Tanzia:Bosi Wa SafariCom Kenya Amefariki!

Tanzia:Bosi Wa SafariCom Kenya Amefariki!

Aya kama hizi huogofya, nifanyeje nisionje mauti...
Nina dawa za kukufanya uishi miaka 206.
BTW R.I.P Robert niliangalia interview yake moja kwenye program ya Churchill alinikosha sana alipo dance nyimbo ya KATIKA.
 
Unaogopa kwa kuwa bado haujafikia hali hiyo, ukiwa uko katika hali ambayo kifo hakikwepeki unakuwa calm ajabu. Hivi huyu boss alikuwa mstahafu au?

Hiyo kweli, kuna sehemu nilisoma kwamba wanyama kama nyumbu wakati wanashambuliwa na simba, huingia kwenye hali ya mshtuko/shock kiasi kwamba huwa hawahisi maumivu wakati wanaliwa wakiwa hai.
Bob alikua mkurungezi wa Safaricom hadi kifo chake.
 
Na vile nilimtazama pale Jeff Koinange Live akicheka cheka na akihave a good time na nilidhani kweli amepona duh kweli hii dunia tunapita tu. Mungu ailaze roho yake pema peponi.
Ni cancer ya nini alikuwa anaumwa
 
Alishakuwa mkenya kabisa ama ataenda kuzikwa kwao Guyana?
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni kubwa zaidi ya mawasialiano ya simu Afrika Mashariki Safaricom, Bob Collymore ameaga dunia, kampuni hiyo imethibitisha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Safaricom, Collymore amefikwa na umauli asubuhi ya leo Jumatatu Juni Mosi 2019 nyumbani kwake jijini Nairobi.

Mwenyekiti wa kampuni hiyo Nicholas Ng'ang'a amesema kuwa afya ya Collymore ilikuwa mbaya majuma ya hivi karibuni.
Collymore, alichukua likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017 na kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu ya saratani.

Alirejea Kenya mwezi Juni mwaka jana, Gazeti la Standard media nchini Kenya limeripoti.

Marehemu ameacha mke na watoto wanne.

Collymore alianza kuongoza gurudumu la Safaricom mwaka 2010 kutoka kwa Michael Joseph ambaye kwa sasa ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo, pia mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege la Kenya Airways.

Mwaka 2017 wanahisa walipiga kura kuongeza mkataba wa Bob Collymore kwa miaka miwili baada ya mkataba wake kuisha.

Mkataba aliokuwa akiufanyia kazi ulikuwa unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mkurugenzi aliyekalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi kwenye historia ya kampuni hiyo.

_107652524_46d0c1ee-f3fa-42f2-b7ca-edd3334f4caf.jpeg
 
Kila nafsi itaonja umauti,Apumzike kwa Amani Bob Collymore.
 
Back
Top Bottom