TANZIA TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) nchini Tanzania, afariki dunia

TANZIA TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) nchini Tanzania, afariki dunia

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God ) Mchungaji Dk. Getrude Lwakatare amefariki dunia Alfajiri ya leo. Mtoto wa amarehemu amethibitisha kifo.

View attachment 1424321

Mtoto wa Marehemu Mama Rwakatare, Mutta Rwakatare amethibitisha kwa kusema

"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu" amesema Muta.

2013, Mama Rwakatare alifiwa na Mumewe, Mzee Kennedy Rwakatare. Zaidi soma TANZIA: Mch. Getrude Rwakatare amefiwa na mumewe

2012, Mama Rwakatare aliichongea JF Bungeni. Zaidi soma Mama Lwakatare aichongea JamiiForums

Tutakukumbuka kwa mchango wako kwenye nyanja za elimu na jamii kwa ujumla.

Umepigana vita na mwendo umeumaliza

Upumzike kwa amani!!
Duh...!. Asante kwa taarifa
RIP Mchungaji Dr. Getrude Rwakatare.
P
 
Pumzika kwa amani Mama Gertrude Rwakatare
IMG-20200420-WA0013.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom