TANZIA: Bi. Asha B. Makame afariki dunia

TANZIA: Bi. Asha B. Makame afariki dunia

View attachment 318027

TANZIA: Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha B. Makame afariki dunia huko Dubai akitokea nchini India kutibiwa.

Bi. Asha Makame alipata umaarufu kwenye Bunge la Katiba kutokana na michango yake wakati mijadala.
mungu akuweke mahala pema mama jasiri wa kiafrika. tutakukumbuka kwa kutetea maslahi ya wanyonge zanzibar.
 
Kasaidia Maalim kunyimwa nchi. Mungu amuweke panapomstahili.
 
Ametangulia akawaacha "Machotara hizbu"

Aliwahi kusema hawatakabidhi Zanzibar kwa vijikaratasi vya kura!! Anarudi Zanzibar amefumba macho mpoleeee!!!
 
RIP mama.

Itakuwa vyema zaidi tukiepuka kumtwisha marehemu mzigo wote kwa vile tu yeye alikuwa jasiri wa kuropoka (kuupa sauti hadharani) msimamo wa wenye nchi kuhusu utekelezaji halisi wa demokrasia nchini.

Yeye kama kawaida ya "mashabiki/wakereketwa" alikuwa hmv tu - pengine hata asiyeelewa vyema uzito, athari na matokeo ya anachokisema.
 
Siku zote nimekuwa nikirejea katika rai aliyoitoa siku moja mhe Zitto Kabwe kwamba wanasiasa tuwe na akiba ya "maneno".Ni jambo la kawaida nchini kwetu katika majukwaa ya siasa kushuhudia wanasiasa hususani wa chama tawala kuzungumza maneno ya KUFURU na kusahau kuwa hii dunia ni ya mungu na tunapita tu.

R.I.P msema hovyo wa Zanzibar
 
View attachment 317991

Aliyewai kuwa Mwakilishi wa bunge maalum la katiba na Waziri wa wanawake na watoto Zanzibar na Makamu wa Jumuiya ya wanawake wa CCM ametangulia mbele ya haki huko Dubai baada ya kurejea matibabu yake huko India.

Mwenyeenzi Mungu amsamehe makosa yake na amlaze mahali pema. Amin
Basi mpeni pole , marehemu alaumiwi lakini huyuuu!!
 
Sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
 
Duniani ulikuwa ukipambana na CUF sasa nenda kapambane na Mungu, halafu Wa Hizbu hawako hivi Huyu ni chotara haswa hata macho yanaonesha, Mungu akusamehe akuweke pahala Pema, Amen
 
Ni huzuni, poleni sana Familia, ndugu, jamaa na marafiki, Wazanzibari na Watanzania wote. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!
 
Mama kafa na mfadhaiko tu zanzibar hakukaliki maana yale maneno yake nadhani alijuta kwa nini alikuwa mjumbe wa bunge la katika, pole kwa wafiwa mama kaotoka kutibiwa India akaenda kupumzika Dubai, Mungu bana mtu unachafua amani kwa kujua kikinuka unasepa nje ya nchi kisa uwezo unao ukijua watakufa masikini watakao jifungia ndani, kumbe kifo hakiepukwi, kaenda na wasiwasi wa kuona ccm inapoteza nchi hata ndio mahaba sasa, si yale ya ukawa kwa Lowasa.
 
kwa yaliyotokea kwenye BMK mimi jamani sina la kusema , namwachia Mungu mwenyewe aamue cha kufanya .
 
Asante kwa taarifa, lakini Kiswahili chako kibovu sana! "ametangulia mbele ya haki huko Dubai", hii nini maana yake! Aliyekwambia Mwenyezi Mungu anaishi Dubai nani? Unataka kusema Dubai ndiko mbele ya haki?? Najua umekosea, jifunze kunyoosha maelezo!
Ubarikiwe!
Comment yako si bure.
 
Jamani Mungu ampumzishe Bi Asha, nilikua nampenda sana huyu Mama
 
Back
Top Bottom