Tanzia:Bosi Wa SafariCom Kenya Amefariki!

Tanzia:Bosi Wa SafariCom Kenya Amefariki!

Jackal

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
9,971
Reaction score
13,608
BREAKING: Safaricom CEO Bob Collymore confirmed dead.

SAFARICOM CEO Bob Collymore dies of cancer at his home in Nairobi; chairman Nicholas Nganga says his condition worsened in recent weeks.
FB_IMG_1561956780978.jpg

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni kubwa zaidi ya mawasialiano ya simu Afrika Mashariki Safaricom, Bob Collymore ameaga dunia, kampuni hiyo imethibitisha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Safaricom, Collymore amefikwa na umauli asubuhi ya leo Jumatatu Juni Mosi 2019 nyumbani kwake jijini Nairobi.

Mwenyekiti wa kampuni hiyo Nicholas Ng'ang'a amesema kuwa afya ya Collymore ilikuwa mbaya majuma ya hivi karibuni.
Collymore, alichukua likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017 na kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu ya saratani.

Alirejea Kenya mwezi Juni mwaka jana, Gazeti la Standard media nchini Kenya limeripoti.

Marehemu ameacha mke na watoto wanne.

Collymore alianza kuongoza gurudumu la Safaricom mwaka 2010 kutoka kwa Michael Joseph ambaye kwa sasa ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo, pia mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege la Kenya Airways.

Mwaka 2017 wanahisa walipiga kura kuongeza mkataba wa Bob Collymore kwa miaka miwili baada ya mkataba wake kuisha.

Mkataba aliokuwa akiufanyia kazi ulikuwa unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mkurugenzi aliyekalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi kwenye historia ya kampuni hiyo.

View attachment 1143558
 
Kumbe unaogopa kufa, mi nilishawahi kunyooshewa a gun at point blank range na wahuni.

Nani asiyeogopa kifo, labda yale mazombi ya kujilipua, duh! Hilo kunyooshewa hicho kidude yaani noma, pole sana maana sipati picha, nimezoea kwenye movie.
 
Back
Top Bottom