TANZIA: George Tyson Afariki - Msiba mwingine Tasnia ya Filamu

TANZIA: George Tyson Afariki - Msiba mwingine Tasnia ya Filamu

Bongo movie ndio inazidi kudidimia....

best artist Kanumba ndio alishatutoka....

Sasa ba best Director hatunae ten....

RIP Tyson
 
Tusihuzunike juu ya kifo ila tutafakari tumejiandaa vipi kupokea KIFO!!!
 
Haya magari mnanunua hovyohovyo Japan na kujiendeshea kama pro....mjue yanachinja. Muwe mnaenda proper driving school na myaheshimu magari....yanaua...sawa vijana??..


Out.

Lione hili nalo!


R.I.P Jembe la "Girlfriend"
 
Alikua pia ana direct kipindi cha wanawake live cha joyce kiria, R.I.P George Tyson.
 
mnavyoongea kama vile mlitaka afe lulu,mara jembe,nguli,kichwa n.k.R.I.P TYSON
 
10376930_926363547378064_4238843475968517989_n.jpg

R.I.P Baba Sonia. mia
 
Taarifa nimezpata kutoka Morogoro GEORGE TYSON aliyekuwa mume wa MONALISA amefariki kwenye ajali leo Mwenye tarifa zaidi
 
Taarifa nimezpata kutoka Morogoro GEORGE TYSON aliyekuwa mume wa MONALISA amefariki kwenye ajali leo Mwenye tarifa zaidi

taarifa zipo hapa Jamvini tangu saa sita za usiku,.

Nenda Celebrity Forum utapata kufahamu zaidi!
 
Naona Mchawi ni huyu hapa hizi Tabiri zingine hazifai nafuu hawa watabiri wakapigwa Marufuku maana maneno mengine unapoongea SHETANI nae huwa yupo karibu na kusikia na kuyafanyia kazi.

Mtoto wa Sheikh Yahya Hussein atabiri Jinamizi la Kifo kuendelea kuwatafuna wasanii na Wanahabari Nchini..!!


Posted by Gumzo on January 4, 2014

MTOTO wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein, Maalim Hussein Yahya ametoa utabiri wake wa mwaka na kusema kwamba vifo zaidi vitaendelea kutokea kwa mastaa wa filamu, muziki, waandishi wa habari, viongozi wa dini pamoja na wanasiasa, Risasi Jumamosi linaweka bayana.

[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Akifafanua kuhusu utabiri wake huo, Maalim Hussein alisema kwamba pamoja na vifo hivyo lakini mwaka huu utakuwa ni wa mafanikio kwa baadhi ya mastaa na wanahabari.


"Pamoja na kwamba vifo vitatokea kwa mastaa na wanahabari lakini wapo kati yao watakaopata neema ya uongozi na kuwa watu wakubwa kwa kushika nyadhifa mbalimbali," alisema Maalim Hussein.
Akizungumzia kwa upande wa siasa, Maalim Hussein alisema nyota zinaonesha kwamba kuna kiongozi mmoja kwenye vyama vikubwa vya siasa atavuliwa uongozi ghafla na kutokana na sakata hilo ataanguka na kufariki dunia.
Kama vile haitoshi, Maalim Hussein alisema baadhi ya viongozi wa dini watapata kashfa ambazo zitawasababishia umauti pamoja kuvuliwa uongozi katika nyadhifa walizonazo.
Maalim huyo ameongeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu kutatokea vuguvugu kubwa litakalosababisha mapigano ya jamii kwa jamii na jambo hilo huenda likasababisha vifo.
Mbali na misiba hiyo, Maalim Husseina alisema kwamba mwaka huu kutakuwa na msiba utakaoligusa taifa moja kwa moja na kuongeza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete atafanya tukio kubwa la kutikisa nchi ambalo litaleta neema kubwa kwa jamii.
"Huu ni utabiri wangu kwa mwaka, natarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza mengi kwani haya ni baadhi ya mambo machache kati ya mengi," alisema Maalim Hussein.
Mwaka jana, Maalim Hussein alitabiri kutokea vifo vya baadhi ya mastaa ambavyo vilitokea na kuufanya utabiri wake kutimia.

 
Back
Top Bottom