa kazi. Hao wabunge huko bungeni wanafanya nini? Watu watakwisha kwa tamaa ya posho badala ya kuangalia Kwanza afya zao.
Watu 60M watakwisha?

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Watoa matusi haraka haraka ni watu wenye akili ndogo sana hasa wanapokuwa wanafanya hivyo kwa hisia bila kuwa na taarifa kamili. Kwa maoni yako sasa wewe unaamini kuwa kila kifo kinachotokea Tanzania ni kwa sababu ya korona na ni makosa ya serikali.
Ukikubali kuelewa utaelewa kama utaki basi ulazimishwi; sehemu kama mkoa Mara..Katavi na miji midogo midogo zimepata maambukizi ya Corona kwa uzembe wa serikali. Ugonjwa ulichelewa kufika Tanzania na sisi kama serikali pia tukawa tunachelewa kufanya monitoring ya movement ya watu.

Ikafikia hatua adi nchi nzima imetapakaa ugonjwa; nani kasema vifo vyote vimetokana na Corona? ila ya Waziri usibishe imetokana na Corona..mimi ni mwana karibu.
 
Back
Top Bottom